Kikwete baba tunakukumbuka na tunazidi kukukumbuka

Kikwete baba tunakukumbuka na tunazidi kukukumbuka

Kutokana na hizi kauli za " Hawa ndio vichaa tunaohangaika nao" unaweza kusema kweli maisha hapo nyuma yalikuwa nafuu.......lkn kila ukiwaza kuwa CCM ni ile ile basi utajua tu kuwa bado rhumba la maisha halijabadilika.
 
Napenda kutumia mamlaka niliyonayo (sasa hapa usiniulize mamlaka gani, au nimeyatoa wapi, ni siri yangu) kumtawadha ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Baba mdogo wa taifa...
Kumbuka cheo hiki hakipo kwenye katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (msije kusema nimevunja katiba) bali cheo hiki ni ceremonial...
Yani ni kumpa nafasi nyingine tena ndugu JK ya kulitumikia taifa kama mshauri mkuu wa nchi katika maswala mbali mbali yanayohusu welfare ya wananchi kama uchumi, afya n.k huku pia akiendelea kutuwakilisha katika nyanja za kimataifa...
Kumbuka kuwa cheo hiki kimekaa wazi kwa takrabini miaka 16 ikiwa ni tangu alipotutoka baba wa Taifa Mwal JK Nyerere... Maamuzi haya yamekuja baada ya Mh Mwinyi na Mkapa kutoonekana kupendelea tena kujihusisha moja kwa moja na majukumu ambayo alikuwa nayo Baba wa Taifa...
Mungu ibariki Tanzania, nachukua fursa hii kumpongeza ndugu JK kwa majukumu haya mapya niliyo mkabidhi kama 'Baba mdogo wa Taifa' nikitegemea utakitendea haki cheo chako hiki kipya...
 
Dah! Au umetumbuliwa ndio maana unamkumbuka sana jk?
 
Chonde chonde baba yetu sio wote tuliokuona mbaya wengi tunakukumbuka baba. Semasema kidogo tunakufa na hali ngumu ya maisha duu!! Uuwi tunaipata mbaya biashara ndo usiseme haziendi tumenyooka mbaya..
Mna laana ya kumtukana matusi mengi.
 
Wakuu,
Ukweli ni kwamba Mzee wetu kikwete alikuwa ni mtu "Rahimu" na mkarimu sana. Mnyenyekevu wa moyo, Mwenye huruma na ubinadamu wa hali ya juu.Wakati wote alipenda kujishusha kiasi kwamba isingekuwa itifaki na katiba, mtu usingeweza kujua kama yeye ndie alikuwa na amri juu ya majeshi yote nchini. Wala mzee wetu hakupenda visasi wala shari kwa vyovyote vile. Ni nani 'Role Model' wako katika siasa za Tanzania?
Lakini sio siri tulimzodoa mzee wa watu. Aibuuuuu! tukamkejeli kwa kila namna tuliyoweza, mzee wa watu anacheka tu! huku tunaendelea kumdhalilisha bila ya aibu.Mzee wa watu agaugua akafanyiwa operesheni, badala ya kumpa pole tukamzodoa na kumtolea maneno ya kejeli na dhihaka!. Lakini pengine pamoja na kucheka, alikuwa na jambo zito moyoni.

Nafikiri ndio maana akaamua kuwa afanye mbinu ili atufunze adabu na nadhani huko aliko atakuwa anacheka sana tunavyolialia.

Ni maoni yangu kwamba, kama tukiona upo umuhimu, basi wale tuliomkejeli na kumzodoa Mzee Kikwete ni vyema tukamuomba radhi kwa dhati kabisa. Naam , atusamehe ili hiyo dhambi isiendelee kututafuna. Pamoja na hili la kuomba radhi kwa mzee wetu huyu, pia tusememe "Astaghafirullah mara 3", ili Mungu naye atusamehe.

wakuu "Karma ni kweli!"
 
