Hii ni dalili ya watu kuchoka, mishipa ya damu ya CCM inaendeshwa kwa nguvu ya pesa, uhai wa wanachama wake kwa miaka miwili ijayo utategemea pesa zaidi ya mapenzi. Tabia hii inakuzwa na viongozi wenyewe, siku hizi mwanachama hawezi kuhudhuria mkutano bila kupewa pesa na kuhakikishiwa usafiri wa kwenda na kurudi, chama hakiendeshwi hivyo hiyo ni dalili mbaya kwa uhai wa chama.
Hata kama chama kina uwezo kiasi gani ni vizuri mwanachama wa chini akashirikishwa kukichangia,tunaona kwenye mikutano ya Chadema huwa wanapita na vikofia kichangishana hiyo si kuwa wanatemea sana pesa hiyo ili waendeshe chama kwa vile sidhani kama huwa wanapata kiasi kikubwa lakini hata kama mtu atatoa sh.200 bado atajiona ni mmoja wao.
Tunaona hata vyama vya ulaya pamoja na utajiri wao kama Democrats, Reps, Conservative, Labor nk lakini bado huwa vinapitisha bakuli kwa wanachama wake. Nionavyo mimi CCM inajiua yenyewe, ninavyosema hivyo si kwamba itakufa mwaka huu lakini haina muda mrefu.