Kikwete atikisa arusha

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
[h=3]Matukio Ya Arusha[/h]
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Zanzibar katika Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wakati wa hafla ya chakula cha usiku baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mei 31, 2012 usiku katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana wa Arusha walioshiriki kutoa huduma kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wakati wa hafla ya chakula cha usiku baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mei 31, 2012 usiku katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jengo hili liko nyuma ya jumba la mikutano la AICC jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais wa European Investment Bank Bw Plutarchos Sakellaris baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 31, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jengo hili liko nyuma ya jumba la mikutano la AICC jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisamiana na Rais wa Japan International Cooperation Agency (JICA) Profesa Akihito Tanaka na baadaye kufanya naye mazungumzo baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Mshauri wa Mfalme wa Tano wa Morocco Bw Omar Kabbaj baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 
Si tulikuwa tunaambiwa humu kuwa Rais Kikwete anagopa kwenda Arusha imekuaje tena kaenda.
 
ametikiswa. rais kupokelewa na watu watano huoni aibu? tuseme jengo linajengwa na watu watatu?
 
Ndio kawaangushieni pishi la ubwabwa wa siku moja kwenye hoteli gani hiyo tena?? Tunahitaji UCHUMI UNAOPAA si pishi la Ubwabwa la siku moja kwa wateule na familia zao hivo.
 
Tupunguze ushabiki usio na maana. Post hii ingeweza kuwa nzuri sana ingebeba title tofauti na hii.
 
Si tulikuwa tunaambiwa humu kuwa Rais Kikwete anagopa kwenda Arusha imekuaje tena kaenda.

Ni kwanini asubiri huu mkutano ndo aje Arusha tangu 2010. Amejificha nyuma ya mgongo wa AfDB ila siyo rahisi kufanya ziara ya kitaifa arusha anaogopa vidole 2. Hapa amejikaza mno mno na watu wameheshimu mkutano tu la sivyo angela kiwa na bendera za peoples power
 
Ningetarajia haitumie nafasi hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara pale unga limited!!!!!

Tiba

Mkuu pale labda ahutubie usiku ila kwa mchana inaweza kumwachia kumbukumbu mbaya kuliko zote katika maisha yake ya uongozi
 
Haa, hivi watu wanaelewa maana yakutikisa? Mtoa mada ulikuwepo Jangwani Jmosi? Umewahi kusikia kiwanja inauwa NMC

Arusha? Au unaweza kufika Mtwara mara moja? Utaelewa maana ya kutikisa then urudi hapa
 
Magamba at work,accomponed by ritz. Naona hapo katikiswa.
 
Back
Top Bottom