Chonde chonde baba yetu sio wote tuliokuona mbaya wengi tunakukumbuka baba. Semasema kidogo tunakufa na hali ngumu ya maisha duu!! Uuwi tunaipata mbaya biashara ndo usiseme haziendi tumenyooka mbaya..
Ktk wapangaji woote wa pale magogoni, huyu nisingependa lisikia jina lake coz alinicheleweshea maendeleo yangu sehem flani hiv..,
 
Watanzania tulio wengi hatuna ujasiri wa kuwakoromea watawala wetu.

Hivi unadhani Watanzania wanaweza wakafanya uasi wa kupinga watawala waliopo madarakani?

Mi bado sijauona huo ujasiri aisee.
Mbona mi naona kawaida tu ofisi yako IPO bandarini au TRA
 
Magufuli japokuwa nampinga kwenye mambo kadhaa, siwezi sema bora kikwete, huyu hakuwa rais huyu, alikuwa anatawala tu ili mradi liende baasi...leo hii watu nashangaa mnasema mnammiss, napatwa wasiwasi na maono yenu
Chinchilla nilikuona umzuri sura,nikafikiri na akili yako na roho yako ni nzuri pia?,kumbe sheitwain ,yaani nani asiemkumbuka Kikwete? hata mifugo inamkumbuka Kikwete,wakati wake tulikuwa kama tuko Ulaya au Marekani au Tuseme Peponi,sio sasa hivi tupo Jehanamu marabuku,mimi siku hizi hata karanga nazouza mtaani hazinunuliwi kabisa sababu ya Pombe ya Mambodawakali.
 
Tusiwe vigeugeu kiasi hiki huu ni unafiki na uzandiki wa kiasi chake
Bob ni tunda la JK , mapungufu yao yanafanana kwa ujumla wake
JK alikuwa mwanasiasa kuliko mtendaji, bob ni mtendaji hana siasa
JK alisikiliza sana watu, bob hasilizi yeyote
Wote hawa wawili walishindwa kubalance siasa na utendaji
Mshana mkuu,i salute you,.,.,.,.periooooood,umejaza material kichwani mkuu.
 
Siishi kijijini wala simtegemei mtu, na sera ya Magufuli ya kubana matumizi imenisababishia hasara kubwa pengine kuliko hata wewe, lakini sii kitu kitakachonifanya nimuone Kikwete ni bora kuliko Magufuli,
Magufuli ni decisive leader ambaye haogopi kufanya maamuzi
na hata kama yatakuwa na negative impact, mimi naamini afadhali niwe na kiongozi mwenye ujasiri wa kufanya maamuzi hata kama atakosea (kitu ambacho ni human) kuliko yule asiye na maamuzi
A WRONG DECISION IS BETTER THAN INDECISION
Ujue Chinchilla nilichukua picha yako nikaweka kwenye wallet yangu kwa jinsi ulivyonipa raha,lakini sasa hivi naitupa toilet na kuiflash iende na maji taka,na ukizidi kumsema Kikwete nakutumia jini kisoke,chunga sana.
 
Kama mzee mstaafu atuombee tulegezewe kamba

Mulegezewe kamba vipi muendelee kupiga dili kuwadhurumu wanyonge? Hakuna dili, Hakuna escrow, Hakuna lugumi, Hakuna tenda na hakuna kulimbikiza kodi za nyumba mpaka kufukia mabilioni. Mwenye kuikumbuka serikali ya Kikwete ni mtu mwenye kupongeza wizi, ufisadi, ubinafsi na asiyependa haki kwa wote. Sasa nikufanya kazi tu, there is no short cut. SERIKALI ya nne imetutia hasara kubwa, waliofaidika ni wachache na ndiyo wenye kuliA. Mwacheni Kikwete apumuzike aangalie makosa yake.
 
Chonde chonde baba yetu sio wote tuliokuona mbaya wengi tunakukumbuka baba. Semasema kidogo tunakufa na hali ngumu ya maisha duu!! Uuwi tunaipata mbaya biashara ndo usiseme haziendi tumenyooka mbaya..
Utakumbuka hadi marehemu siyo muda wa kukumbuka Giza lilopita tuangalie Giza lililopo
 
Pumzika Salama bb n dn yako tu ilikuponza lait haya magumash ya ss yangefanyika wakat wako ungeckia matamko kla mahali lkn kwa kuwa mwenzao wapo kmya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom