Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,186
- 56
Vyanzo vyangu vya hapa USA vimethibitisha uvumi ambao kwa muda umekuwa unaendela Tanzania kuwa serikali ya marekani ina mpango wa kujenga kituo cha kijeshi cha kudumu (permanent base) nchini Tanzania.
Ingawa serikali ya Tanzania imekuwa inajaribu kuficha hizi habari kwa visingizio kuwa mambo ya kijeshi hayajadiliwi kwa vile yanahusu usalama wa taifa, nimeamua kuwaambia wanajeshi kuwa hili suala la kuwa na base ya wamarekani Tanzania ni kubwa na hivyo ni vyema wakaruhusu watanzania wakalijadili.
Siku za karibuni Kikwete amekuwa na vikao vya wazi na vya siri na wamarekani ambao wanatafuta nchi katika pwani na pembe ya afrika ili wajenge kambi ya kijeshi ya kudumu kama ile waliyo nayo kule KATARI (sijui namna ya kutamka hii nchi kwa kiswahili) kule mashariki ya kati.
Wazo la kuweka kambi Ethiopia limeonekana gumu kutokana na hali ya usalama, chaguo la pili la marekani lilikuwa Kenya ambayo hali ya ukabila inatishia usalama wa Kenya. Wamarekani wameamua kuchagua Tanzania ambao so far wanaona kama nchi yenye amani na utulivu.
Habari zinasema kuwa kimsingi Kikwete amekubali (nani angekataa pesa kibao wamarekani walizotoa) na Marekani imelipa pesa indirect kwa kuahidi kutoa mabilioni ya pesa za msaada. Yes, hizi pesa walizoahidi juzi za kuisaidia Tz zitaishia mfukoni mwa wachache na zitakazobaki zitasaidia kujenga base.
MY TAKE.
1. Mimi naunga mkono suala la wamarekani kuwa na base ya Tanzania maana ikiwepo au isiwepo sioni faida au hasara yoyote ukichukulia kuwa Kikwete na wenzake wanauza nchi kila siku.
2. Ni vizuri Kikwete aendeleze mchezo wa kula pande zote mbili za wa-Irani na wamarekani.
3. Kikwete awaambie ukweli wa-Tanzania wa kile kinachoendelea.
4. IMF na Benki ya dunia wakome kusifia Tanzania kuwa inaendelea wakati wakijua ni uongo ila wanatimiza moja ya masharti ya Tz kukubali ku-host base ya marekani.
5. Kikwete atimize ahadi yake kabla Raila hajashinda uchaguzi wa Kenya maana Raila naye amekubaliana na wamarekani katika hili.
Thanks!