Mzimu wa marehemu Aquilina waendelea kuwatesa viongozi wa CHADEMA

Abdalah Abdulrahman

Senior Member
Aug 29, 2019
137
250
Baadhi ya viongozi wa siasa huwatumia wananchi kama inavyotumika karatasi ya chooni (toilet paper) au mshumaa kwa malengo ya kuwasaidia kusafisha mabaya yao,kuwasafishia njia,kuwapa mwaga huku wakiwaacha wanachama wao wakiteketea.

Ninasema hivyo kwani ni Chadema iliyowadanganya wanachama wake wadeki na kutandika kanga barabarani ili wabunge na madiwani pamoja na mgombea wao wa uraisi apite kipindi cha uchaguzi,baada ya uchaguzi manufaa yote waliyopata ya ongezeko la ruzuku,mfuko wa jimbo,mafao,mikopo nakadhalika, hakuna hata kitu kimoja wanachama waliambulia,maeneo waliyoyaongoza viongozi hawa yamebakia hayana maendeleo kwa ubinafsi wao wa kuangalia maslahi yao na ya familia zao kwanza.Ni viongozi wa Chadema waliowashawishi wanachama wao waandamane na kuwapiga mawe polisi,waliokamatwa hakuna hata kiongozi mmoja wa chama alieenda kuwatembela na kuangalia familia zao.

Mifano hii na mingine inaturejesha katika kisa hiki cha uchungu cha kupotea kwa maisha ya ndugu yetu Aquilina katika vurugu zilizoanzishwa na wafuasi wa Chadema. Baada ya kufariki kwa binti Aquilina,serikali ilichukua jukumu la kuusitiri mwili wa marehemu na kuwafariji wazazi na walezi wa Aquilina.Hakuna kiongozi yeyete wa Chadema ambaye aliwahi kufika katika familia ya marehemu na hakuna pesa au mchango wowote aliyowahi kupelekwa kwenye familia ya marehemu.Michango iliyochangwa kwa ajili ya zoezi hili iliishia kwa viongozi wachache ndani ya Chama.

Bado haifahamiki kuwa ni waandamanaji wa Chadema walimuua binti huyu pale walipokuwa wakiwarushia mawe polisi,risasi iliyotoka kwa mwandamanaji mwenye silaha au ni risasi iliyotoka kwa polisi ndio ilimuua binti huyu.Ukweli utafahamika tu,lakini tufahamu kuwa nafsi yeyote inayouliwa kwa dhuluma haiondoki bila kuacha athari kwa wale walioidhulumu.Hivyo basi mzimu wa kifo cha Aqulina pamoja na utekaji wa wanachama ndani ya Chadema unaolenga kujinufaisha kwa watu wachache kisiasa utaendelea kuwasumbua viongozi wa Chadema mpaka watakapotubu juu ya dhambi hii na zingine wanazowafanyia Watanzania.Hii inadhihirika katika hoja zifuatazo:-

1. Kushindwa kwenye chaguzi za marudio na za serikali za mitaa
Chadema imeendelea kudhoofika kama sio kufa katika maeneo ya mijini ambapo ilikuwa na nguvu kupitia UKAWA,hii inadhhirika kutokana na matokeo ya chaguzi za marudio katika maeneo mbalimbali ambazo wananchi wamechagua viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa zaidi ya asilimia 90% .Chadema pia imeendela kupoteza mvuto kwa wanachama wake wachache kwa kitendo cha kususia uchaguzi wa serikali za mitaa.Wanachama wameingiwa na wasiwasi na kupelekea kutojiandikisha na wale wengi waliojiandikisha kuazimia kutorudia tena makosa ya kuwachagua viongozi ambao ni wabinafsi wasio na uzalendo na nchi yao.

2. Zomea zomea ya Viongozi wa Chadema
Haikuwahi kutokea mpasuko uliopelekea wanachama kuzomea viongozi wao ndani ya chama,hasa kiongozi mkubwa kama Mwenyekiti wa chama.Hii inaendelea kudhibitisha mzimu wa Aquilini unawatafuna viongozi kutokana na zomea zomea zinazoendelea katika mikutano ya Chadema.Ni hivi karibuni tu Mh Freeman Mboe alizomewa na wanachama wake katika jimbo lake huko Hai wakimtaka aeleze alichowafanyia wananchi katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi wake,na baada ya kushindwa kueleza akahairisha mkutano.

3. Mkosi ya kunusurika kufungwa
Ilibakia alimanusra viongozi wote wa Chadema kwenda jela kutokana na kutiwa hatiani kwa jinai waliyoifanya.Chadema ilitumia tukio hili kujinufaisha na kutenda makosa mengine kama kutakatisha fedha nakadhalika.Tukio hili limeacha dowa kuwa kwani mchakato mzima wa ukusanyaji wa pesa hizi uligubikwa na usiri mkubwa wenye nia ovu ya kupiga hela na kutakatisha pesa chafu.

4. Mkosi inayopelekea kuvunjika viungo
Baada ya wanachama wa chadema kufanyafujo ndani ya Gereza kwa kutaka Mwenyekiti kutolewa bila kufuata utaratibu huku wakimiminia askari magereza matusi kama walivyo wamiminia askari polisi siku ya hukumu ya kesi ya viongozi wa chadema,ilitokea sintofahamu ambyo ilisababisha kuumia kwa viongozi hawa wa chma.Baadhi ya watu waliokuwepo katika eneo la tukio wanasema Halima mdee pamoja na Ester Bulaya waliangukiwa na kundi la wanachama waliokuwa wakiwakimbia askari magereza.

5. Kukusanya wanachama wao ili wawauwe kwa Korona
Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mboe anawahadaa wanachama wake kukusanyika licha ya kuwepo kwa ugonjwa wa Korona amabo unapinga mikusanyiko.Lengo kuu ni kuleta taharuki ya maambukizi mapya kwa Watanzania ili waweze kukusanya michango ya misiba kwa ajili ya kampeni za mwaka huu.

Chadema kama chama kinatakiwa kujitahmini juu ya kutumia damu za watu kufikia malengo yao ya kisiasa.Seriakali inatakiwa kuhakikisha kila jambo wanalofanya Chadema lina mustakabali mwema na nchi,sivyo kutumia kila rasilimali iliyopo kulizuia kwa manufaa ya nchi

Mungu ibariki Tanzania
 
TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,047
2,000
Hata kama mna gangia tumbo kuna muda akili inagoma kabisa. Hivi kweli Kuhusu yule Binti wawatu alouliwa na mapolice unadiriki kuwalaumu chadema? Hebu Kuwa na hofu katika mambo unayofikiria hata kama ndo kutafuta kula ila sio kiivyo. So waungana na wale walosema risasi ilikata kona ikapita kwenye daladala ?
 
Masanjaone

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
848
1,000
Dam ya akwirini inawatafuna CHADEMA.
We angalia saivi tuna gonjwa la CORONA mbowe anatangaza mikutano ! Kama cyo raana ni nini?
2. Wabunge na madiwani wanahama chama kila siku mbowe anaomba maridhiano je! Kama cyo raana ni nini?

DAM YA MTOTO AKWIRINI INAWATAFUNA CHADEMA NENDENI KWENYE KABURI LAKE MKAOMBE RADHI.
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,100

Nchi haina maabara ya kupima corona, mko bize mnapambana na chadema, mapimbi nyie!
 
Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,148
2,000
Hvi una akili timamu unapouliza nani alifyatua risasi iliyomuua Akwiline ?, (RIP),

Inawezekana na kule kwa Daudi Mwangosi mtakuja kusema Chadema ndio waliomuua,

Kati ya Chadema na seriklai ni nani anaeua watu hapa nchini ?,
Hivi mwaka 2019 kulifanyika Uchaguzi wa serikali za mitaa, ??.
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,561
2,000
Abdalah Abdulrahman, Kama watetezi wa propaganda za chama waliopo katika timu ya Polepole, na mmojawapo ni wewe Abdalah, basi kuna kila sababu ya chama tawala kuendelea kupata tafu ya nguvu na hata kuzidi kubebwa na vyombo vya dola ili kiweze kukabiliana na hoja za vyama vya upinzani na hasa CDM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,970
2,000
Wadau jibuni hojaaaaaaaa,acheni mipashoooo
Mbona kesi ya mauaji iliondolewa Na jalada DPP wenu alilifunga.
Ganda la risasi uonyesha mmiliki wa silaha Mbon mmeifuta kesi sasa.
Ccm inapambana chadema kuliko kupambana Na tatizo LA ajira nchini kwani isiiache chadema iliyopoteza mvuto.Kifo cha aquilin kimewaingizia m350 si mtoe hata 100 muite familia Bila wao msingezipata.Kununua mizoga Na kuacha steki sio ndio kuuwa chama.Uliona wapi MTU mwenye njaa akaacha stahiki zake zote mishahara, posho,kiinua mgongo akaunga juhudi mikono mitupu ushahidi si umeona teuzi mmeachwa asilia wasugua bench teuzi wamepewa wahamiaji sababu huko ni ma zero brain angalau Kununua toka upinzani.
Wasababishi Wa mauaji ( mkuregenzi,polisi na mbunge wakipeta.
Busara za upinzani ndio Amani yetu
Ccm ikilala ikiamka inawaza cdm kuliko kuwaza ttzo la ajira nchini
 
WIGWA

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
886
1,000
Hata kama mna gangia tumbo kuna muda akili inagoma kabisa. Hivi kweli Kuhusu yule Binti wawatu alouliwa na mapolice unadiriki kuwalaumu chadema? Hebu Kuwa na hofu katika mambo unayofikiria hata kama ndo kutafuta kula ila sio kiivyo. So waungana na wale walosema risasi ilikata kona ikapita kwenye daladala ?
hapo chadema ndiyo wakubeba lawama asilimia 100 wasingeandamana binti wa watu yasingemkuta hayo chadema siyo chama ni genge la wahuni tu
 
mpima mstaafu

Senior Member
Jul 7, 2018
135
250
Baadhi ya viongozi wa siasa huwatumia wananchi kama inavyotumika karatasi ya chooni (toilet paper) au mshumaa kwa malengo ya kuwasaidia kusafisha mabaya yao,kuwasafishia njia,kuwapa mwaga huku wakiwaacha wanachama wao wakiteketea.

Ninasema hivyo kwani ni Chadema iliyowadanganya wanachama wake wadeki na kutandika kanga barabarani ili wabunge na madiwani pamoja na mgombea wao wa uraisi apite kipindi cha uchaguzi,baada ya uchaguzi manufaa yote waliyopata ya ongezeko la ruzuku,mfuko wa jimbo,mafao,mikopo nakadhalika, hakuna hata kitu kimoja wanachama waliambulia,maeneo waliyoyaongoza viongozi hawa yamebakia hayana maendeleo kwa ubinafsi wao wa kuangalia maslahi yao na ya familia zao kwanza.Ni viongozi wa Chadema waliowashawishi wanachama wao waandamane na kuwapiga mawe polisi,waliokamatwa hakuna hata kiongozi mmoja wa chama alieenda kuwatembela na kuangalia familia zao.

Mifano hii na mingine inaturejesha katika kisa hiki cha uchungu cha kupotea kwa maisha ya ndugu yetu Aquilina katika vurugu zilizoanzishwa na wafuasi wa Chadema. Baada ya kufariki kwa binti Aquilina,serikali ilichukua jukumu la kuusitiri mwili wa marehemu na kuwafariji wazazi na walezi wa Aquilina.Hakuna kiongozi yeyete wa Chadema ambaye aliwahi kufika katika familia ya marehemu na hakuna pesa au mchango wowote aliyowahi kupelekwa kwenye familia ya marehemu.Michango iliyochangwa kwa ajili ya zoezi hili iliishia kwa viongozi wachache ndani ya Chama.

Bado haifahamiki kuwa ni waandamanaji wa Chadema walimuua binti huyu pale walipokuwa wakiwarushia mawe polisi,risasi iliyotoka kwa mwandamanaji mwenye silaha au ni risasi iliyotoka kwa polisi ndio ilimuua binti huyu.Ukweli utafahamika tu,lakini tufahamu kuwa nafsi yeyote inayouliwa kwa dhuluma haiondoki bila kuacha athari kwa wale walioidhulumu.Hivyo basi mzimu wa kifo cha Aqulina pamoja na utekaji wa wanachama ndani ya Chadema unaolenga kujinufaisha kwa watu wachache kisiasa utaendelea kuwasumbua viongozi wa Chadema mpaka watakapotubu juu ya dhambi hii na zingine wanazowafanyia Watanzania.Hii inadhihirika katika hoja zifuatazo:-

1. Kushindwa kwenye chaguzi za marudio na za serikali za mitaa
Chadema imeendelea kudhoofika kama sio kufa katika maeneo ya mijini ambapo ilikuwa na nguvu kupitia UKAWA,hii inadhhirika kutokana na matokeo ya chaguzi za marudio katika maeneo mbalimbali ambazo wananchi wamechagua viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa zaidi ya asilimia 90% .Chadema pia imeendela kupoteza mvuto kwa wanachama wake wachache kwa kitendo cha kususia uchaguzi wa serikali za mitaa.Wanachama wameingiwa na wasiwasi na kupelekea kutojiandikisha na wale wengi waliojiandikisha kuazimia kutorudia tena makosa ya kuwachagua viongozi ambao ni wabinafsi wasio na uzalendo na nchi yao.

2. Zomea zomea ya Viongozi wa Chadema
Haikuwahi kutokea mpasuko uliopelekea wanachama kuzomea viongozi wao ndani ya chama,hasa kiongozi mkubwa kama Mwenyekiti wa chama.Hii inaendelea kudhibitisha mzimu wa Aquilini unawatafuna viongozi kutokana na zomea zomea zinazoendelea katika mikutano ya Chadema.Ni hivi karibuni tu Mh Freeman Mboe alizomewa na wanachama wake katika jimbo lake huko Hai wakimtaka aeleze alichowafanyia wananchi katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi wake,na baada ya kushindwa kueleza akahairisha mkutano.

3. Mkosi ya kunusurika kufungwa
Ilibakia alimanusra viongozi wote wa Chadema kwenda jela kutokana na kutiwa hatiani kwa jinai waliyoifanya.Chadema ilitumia tukio hili kujinufaisha na kutenda makosa mengine kama kutakatisha fedha nakadhalika.Tukio hili limeacha dowa kuwa kwani mchakato mzima wa ukusanyaji wa pesa hizi uligubikwa na usiri mkubwa wenye nia ovu ya kupiga hela na kutakatisha pesa chafu.

4. Mkosi inayopelekea kuvunjika viungo
Baada ya wanachama wa chadema kufanyafujo ndani ya Gereza kwa kutaka Mwenyekiti kutolewa bila kufuata utaratibu huku wakimiminia askari magereza matusi kama walivyo wamiminia askari polisi siku ya hukumu ya kesi ya viongozi wa chadema,ilitokea sintofahamu ambyo ilisababisha kuumia kwa viongozi hawa wa chma.Baadhi ya watu waliokuwepo katika eneo la tukio wanasema Halima mdee pamoja na Ester Bulaya waliangukiwa na kundi la wanachama waliokuwa wakiwakimbia askari magereza.

5. Kukusanya wanachama wao ili wawauwe kwa Korona
Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mboe anawahadaa wanachama wake kukusanyika licha ya kuwepo kwa ugonjwa wa Korona amabo unapinga mikusanyiko.Lengo kuu ni kuleta taharuki ya maambukizi mapya kwa Watanzania ili waweze kukusanya michango ya misiba kwa ajili ya kampeni za mwaka huu.

Chadema kama chama kinatakiwa kujitahmini juu ya kutumia damu za watu kufikia malengo yao ya kisiasa.Seriakali inatakiwa kuhakikisha kila jambo wanalofanya Chadema lina mustakabali mwema na nchi,sivyo kutumia kila rasilimali iliyopo kulizuia kwa manufaa ya nchi

Mungu ibariki Tanzania
Mungu awezi kuibariki Tanzania kwa dhambi za kusingizia wasio husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sesemela

Member
Dec 17, 2019
31
95
Dam ya akwirini inawatafuna CHADEMA.
We angalia saivi tuna gonjwa la CORONA mbowe anatangaza mikutano ! Kama cyo raana ni nini?
2. Wabunge na madiwani wanahama chama kila siku mbowe anaomba maridhiano je! Kama cyo raana ni nini?

DAM YA MTOTO AKWIRINI INAWATAFUNA CHADEMA NENDENI KWENYE KABURI LAKE MKAOMBE RADHI.
Dam ya mtu haimwachi muuaji salama. Tumuogope Mungu, mtoto huyu tumwache apumzike kwa amani mahali pema. Dhambi hii itazidi kuwatafuna mtaropoka hata yasiyostahili.
 
misasa

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
10,529
2,000
Ruzuku haikutumika wala kuwatoa watu korokoroni....watu walikua wameshanyolewa nyewel lakini mwenyekiti akakaa kimya akingojea utakatishaji fedha
Kabisa

Nimeshangaa na nilishindwa kupata jibu sahihi,tunashindwa kuhoji RUZUKU kisa tutaonekana wasaliti
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
852
1,000
Kama mzimu huo unawatesa viongozi wa CHADEMA, utamfanyaje aliye mfyatulia Aquilna risasi??! Vipi kuhusu walio tuma na kuagiza matumizi ya nguvu kubwa kukabiliana na watu wasio na silaa?!! Kama mzimu huo Upo leo umtokee hata mtetezi yeyote wa uzalimu!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom