Kikwete azungumza na Dirk Kempthorne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete azungumza na Dirk Kempthorne

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masaka, Jun 4, 2008.

 1. M

  Masaka JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 437
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Daily News; Wednesday,June 04, 2008 @00:03

  Rais Jakaya Kikwete jana alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani, Dirk Kempthorne kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Arusha (AICC) mjini Arusha.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete alimweleza Waziri Kempthorne kuhusu juhudi ambazo Tanzania inafanya katika kuhifadhi na kulinda mbuga zake za taifa za wanyama.

  Rais pia alimweleza waziri huyo juu ya mafanikio ambayo Tanzania imeanza kuyapata katika kupambana dhidi ya ujangili katika mbunga zake za wanyama. Waziri huyo anamwakilisha Rais George W. Bush na kuongoza ujumbe wa Marekani kwenye Mkutano wa Nane wa Sullivan uliofunguliwa juzi usiku na Rais Kikwete katika Ukumbi wa Simba wa AICC.

  Baada ya kukutana na Waziri Kempthorne, Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na mpigania Haki za Binadamu hodari na mwanasiasa wa Marekani, Mchungaji Jesse Jackson. Mkutano huo pia ulifanyika katika Ukumbi wa AICC.

  ....

  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=9435
   
 2. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  wengine wanapigania vyama, kwi kwi kwi ! wengine wanarithishwa vyama na wakwe zao !
   
 3. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Baada ya kusoma story hii mbona sioni kuipigania nchi kokote? Kukutana na Kemptone na Jesse ndio kupigania nchi? I don't think so...
   
 4. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ulitaka ashike mkuki ndio ujue anapigania nchi??
   
 5. C

  Chief JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa. Si lazima ashike mkuki. Naona anapigania nchi katika mapambano dhidi ya ujangili katika mbuga zetu za wanyama:)
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nasapoti juhudi zozote za kuinasua nchi kutoka ktk lindi la ufukara na matata yanayiokabili...
  Kama anaipigania kwa mema ni budi kumpongeza ila kama ndo ile kutaka kujulikana basi tumekwisha
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2008
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  wewe nawe tumekuchoka na vioja vyako. Unajua tunaweza kukutoa duniani, au haujui ya kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu we endelea. Tutakukabizi rasm kwa mpenda haki siku moja akushungurikie
   
 8. Typical

  Typical JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 261
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hapo JK anachofanya ni kuitangaza nchi ili watalii waongezeke na pato la taifa likuwe!!!

  But kama anapigania nchi as you say "masaka", angedili na hawa wezi(mafisadi) basi wanaopita na hizi fwedha pindi zinapoingia serikalini???mbona yuko kimya.?

  Bado nna dought naye!!!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Katika habari nzika sijaona ambapo inaonyesa JK anapigania Nchi .Naomba mwongozo wa mleta hoja tafadhali .
   
 10. m

  mapambano JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu yuko kwenye ile listi of shame...sina uhakika nayo hii
   
 11. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hii naona tumuachie kadaMpinzani na Masaka wadiscuss
   
 12. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Anapigania ujangili katika mbuga za wanyama?? ama anavutia watalii wakuja lala kwenye hoteli yake na shemejize ya kitalii aliyo ijenga kwenye mbuga zetu??

  Ndo maana sitoshangaa marekebisho ya mikataba ya madini yanakuja na sera za kuwanufaisha watafiti zaidi kuliko wawekezaji! ( refer Sinclair)

  Hakuna jambo analolifanya JK la kuipigania nchi, nyuma ya pazia daima katika move zake ni kuipiga nchi ama kwa kulinda fisadi wenziwe ama kujitengenezea mazingira ya faida zake binafsi!

  Haipiganii nchi bali anaipiga kwa hakika, na tusipo simama kidete, makonzi yake yaweza idondosha milele.
  Ee maulana tusaidie!
   
 13. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kweli kila ngoma ina mchezaji wake, na jinsi tunavyoendelea kujadili tunapoteza muda wa kujadili EPA na mengineyo, na muda unaenda na wao wanapeta wanakua wametimiza matakwa yao
   
 14. Mzozo wa Mizozo

  Mzozo wa Mizozo JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2008
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 427
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi kaamua pigana katika Sekta ya Wanyamapori kwa kueleza kuna pundamilia na swala na tembo wenye masikio makubwa wangapi sasa hapa Tanzania.

  Mbona sioni kama anapigania nchi kwa kupambana na Mikataba Mibovu ya Madini ambatyo inaliingiza taifa gizani katika Bottomless Pit!

  Mbona sioni kama anafanya lolote kupigana dhidi ya Mafisadi ambao kafanya juhudi zote kuhakikisha ya kwamba anawakumbatia na kuwalinda kwa uwezo wake Wote akiwa kama Rais wa Jamuhuri?

  Tuongelee hao.
   
 15. C

  Chief JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nilitaka "kumuunga" mkono kada kuhusu kuwa hatuna haja ya kuona JK ameshika mkuki kujua kuwa anapigania nchi, isipokuwa ni katika masuala ya ujangili kutokana na mada yenyewe. Hapa ameona kuwa JK kweli anapigania nchi.
   
 16. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  just deal with it !
   
 17. M

  Masaka JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 437
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na sasa Kikwete amekwenda UK kutetea masilahi ya nchi na amewakoromea wazungu kwa matatizo ya uchumi. kiongozi gani afrika anayeweza kuwakoromea wazungu?

  Hongera kikwete kwa kuleta maendeleo ya Tanzania!
   
 18. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Self serving submissives stupidly supporting a succiduous suicidal stagnant stupor succès de scandale styled staled state.
   
 19. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  itabidi sasa tuwekewe kamusi!maana kazi kweli kweli!
   
 20. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2008
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Pls, layman language(plain English)....inakuwa unatupa kazi kila mara kuangalia dictionary hayo ma jargon yako ni mazito......leave it for crosswords puzzle
   
Loading...