WAZEE WETU WASILIPWE TU 'MBEGU ZA WALIZOKOPWA BILA HIARI' ZAIDI YA MIAKA 30 ILIYOPITA BALI NA 'MAVUNO YA JUU' PIA
Haki ya mtu inapocheleweshwa kiasi hiki kama ilivyotokea kwa wazee wetu hawa ni sawa na kusema ni uamuzi wa serikali kuwanyima haki yao hawa 'SENIOR CITIZENS' wetu kiukatili mno. Wana-JF, kama sehemu ya jamii, tunayo jukumu kuhakikisha Wazee hawa wanalipwa 'Mbegu zao stahiki' na 'Mavuno yake yote' ambayo ingeweza kupatikana kwa mfanyabiashara yoyote kutumia kila shilingi yao kwa miaka hiyo yote kwenye shughuli za uzalishaji.
Katika hili NGOs, Vyama Vya Hiari, Vyama Vya siasa, na Vyombo vya habari sote tunalojukumu lisilokwepeka kwa wazee hawa kuhakikisha kwamba kwa tangazo hili la Mhe Kikwete wazee wetu wanalipwa zaidi mavuno ya juu katika fedha stahiki waliokua walipwe tangu miaka hiyo yote.
Mhe Kikwete alikua wapi miaka yote mpaka akawaache wazee wetu waadhirike na kupigika kimaisha kiasi hicho wakati amekwepo serikali kwa miaka yote hiyo??
Na walipwe fedha zao pamoja ya gharama zote ya thamani ya hela hizo kwa kuzingatia kipindi chote amcho wazee hawa wamezuiliwa kutumia fedha zao hizo kwenye shughuli nyinginezo za uzalishaji ambazo zingechangia kuongezeka zaidi kwa thamani ya kila shilingi kama wangezipewa tangu huko nyuma.
Tofauti na hapo, itakua ni WIZI MTUPU kukopa hata shilingi 1 ya wazee wetu hawa tangu miaka 30 iliopita, na kuendeshea shughuli binafsi bila ridhaa yao, na kuja kuwarudishia shilingi hiyo hiyo 1 baada ya kipindi chote hicho.
Sote hapa JF tangu sasa tunakodolea macho kutaka kuona kwamba kwa ahadi hiyo ya Kikwete; Wazee wetu watalipwa HAKI STAHIKI au mazingaombwe kama kawaida kutoka Hazina??