Kikwete baba tunakukumbuka na tunazidi kukukumbuka

Kikwete baba tunakukumbuka na tunazidi kukukumbuka

Ila Mgufuli bado unampenda...ingawa njaa kakuletea..uwongo?

Yaani huyu baba acha kabisa, kaduka kangu kalikuwa kanazungusha angalau mahitaji ya nyumbani yalikuwa yanaendeshwa na duka, sasa nikakuta nyumbani ndio kunaendesha duka lol! Ni rais wangu nitafanyaje sasa, kama nilivyosema awali naamini ni kipindi cha mpito tu
 
Yaani wengine hatuoni kabisa tofauti ya aliyepita kwa sababu hatujawahi kupiga madili hatukuwa tunaishi kijanja kijanja tuliishi kwa vipato vyetu harali sasa nyie mliozoea mamillion acha muisome namba
 
Yaani huyu baba acha kabisa, kaduka kangu kalikuwa kanazungusha angalau mahitaji ya nyumbani yalikuwa yanaendeshwa na duka, sasa nikakuta nyumbani ndio kunaendesha duka lol! Ni rais wangu nitafanyaje sasa, kama nilivyosema awali naamini ni kipindi cha mpito tu

Ukipenda chongo unaita kengeza
Hata hali isipobadilika nna uhakika utampigia kura 2020 arudi tu aendelee kutuletea njaa ha haaa...
 
Miezi tisa iliyopita mulimuona hafai na legelege kumbe alikuwa akiwahurumia.
Kikwete mjanja sana alicheza karata nzuri.
Alijua kabisa yeye mwenyewe kaharibu sehemu nyingi tu, sasa akaona awaletee mtu atakae haribu zaidi kuliko yeye na kuwafanya mumkumbuke.

Ama hakika Magufuli amefanya JK aonekane alikuwa ni bonge la raisi.
 
Si mmetuambia kuwa Magu ni chaguo la Che Nkapa na alipigiwa kura na wa NEC waliokuwa wafuasi wa Lowassa kumkomoa Jk?
 
Si mmetuambia kuwa Magu ni chaguo la Che Nkapa na alipigiwa kura na wa NEC waliokuwa wafuasi wa Lowassa kumkomoa Jk?
Asee nimetumia zaidi ya dakika 10 nikisoma kwa kurudia rudia hii reply yako umeandika nini na inataka nini lakini nimetoka kapa... yaani sijaelewa kitu.
 
Asee nimetumia zaidi ya dakika 10 nikisoma kwa kurudia rudia hii reply yako umeandika nini na inataka nini lakini nimetoka kapa... yaani sijaelewa kitu.
Kama hujaelewa unaachana nayo unafanya ishu zingine, Hilo swali sio Compulsory kuwa lazima uelewe au ujibu kama vile upo Kwny Mtihani!

Interval ya mimi ku post na wewe ku reply ni chini ya dakika kumi lakin wewe umeweza kutumia zaid ya dakika 10 kuisoma kabla huja reply!!
 
Kuna hatari ya nahodha na nahodha mstaafu kupigania usukani chombo kikenda mrama.

Kwanini wananchi wanajiona hawawezi kusema wenyewe mpaka awasemee Kikwete?
Hizo ndio products zake Kikwete, kwamba mwananchi hawezi kujitegemea hata kwa jambo dogo kwa kufanya kazi mpaka atafute wafadhili. Hawezi kujitetea/kujieleza kwa lolote mpaka waseme viongozi.
 
Mkuu vipi kuhusu maisha ya mtanzania kwa sasa je utalinganisha maisha yalivyokuwa kipindi cha JK na sasa? miezi tisa tu hii majanga je huko tunapoelekea?? nadhani hali iliyopo kwa sasa wewe haikugusi kabisa mkuu hakuna unafuu sana sana wananchi tunakufa njaa tu.
Hali ni ngumu sana kwakweli.
 
Hizo ndio products zake Kikwete, kwamba mwananchi hawezi kujitegemea hata kwa jambo dogo kwa kufanya kazi mpaka atafute wafadhili. Hawezi kujitetea/kujieleza kwa lolote mpaka waseme viongozi.
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Habari ya Watanzania kutegemea sana viongozi ilikuwepo tangu enzi za Baba Kabwela.
 
Ivi wana ccm wanashabikia uongozi uliopo kunanini nyuma ya pazia kuna ka neema wanapata zaidi au maana hali ilivyo ngumu bado mtu anashabkia hali ngumu. Na hali iko wazi mwelekeo hauonekani kabsaa. Sasa mashabiki wa ccm ni akili yakuchambua mambo hamna au kuna mgao mnaupata

Kila kitu ni sawa kila kitu mzee akiongea hakikoselewi au kwasababu jamaa kajivika u mungu hamuwez mkosoa.

Sasa ni adabu za uoga....Ngoja kamba ilegezwe utashangaa zile adabu zimeishia wapi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom