Kikwete amsafisha Chenge; Asema Hakuna Rushwa Kwenye Kashfa ya Rada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amsafisha Chenge; Asema Hakuna Rushwa Kwenye Kashfa ya Rada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 2, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]• ASEMA HAKUNA RUSHWA KWENYE KASHFA YA RADA

  na Martin Malera
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  RAIS Jakaya Kikwete amevunja ukimya kwa kusema kwamba hakuna rushwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada kutoka nchini Uingereza.


  Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina, lakini kwa kauli hiyo ni dhahiri kwamba amemsafisha Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa ndani na nje ya chama chake kuhusika na kashfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE- System.

  Chenge, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, anatajwa kuhusika kutoa ushauri wa kisheria wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ushauri ambao unatajwa kuzingatiwa katika hatua za uamuzi.


  Mwingine anayehusishwa na kashfa hiyo ni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Idriss Rashid.


  Pamoja na hao, wanatajwa wafanyabiashara wenye asili ya India, lakini ambao wanaishi/walipata kuishi Tanzania, Tanil Somaiya, ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya uwakala wa simu ya Shivacom na Sailesh (Shailesh) Vithlani kuwa watu wa kati wa biashara hiyo.


  Akijibu swali kutoka kwa mmoja wa wahariri aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa kwa waliohusika na ununuzi wa rada wakati chenji yake imesharejeshwa, Rais Kikwete alisema Serikali ya Uingereza iliyokuwa ikichunguza kashfa hiyo imebaini kuwa hakukuwa na rushwa katika ununuzi wa rushwa.


  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, uchunguzi wa Serikali ya Uingereza ulibaini kuwa kulikuwa na makosa ya uchapaji, lakini hakuna mtu aliyehusika kutoa wala kupokea rushwa.


  "Kama Uingereza waliochunguza kashfa hiyo wamefika mahala wanasema kulikuwa na makosa ya uchapaji tu, mtu wenu mnamfikisha mahakamani kwa ushahidi upi?" alihoji Rais Kikwete.


  Mchakato wa ununuzi wa rada, uliwahusisha watu wa madaraka na kada mbalimbali ambao ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair.


  Blair anatajwa kuwa ndiye aliyemshawishi aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin Mkapa, kununua rada hiyo kutoka Kampuni ya kutengeneza silaha ya Uingereza BAE-Systems. Wakati huo aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa, Clare Short, alikataa katakata Tanzania, moja kati ya nchi masikini kabisa duniani, kutumia sh bilioni 40 kununua rada katikati ya umasikini unaonuka.


  Hata hivyo chenji hiyo ya rada, zaidi ya sh bilioni 75 zimerejeshwa nchini baada ya hati ya makubaliano baina ya pande zinazohusika kusainiwa.


  Hati hiyo ilisainiwa kati ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya Uuzaji wa Silaha ya Uingereza (BAE - System), Ofisi ya Uingereza ya Kupambana na Ufisadi (SFO) na Idara ya Kimataifa ya Misaada ya Maendeleo (DFID).


  Chenge mwenyewe huko nyuma alipata kuzungumzia suala hilo na hasa, kumiliki kwake kwa akaunti ya fedha nyingi nje ya nchi inayohusishwa na mlungula wa ununuzi wa rada.


  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Edward Hosea, alipata mara mbili kunukuliwa akisema Chenge hakuwa na kesi ya kujibu katika kashfa hiyo ya rada.


  Kuhusu sakata la wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), iliyohusisha Kampuni ya Kagoda iliyochota sh bilioni 40, Rais Kikwete alisema suala haliko kwake bali mikononi mwa vyombo vya dola.


  "Hili la Kagoda liko mikononi mwa vyombo vya dola, wanaendelee nalo," alisema Rais Kikwete.

  Hata hivyo Rais Kikwete alitamba kuwa serikali yake imejitahidi sana kupambana na rushwa kwa kuimarisha uwezo wa TAKUKURU.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Bingo!!! Kulikuwa hakuna Rushwa just a regular 10% KAMA KAWAIDA...

  Samahami Mliodhani hiyo 10% ni RUSHWA...
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  naona ametofautiana na BAE system ya Uingereza.
   
 4. EXTERMINATOR

  EXTERMINATOR JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyani awezaje kuwa hakimu kesi ya ngedere. Na yeye pia ana mkono kwenye EPA na RADA ndo maana anatetea
   
 5. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi alijibu nini kuhusu swali la Kagoda iliyochota mahela ya uchaguzi 2005?au aliipotezea?
   
 6. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa nchi hii chini ya utawala huu chini ya chama hiki CCM kupigana vita na rushwa lau kuipunguza ni ndoto takururu na vyombo vyote vya kupambana na rushwa ni kupoteza pesa za wananchi.Rushwa katika CCM ni sera namba moja.Nashindwa kuelewa kwanini wasitangaze hilo rasmi ili tusiwabugudhi na kuwahoji?
   
 7. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  [h=1]BAE Systems fined for Tanzania radar sale: reaction[/h][h=2]BAE Systems was fined £500,000 by a London judge and must pay the rest of an agreed £30m fine to Tanzania, to settle a long-running corruption probe by the Serious Fraud Office. Here is a round-up of reaction to the result:[/h]
  Gavin Cunningham, director, forensic accounting and investigations division, BTG Global Risk Partners, formerly a principal investigator at the Serious Fraud Office:

  "The penalty imposed by the judge of £500,000 plus costs bears no comparison to the $400m (£258m) penalty imposed by the US authorities on BAE, and partly reflects the problem in bringing a charge under the Companies Act. The agreement by BAE to pay £30m for the benefit of the people of Tanzania is effectively a civil arrangement and not part of the criminal penalty.

  "The difficulties the judge had in accepting the basis of plea is self evident from his judgement which expresses astonishment at how anyone could be so naïve to think that the monies were legitimate lobbying expenses.

  "I expect the new Bribery Act to sharpen the teeth of the SFO."
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Book gives insight into stinking radar, jet deals[/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 13 February 2012 11:01[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]
  former Tanzanian Attorney General Andrew Chenge

  By The Citizen Reporters
  Dar es Salaam. An internationally acclaimed book by a seasoned journalist and anti-corruption whistleblower has made chilling revelations on how the Tanzanian government was sweet-talked into buying
  malfunctioning and grossly over-priced equipment.Third phase President Benjamin Mkapa and former British Prime Minister Tony Blair feature prominently in the recently published 672-page book titled ‘The Shadow World-Inside the Global Arms Trade’.
  The author is seasoned South African journalist Andrew Feinstein, founding co-director of Corruption Watch, an anti-corruption non-governmental organisation.

  The equipment include the $40 million military radar and a brand new Gulfstream presidential jet for another $40 million, in a country in which the poorest third of its population lives on less than a dollar a day.

  According to the author, the idea that Tanzania should have the military radar did not originate from the country’s leaders, but was pushed by Mr Tony Blair, during his tenure at Number 10 Downing Street.He specifies that the ex-British premier not only sold the radar idea to then-President Mkapa, but coupled it with a promise to ensure that the deal was sealed.

  “While trumpeting his Commission for Africa’s recommendations for improved governance on the continent, Tony Blair persuaded the President of Tanzania, one of the world’s poorest countries, to purchase an air radar system for military aircraft at the cost of Sterling Pounds 40 million,” reads part of the book.

  The book first published in the UK late last year by Penguin Books, alleges that massive corruption and money laundering was done by Asian-Tanzanian business tycoons Sailesh (or Shailesh) Vithlani and Tanil Somaiya to sell some of the equipment to former Tanzanian Attorney General Andrew Chenge and former Central Bank Governor Idriss Rashidi.

  Requested for his reaction, Mr Chenge said it would be imprudent for him to comment because he had not seen the book. He asked this reporter: “What is the title of the book again?” The former Attorney General, whom the reporter had encountered shortly after yesterday’s session of the National Assembly was adjourned on Friday, then excitedly remarked:“God loves me, because I will surely consult my lawyers after reading the book to see the possibility of suing the author. This means I will make money. Is this not a blessing from God?”

  According to the book, Somaiya and Vithlani had been making good money from arms deals for many years before the radar purchase.

  “They were involved in public procurement contracts worth well over $240 million,” says the author in the book that has been described by South African Archbishop Desmond Tutu as “peeling back the veil of secrecy behind which the global arms trade undermine accountable democracy, socio-economic development and human rights, causing suffering across the world.”

  “In the same way that Andrew Feinstein (the author) exposed a corrupt arms deal that darkened South Africa’s rainbow nation, he has now turned his forensic gaze on the impact of similar weapons deals around the world,” comments Archbishop Tutu on the back cover.

  In 2004-5, says the book, Vithlani and Somaiya won a multi-million dollar tender from the Ministry of Defence for the supply of around 650 trucks and buses for the Tanzania People’s Defence Forces (TPDF).“While the government paid the suppliers the full amount of the purchase price in 2006, only 350 of the vehicles had arrived in the country by 2009,” says the book.

  In applying for the tender, says the book, Somaiya and Vithlani fraudulently claimed to be the owners of Incar Tanzania Limited, the authorised dealer for Iveco trucks from Italy.

  “It was not until 2006 that they actually bought the company. The Incar company file has meanwhile mysteriously vanished from the Business Registration and Licensing Authority office in Dar es Salaam,” says the book.
  The book was published last year at a time when BAE had already agreed to compensate Dar for the £30 million air traffic control system.

  According to information from the House of Commons, BAE is expected to sign a memorandum of understanding with the Tanzanian government later this month with regard to the £30 million payment. The full sum will become due 14 days after the document is signed.
  The compensation deal has been dogged by political problems ever since BAE agreed to pay.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 8. d

  dguyana JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Da raisi wangu wee!!!
   
 9. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mimi napata tatizo sana na serikali ya awamu ya nne! Nakuheshimu sana JK kama Rais wangu ninaamini wewe ni chaguo la Mungu maana uongozi wa taifa lolote unawekwa na Mungu hata kama uliupata kwa njia zozote zile za kisanii lakini Mungu akaruhusu mimi ni nani kupingana na Mungu?

  Tatizo langu ni pale Waziri wako wa mambo ya nchi za nje ambaye kwa uelewa wangu ni mtu ambaye kadhia hii ilikuwa inakuwa reported kwake maana ilikuwa inahusu nchi na nchi anasema kulikuwa na rushwa kwenye rada na hili amelirudia tena kwenye kipindi cha dk. 45 cha ITV iweje leo Mheshimiwa Rais wangu useme hakukuwa na rushwa katika ununuzi wa rada?

  Huoni kwamba watu wanaweza kukukosea adabu na kufikiri ni mmoja wa waliofaidi sehemu ya hiyo rushwa? sitaki kuamini hivyo Mheshimiwa Rais lakini wakati mwingine kutetea jambo ambalo ni obvious linawafanya/linatufanya watanzania wengine tushindwe kukuelewa.

  Kwakuwa Mungu anasema tuheshimu wenye Mamlaka na wewe una mamlaka nitabaki kukheshimu lakini ningependa kukuomba uwe unachagua maneno unapozungumzia mambo mazito ya taifa hili.

  Asante
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Sasa ulitegemea aseme nini wakati na yeye alikuwa mnufaika na hiyo rushwa?
   
 11. S

  SON OF DAVID Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kichaa ndio anayeweza kukata mkono unaomlisha.
  Ni mwendawazimu ndo anaweza kukata tawi alilokalia- maana haogopi kuanguka.
   
 12. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Naamini Dr. Slaa atakuwa ame-take note kwani hiyo ni kete kwa uchaguzi 2015 kwa kuwa ccm sasa nidhahiri haiwezi kutengwa na rushwa.kwa ccm rushwa is just 10% commission.
   
 13. B

  Baba Tunde JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 359
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red ndugu zangu! Kwenye utawala huu wa CCM na rais dhaifu, kupigana na rushwa ni ndoto.
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Ulitegemea jibu gani zaidi ya hilo kutoka kwenye huu utawala
  Maana 10% kwao sio rushwa ni asante ndo maana waliwahi kuidhinisha sheria ya takrima
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  walikula wote hii pesa sasa mnategemea nini?
   
 16. D

  Do santos JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wote tumemsikilza rais alichojibu na kimeeleweka sasa hapa mnataka kupotosha,ushahidi wenu mtasema gazeti limeandika hovyooo....! wagala punguzeni chuki jamaa kafanikiwa sana ktk uongozi wake.Mbona hamsemi alichosema kuhusu sekta ya afya ilivyopiga hatua.Acheni kuropoka kama yule mwandishi aliyesema ct scan kwa bei ya shangingi
   
 17. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama ni muislam kamili na huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani muapizeni akatae kuwa hakula rushwa ya mkataba wa IPTL? Yeye ni mmoja wao katika genge la kufisadi hii nchi lazima atawatetea wenzie!!
   
 18. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Georgia

  You are right!

  Rais Jakaya Kikwete ni mvivu kusoma ama his memory is very short. The bunch of Wahahariri wangemuliza ajibu kwa ufasaha ni sababu gani zilimfanya Andrew Chenge akajiuzulu uwaziri?

  Kama sio rushwa what really transpired . RADA ilininuliwa kwenye awamu ya kwanza ya Ben Mkapa . What made the change kuchukua zaidi ya miaka kumi kurudisha if it was simply a typing error?

  Jakaya hao washauri wanaokuzunguka hutaenda nao kaburini . Nakuahidi ukimaliza mwaka 2015 unatarajia kwenda kuishi wapi? I think it's better ukaboresha magareza for sure tutakuondolea hiyo immunity and jail will be your first choice wewe endelea kujifunika na net kuzuia mvua. Hata watoto wako wezi mtaungana wote in jail.

  You have the chance then take it watu wote Deep Green, Kagoda, Meremeta na akina Richmond , na RADAR peleka jela wewe cheka tu ulisema mwenyewe akili ya kuambiwa changanya na ya kwako?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  [h=1]BAE criticised by UK MPs over Tanzania corruption[/h]By Mark DoyleBBC International Development Correspondent[​IMG]BAE, based at Warton near Preston, Lancashire, agreed to pay £30m to the Tanzanian people
  Continue reading the main story[h=2]Related Stories[/h]

  The British arms and aircraft firm BAE Systems has been severely criticised by a UK parliamentary inquiry into a corruption case surrounding an air-traffic-control deal with Tanzania.
  MPs accused BAE of unilaterally setting up a compensation arrangement for Tanzania that was a "complete sham".
  BAE admitted to not keeping full accounting records of £8m ($12m) it paid to an agent who brokered the deal.
  After a plea bargain, it was not found guilty of any wider corruption charges.
  The controversy relates to the supply in 1999 of an air-traffic radar control system.
  But it could also be a test case for campaigners who say bribery and corruption are a brake on economic development.
  In a plea bargain with the prosecuting authorities, the Serious Fraud Office, BAE agreed to pay £30m to the Tanzanian people.
  The £30m was effectively a compensation payment to Tanzania - because of the revelation of the embarrassing £8m payment and allegations that the military-style air-traffic system was unnecessarily complex and expensive.
  BAE and the Serious Fraud Office said they could not say if the £8m was used for bribery to seal the radar sale.
  A top BAE lawyer, Philip Bramwell, said the company sincerely apologised for events of the past - and he agreed it would not make payments similar to the £8m now.
  'Naive'MPs on the watchdog International Development Committee dismissed some of the company's positions as "waffle" and "dissembling".
  They repeated a judge's comments that it was "naive in the extreme" to think the £8m was used legitimately and that there was "a high probability" that the sum had been used in the negotiating process to "favour" the BAE bid to supply the radar.
  The MPs also asked BAE executives why none of the £30m had yet been paid.
  They questioned the right of the company to set up its own advisory board to decide on how the money should be spent - rather than give the money directly to the government of Tanzania, as a group of Tanzanian MPs had requested.
  Committee chairman Malcolm Bruce MP asked whether it was not "offensive" for the company to suggest it knew better how to spend the money than the government of Tanzania.
  With the Tanzanian government, British aid ministry the Department for International Development has drawn up a plan to spend the money on the Tanzanian education system - for desks, text books and teachers' accommodation.
  Mr Bruce advised BAE to hand the money over to this project "as soon as possible".
  The director of the Serious Fraud Office, Richard Alderman, who also appeared before the committee, said he was surprised the money had not yet been disbursed as promised by BAE.
  He undertook to write to the company to ask why not - and said there would be "consequences" if there were further delays
   
 20. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  'In Vino veritas, in Aqua sanitas'. Pole sana!
   
Loading...