Elections 2010 Kikwete azomewa Mwanza!

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
284
482
Ndugu wana-JF mlioko Mwanza, nimepigiwa simu dakika tano zilizopta 06:30 hivi na jamaa yangu aliyeko mitaa ya Nyegezi jijini Mwanza kwamba msafara wa Kikwete umepita eneo hilo ili nisikilize live makelele ya jinsi anavyozomewa.

Jamaa yangu ananiringishia kwamba pamoja na kwamba nimesikia kelele lakini sijabahatika kuona jinsi anavyonyooshewa alama ya vidole viwili (V).

Mlioko Mwanza tujulisheni zaidi.
 
Kama ni kweli, basi imekaa vizuri! Na ninawapongeza watu wa Mwanza kwa ujasiri huo. Hawana unafiki wa kujipendekeza kama wale wa mikoa ya kusini.
 
Kama walikuwa wanamtazama dr wa ukweli kupitia tbc1, wameshafanya maamuzi, lakini naomba wasizomee kwani watasababisha fujo
 
Tena bado mwanza napajua sana, wamwabie asiende milimani kwetu, kuna watu hawaogopi kufa huko. Hata Masha hawezi kwenda sehemu kama Bugarika, Mahina, Bugando milimani huko nikibano tu. Acha ujumbe ufike.
 
Mwisho wa ufisadi ni huu hapo..........Anapozomewa JK ujue ............it is all over.................
 
Kikwete, kwa kweli afadhali atulie tu. Maana kama watu hawamtaki tena, sasa anataka kuwa rais wa nani tena? Kwa kweli hata ikitokea miujiza akashinda atapata shida kubwa sana kutawala afadhali hata kushindwa. Wamshauri jamani mzee huyu atulie tu. Urais ndo huo unamtupa mkono; na haurudi tena. Pole yake. Alichezea dhamana ya miaka 5 aliyopewa na watanzania. Majuto ni mjukuu.
 
Mwanza ndivyo walivyo, Wakiamua jambo lao hata malaika ateremke toka mbinguni hawamsikilizi. Nyerere aliwashindwa tena wakati wa njaa akiwahimiza kulima mtama wakakataa na kwenye hotuba yake mwaka 1980 pale Nyamagana aliishia kuwatukana kwamba "waskumuma mmekataa kula ugali mwekundu".

Mwaka 1985 Paulo Bomani aligombea Mwanza akashinda. Akafanya kosa la kuhamia Dar badala yake akaporomosha bonge la jumba pale pembeni ya katikati ya shule ya Nyakabungo na Lake Secondary jirani na Mama Matemba.

Mwaka 1990 wana-Mwanza wakasema hata akigombea na shetani basi watampa shetani. Akaibuka mgombea asiyejulikana aitwaye Paschal Kulwa Mabiti. Akamchakaza Bomani licha ya kujulikana kwamba aligombea uhuru, alianzisha Nyanza Cooperative Union.

Kunanguka huko hata Nyerere kwamba wana-Mwanza wamemuondoa Bomani kwa kura ya chuki.

Kikwete anawajua vizuri wana-Mwanza. Mwaka 2005 wakati anagombea ndani ya CCM wajumbe waliokuwa wanawasili Dodoma walikuwa wanapokelewa na kila mgombea. Walipokuwa wanafika Kigoda, Salim, Malecela, Sumaye na kila aliyegombea alikuwa anaenda kwenye basi au stesheni kuwapokea.

Treni ya Mwanza ilipofika Dodoma wana-Mwanza walikataa kupokelewa na mgomea yoyote na walibaki wakiimba "sisi ni JK tu hatutaki mwingine". Kigoda aliondoka kimyakimya na Dodoma nzima ilijua kuwa ni JK tu licha ya kwamba NEC ilikuwa bado haijachagua majina matatu.

Walipobaki JK, Mwandosa na Salima kundi hili la Mwanza ndilo lililosababisha hata kule Chimwaga (UDOM ya sasa) kumwage wanajeshi wa JWTZ wala siyo FFU wakihofia wataleta vurugu kama Kikwete angeshindwa. Msishangae JWTZ kumwagwa sasa hivi. Tulioona Dodoma ile 2005 hatushangai, tena wakiwa wao kwa wao CCM.

Hivyo Kikwete anajua tabia hii ya wana-Mwanza. Anajua walivyomuinua, anajua watakavyomtikisa.
 
kIKWETE SASA sijui atarudi tena temeke , maana huku nako Slaa kafanya kufuru Mwembe Yanga
 
Ooh hakuna haja ya kumzomea wanamwanza, tumwage tu kwa amani hapo j/pili 31. Tukimzomea anaweza kuona aibu kuondoka ikulu na kumwagiza Abuu Shimbo kuifanyia vurugu katiba.
 
Leo kulikuwa na mikutano miwili yenye mvuto sana jijini Mwanza.Wagombea ubunge wawili mh Wenje wa CHADEMA jimbo la Nyamagana akiwa viwanja vya Mirongo na mh.kikwete CCM mbunge hasiye na jimbo maalumu akiwa viwanja finyu vya Sahara.
Hali ilikuwa hivi kule kwa kikwete mbali na kusomba watu toka mikoa jirani watu walikuwa si wengi sana.huku kwa wenje wananchi wenye mapenzi mema walikuwa wamejaa.Baada ya wenje kumaliza kampeini ikapita helkopita ya Kikwete jirani na Wenje.kazomewa sanaaaa. Baada ya Kikwete kufika Sahara kakuta watu wa kawaida tu. Kama kawaida kaanza "ccm oyee!"walioitikia ni wale waliokuwa wamevaa tshirt za ccm tu.alivyoanza kuongea tu wale waliokuwa hawajavaa nguo za ccm wakaanza kuondoka.

Maandamano ya wenje yalitia Fola mno. Waandamanaji kama kawaida wakiimba "tumechoka na Mafisadi"

Ajabu ni kuwa imagine mgombea ubunge anapimana nguvu na mzee wa kaya na watu wakawa sawasawa. Masha hoiiiiii. Yaani anazomewa kila apitapo.
Habari ndo hiyo.
Source ni mimi mwenyewe.niko foot step kutoka maeneo ya tukio hadi hivi ninavyoandika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom