Daily News; Wednesday,June 04, 2008 @00:03
Rais Jakaya Kikwete jana alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani, Dirk Kempthorne kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Arusha (AICC) mjini Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete alimweleza Waziri Kempthorne kuhusu juhudi ambazo Tanzania inafanya katika kuhifadhi na kulinda mbuga zake za taifa za wanyama.
Rais pia alimweleza waziri huyo juu ya mafanikio ambayo Tanzania imeanza kuyapata katika kupambana dhidi ya ujangili katika mbunga zake za wanyama. Waziri huyo anamwakilisha Rais George W. Bush na kuongoza ujumbe wa Marekani kwenye Mkutano wa Nane wa Sullivan uliofunguliwa juzi usiku na Rais Kikwete katika Ukumbi wa Simba wa AICC.
Baada ya kukutana na Waziri Kempthorne, Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na mpigania Haki za Binadamu hodari na mwanasiasa wa Marekani, Mchungaji Jesse Jackson. Mkutano huo pia ulifanyika katika Ukumbi wa AICC.
....
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=9435