Issue ya REDET na Synovate waulize wenyewe... lakini ukitumia medula oblangata uliojaliwa na Mungu, ulizia uchaguzi wa serikali za mitaa CCM iliibuka na kura kiasi gani? Alafu jiulize ni kitu gani cha ajabu kimetongea tangu wakati huo mpaka sasa? Jiulize kipi CHADEMA imekuja nacho cha ajabu ambacho kitaweza kubadili matokeo kiasi hicho? Jiulize CCM inaowabunge wangapi? Niulize CCM inatarajia kupata wabunge wangapi? Jiulize wabunge na madiwani wa CCM ambao wametapakaa nchi nzima hawana mchango kwa kura za Rais wao.
Sisi waTanzania watu wa ajabu sana tunaamini mazingaombwe mno....
Kasheshe usijifanye hujui hizi taasisi za utafiti kwa nchi zetu jinsi zinavyofanya kazi na zinafanya kazi kwa maslahi ya nani. Haziko huru katika kutoa matokeo yao na ndio maana mwaka huu wameshikwa na kigugumizi.
Naomba nawe utumie medula oblangata yako kujiuliza, ni kwanini JK ambaye ni mgonjwa ameongezewa ratiba ya kuzunguka kwa ajili ya kampeni? Siku ya uzinduzi wa Kampeni Kinana alisema kwamba mwaka huu kwa kuzingatia afya ya mgombea wao, wamempunguzia kilomita atakazosafiri kwa njia ya barabara ikilinganishwa na alizozunguka mwaka 2005. Swali, je kwanini wamebadilisha huo mwelekeo? Kwanini Mama kikwete anahaha kila kona kuomba kura za JK? Kwanini Ridhiwani anazunguka kila kona kusaka kura za JK? Something is wrong some where na ndio maana REDET na Synovate wamekaa kimya kwa kuwa jahazi linakwenda mrama.
Maswali yako yananifurahisha sana, kutapakaa wabunge nchi nzima haimaanishi kwamba wanakubalika, na ninaomba nikusahihishe kwamba ni wagombea ubunge. Kumbuka hii ni ngwe mpya ndugu yangu na ndio maana kuna wabunge wengi wa CCM ambao walikuwepo miaka 5 inayoisha sasa, lakini wamepoteza nafasi za kutetea ubunge kwenye kura za maoni ndani ya chama chao. Kama mtu alikuwa mbunge kipindi cha 2005 - 2010, haina maana kwamba atachaguliwa tena. Kwa hiyo hoja yako kwamba CCM wabunge wake wametapakaa nchi nzima, is invalid.
Labda nikuongezee angalizo, uchaguzi mkuu wa 2005, kwenye majimbo ya Kiteto, Busanda na Biharamulo, CHADEMA walipata kura chache sana, lakini kwenye chaguzi ndogo ilibidi top brass ya CCM ipige kambi kwenye hayo majimbo na bado CHADEMA ilipata zaidi ya 40%.
Huwezi kulinganisha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, ni vitu viwili tofauti na vinachukuliwa kwa uzito tofauti hata ndani ya CCM yenyewe. Kwa hiyo let us focus on the general election iliyo mbele yetu.
Bottom line ni kwamba kama CCM ingekuwa na uhakika wa ushindi wala wasingebadilisha ratiba ya JK ambaye ni mgonjwa na tayari alishaanguka tangu siku ya kwanza. Pia wasingeishirikisha familia kama wana amini kwamba wagombea ubunge na udiwani waliotapakaa nchi nzima wana mchango kwenye kura za JK.