Kikwete azomewa Mbulu

............kilichowaudhi wasikilizaji ambao kwa kweli walikuwa wengi ni kusema kuwa yeye JK na sisim ni original na Dr Slaa ni photocopy. kwa vile kuguna hakukusikika vizuri walianza miluzi na mkuu akashuka na kuondoka. Pamoja na hayo watu walikuwa wakiimba peoples power kwa shangwe na polisi walitupa bomu la machozi ili kuwatawanya jumla watu kwani giza lilianza. hii itamnyima zaidi kura kwani waliopatwa na bomu hili ni miongoni mwa wale ambao wangempa kura.

kwa ujumla baada ya tukio hilo na watu kuosha nyuso zao walijipongeza sana kwa kufikisha ujumbe.

Sasa watu wanamsubiri katika miji midogo ya Dongobesh na Haydom maeneo wanayomchukia sana Marmo. Mahudhurio yanatabiriwa kuwa siyo mabaya na wala siyo kwa kutoa kitu. Tunaaminini hatarudia kosa la Mbulu tena
 
Chanzo cha habari..>???

Kuna magazeti ambayo huwa hayamung'unyi maneno na ndio walioandika habari hiyo (Gazeti la Mwananchi).

Soma hapa: CCM yakataa ombi la Spika Sitta

Vipande vya habari hiyo vinasema hivi:

... Hayo yametokea wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete akizomewa na kikundi cha watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa Chadema wakati akihutubia wilayani Mbulu.

Kutoka Mbulu, habari zinasema kuwa wakati Kikwete akihutubia mkutano wake wa mwisho mjini Mbulu, kikundi cha watu kilichokuwa upande wa pili wa uwanja kilikuwa kikipiga miluzi na kuzomea, ambayo ilionekana kuudhi wafuasi wa CCM.

Kutokana na kucheleewa kufika Mbulu, Kikwete alihutubia kwa dakika chache na baadaye kumtambulisha mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Phillip Marmo na baadaye kumaliza mkutano huo.

Mheshimiwa Njiwa nadhani umepata taarifa kamili. Kama watu walizomea kiasi cha wengine kusikia, basi ni kwamba hiyo zomea zomea ilikuwa kubwa ya kutosha. Labda ndio maana alihutubia kwa dakika chache, akichelea kuzomewa zaidi na hivyo kutoa aibu.

Tatizo la majimbo yote ambayo walichakachua matokeo, CCM wamejiwekea upinzani wao wenyewe. It is very unfair kupitisha jina la mtu mwenye kura 2000, halafu unamwacha aliyepata kura 6000 au zaidi. So, CCM wajiandae kwa kura za chuki. Pia madai kwamba hao waliozomea ni wafuasi wa CHADEMA yanaweza yasiwe ya kweli, ni CCM hao hao ambao mgombea wao (kwenye kura za maoni) alikatwa jina ama alifanyiwa mchezo mchafu na hivyo wanamtumia ujumbe Mwenyekiti moja kwa moja. Ujumbe umefika, next time CC na NEC watachakachua matokeo kwa uangalifu zaidi na siyo kutoa sababu za kijinga kama uraia au uchanga wa kisiasa na nyinginezo.
 
Watu walihudhuria mkutano wa JK katika jimbo la Mbulu leo 17/09/2010, walimzomea mgombea huyu baada ya kuanza kuisemea Chadema vibaya. Walianza kwa kupiga miluzi huku wakiondoka katika mkutano huo wakati JK akihutubia. Polisi walijitahitahidi kuzui watu lakini hawakufanikiwa.

Hali hiyo ni mwendelezo wa wa zomea zomea inayoikumba mikutano ya CCM katika jimbo hilo la Mbulu. Akiwa Haydom Mgombea wa ccm Philip Marmo alizomewa na kuachwa huku DC akiamuru polisi kuzuia watu waliohudhuria wasiondoke lakini ilishindikana.

Mbali na Hilo Hata kule Arusha katika uwanja wa Amri Abed JK alichelewe kuingia alifika uwanjani saa kuna mbili kasorobo na wana CCM walikuwepo kwa uwanja tokea saa nne asubuhi, Na pia wakati alipo anza kuhutubia na watu wakawa wanatoka taaratibu na kinachosemekana ni kuwa kilichosaidia ni kuwa njia za kutokea uwanjani ni zilikuwa ni milango midogo na ingekuwa yale ma gate makubwa yako wazi kweli angebaki akihutubia wana CCM tu maana wananchi walienda kuangalia wasaniii na ndio mbinu CCM walio itumia kuwavutia watu kuja kujaza viwanja tuuu, Nasikia TOT nayo imeshiwa kabisa wanafunikwa na vijana wa Kizazi kipya.

Hiyo ni hali halisi tu kwa mtazamo kuwa ndani ya CCM kuna makundi makubwa na si kidogo na sio swala la kubeza kama wanavyosema wana CCM wao wenyewe, ita wagharimu sana kurudisha hayo makundi karibu na ndio maana nashanga kila mikutano ya JK kwanza Ridhwani utakuta ametangulia hapo lazima tujiulize kwanini?? na ukija chunguza wagombea wengi walichaguliwa kwa kura za maoni wameingiza watu wao katika kampeni zao na sio wanachama husika wa CCM na utakuta wanachama wengine wametengwa ambao ndio wanao takiwa pambana na unakuta ndio wana nguvu ya kuwavuta wapiga kura. na hapo ndipo utakuta makundi kunao waliokuwa wanataka wagombea wao kama Iringa mjini,Nyamagana,Nzega,Arusha mjini, na kadhalika.

Mi nadhani ile dhana ya vigogo wa CCM waondio kauli ya mwisho wajaribu kuhisahau iyo dhana maana wakati unabadilika na muda unakwenda pia hawawezi zuia mvua kunyesha na muda huo unakalibia na sio zaidi ya miaka 2 ijayo kuta kuwa na mabadiliko makubwa sana kutokea UVCCM kuja ngazi za juu CCM

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo atafanya mikutano ya kampeni Wilaya za Mbulu, Hanang na Babati.
Mkutano wa Kwanza wa kampeni utafanyika Kata ya Dongobesh wilayani Mbulu ambapo Mheshimiwa Kikwete jana amemalizia kwa mkutano mkubwa wa kampeni.
Baadaye msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Hydom wilayani Mbulu.
Kutokea Hydom msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaendelea Wilaya ya Hanang; Basotu, Katesh na Endasaki.
Mheshimiwa Kikwete atamalizia mikutano yake ya kampeni kwa siku ya leo Wilayani Babati ambapo atafanya mikutano ya kampeni Dareda na Babati.

SOURCE: Blog ya Kampeni ya Kikwete 2010

Hiyo taarifa ya Mbulu Mjini haikuandikwa kwa sababu zao wanazozijua. Laiti Tanzania nzima ingekuwa kama Mbulu ya miaka ile na sasa.
 
sasa ni wzi watz wamechoshwa na danganya toto wamekuwa watu wazima kwa hiyo hawako tayari kunyamazishwa kwa kuahidiwa pipi..............kikwete bwana kazi kujaza tu maahadi wakati ile ahadi yake na falsafa yake na aliyoiamini mwenyewe ameamua kuikataa baada ya kuwadangaya watz kuwa maisha bora kwa kila mtz.....sasa haisemi tena kwani ni hukumu yake kubwa
 
nimeongewa na baadhi ya watu, wanasema pia WATU wa BABATI wanamsubiri kwa hamu kubwa, ili wafanye kama walivyofanya wenzao wa mbuli.
 
Jakaya Kikwete akizomewa na kikundi cha watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa Chadema wakati akihutubia wilayani Mbulu

sasa nyinyi mlitarajia nini?[/B]
 
Babati sio ndiko kwa wagombea wa mizengwe Chambiri na Jitu Patel? Kuna kazi mwaka huu.
 
Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo atafanya mikutano ya kampeni Wilaya za Mbulu, Hanang na Babati.
Mkutano wa Kwanza wa kampeni utafanyika Kata ya Dongobesh wilayani Mbulu ambapo Mheshimiwa Kikwete jana amemalizia kwa mkutano mkubwa wa kampeni.
Baadaye msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Hydom wilayani Mbulu.
Kutokea Hydom msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaendelea Wilaya ya Hanang; Basotu, Katesh na Endasaki.
Mheshimiwa Kikwete atamalizia mikutano yake ya kampeni kwa siku ya leo Wilayani Babati ambapo atafanya mikutano ya kampeni Dareda na Babati.

SOURCE: Blog ya Kampeni ya Kikwete 2010

Hiyo taarifa ya Mbulu Mjini haikuandikwa kwa sababu zao wanazozijua. Laiti Tanzania nzima ingekuwa kama Mbulu ya miaka ile na sasa.

Mbona kote twasikia JK anahutubia sio zaidi ya dakika 20? na utakuta hapo wana CCM walisha fanya maandalizi ya kufa mtu gharama kibao muda wa wanachama wa CCM unaishia kumsubili mgombea na akifika tu unakuta watu wamenuna kama nini sijui oooh JK anachelewa sana.

Je anafuata kanuni na sheri za uchaguziiii? anahutubia katika muda muafaka ??? Je wananchi kwa Ujumla na wana CCM wanaridhika na Hotuba zake za 20min??? Je afya yake iko poa au anakua katika hali ya uchovu???

Na je ataweza toboza next 4 yrs kwa hali yake ya kiafyaaaaa???

Sasa polisi wazuie watu wasiondoke jmaaaaaaaaaaaaaa vipi?
Video clip pls
 
hao watu wanaozuiwa kuondoka mkutanoni ni wale waliofadhiliwa na chama. inawezekanaje kuwalazimisha watu wakusikilize?
 
Hivi mkuu hakudondoka wakati anazomewa? au wapambe walimshikilia? Maana ana mgogoro mkubwa kiafya na kisaikolojia!!
 
Lizomeeniii!!!Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,Lichekeni haaaaaaaaaaaaa,haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!
:becky::becky:
 
Back
Top Bottom