Kikwete amsafisha Chenge; Asema Hakuna Rushwa Kwenye Kashfa ya Rada

Kwa hiyo ina maana kuna mtu humu amewahi kudhani JK anaweza kwenda kinyume na maslahi ya chama?

JK ni dhaifu...
 
Rais DHAIFU halafu pia MUONGO....halafu tukisema ukweli wanalalamika tunamtukana msanii!!!! Hii kauli ya kumsafisha Vijisenti ni uongo wa hali ya juu.
 
Mtanzania, ulitarajia mkuu asemeje. haya ni mambo ya kawaida tu. Kumbuka hayo yalifanyika enzi za Takrima na asante(10%) mambo ambayo kwao sio rushwa. Lakini Anyway, wacha tungoje awamu yake na chama chake iishe, kila kitu kitakuwa wazi, uozo wote utafukuliwa ikiwa ni pamoja na la IPTL.
 
Kinyamana, ni kweli tunapaswa kuiheshimu mamalaka iliyopo madarakani. Lakini ni vizuri tukaiheshimu mamlaka hiyo katika mambo mema. Maana ziko mamlaka nyingine zinawekwa na Mungu lakini Mungu huyohuyo anaweza kuzikataa mamlaka hizo baada ya kutenda maovu. Mkumbuke Sauli (Enzi za Samweli) alikataliwa na Mungu baada ya kutenda mambo maovu. Nani ajuaye, huenda hata mamlaka iliyopo sasa Tanzania imekataliwa na Mungu ndio maana mambo yanakwenda hovyo hovyo tu.
 
I hope JK huaga anasoma current affairs kabla ya kuongea. Ukweli wote wa hii dili ya radar uko kwenye kitabu hiki hapa. Watanzania wote walioshiriki kwenye hili dili na rushwa yote waliopewa imetajwa humu ndani. Mwenye mcho haambiwi tazama!

41RLAzf%2BxJL._SL500_AA300_.jpg


The Shadow World is the harrowing behind-the-scenes tale of the global arms trade, revealing the deadly collusion that all too often exists among senior politicians, weapons manufacturers, felonious arms dealers, and the military-a situation that compromises our security and undermines our democracy.


Pulling back the curtain on this secretive world, Andrew Feinstein reveals the corruption and the cover-ups behind a range of weapons deals, from the largest in history-between the British and Saudi governments-to the guns-for-diamonds deals in Africa, the imminent $60 billion U.S. weapons contract with Saudi Arabia and mind boggling radar equipment sold to Tanzanian air force that has 8 planes at cost equivalent to the amount spent on healthcare. He exposes in forensic detail both the formal government-to-government trade in arms and the shadow world of illicit weapons dealing, and lays bare the shockingly frequent links between the two. Drawing on his experience as a member of the African National Congress who resigned when the ANC refused to launch a corruption investigation into a major South African arms deal, Feinstein illuminates the impact this network has not only on conflicts around the world but also on the democratic institutions of the United States and the United Kingdom.


Based on pathbreaking reporting and unprecedented access to top-secret information and major players in this clandestine realm, The Shadow World places us in the midst of the arms trade's dramatic wheeling and dealing-from corporate boardrooms to seedy out-of-the-way hotels-and reveals the profound danger and enormous financial cost this network represents to all of us.
 
rais kikwete,juzi juzi,akihutubia taifa,pamoja na mambo mengine,alisema kwy ununuzi wa rada,hakukuwa na ufisadi hata chembe,na mwaka mmoja,uliopita kwy mkutano wa ccm,alimwomba msekwa awataje kwa majina wale mapacha wa3,ndio jina la Chenge likatajwa,akihusichwa na rushwa ya rada,nape mnauye akawa fungu na rais,kuzunguka nchi zima,kuwataja magamba,je unamwelewa huyo dr Mrisho kikwete?
 


• ASEMA HAKUNA RUSHWA KWENYE KASHFA YA RADA

na Martin Malera


RAIS Jakaya Kikwete amevunja ukimya kwa kusema kwamba hakuna rushwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada kutoka nchini Uingereza.


Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina, lakini kwa kauli hiyo ni dhahiri kwamba amemsafisha Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa ndani na nje ya chama chake kuhusika na kashfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE- System.

Chenge, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, anatajwa kuhusika kutoa ushauri wa kisheria wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ushauri ambao unatajwa kuzingatiwa katika hatua za uamuzi.


Mwingine anayehusishwa na kashfa hiyo ni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Idriss Rashid.


Pamoja na hao, wanatajwa wafanyabiashara wenye asili ya India, lakini ambao wanaishi/walipata kuishi Tanzania, Tanil Somaiya, ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya uwakala wa simu ya Shivacom na Sailesh (Shailesh) Vithlani kuwa watu wa kati wa biashara hiyo.


Akijibu swali kutoka kwa mmoja wa wahariri aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa kwa waliohusika na ununuzi wa rada wakati chenji yake imesharejeshwa, Rais Kikwete alisema Serikali ya Uingereza iliyokuwa ikichunguza kashfa hiyo imebaini kuwa hakukuwa na rushwa katika ununuzi wa rushwa.


Kwa mujibu wa Rais Kikwete, uchunguzi wa Serikali ya Uingereza ulibaini kuwa kulikuwa na makosa ya uchapaji, lakini hakuna mtu aliyehusika kutoa wala kupokea rushwa.


“Kama Uingereza waliochunguza kashfa hiyo wamefika mahala wanasema kulikuwa na makosa ya uchapaji tu, mtu wenu mnamfikisha mahakamani kwa ushahidi upi?” alihoji Rais Kikwete.


Mchakato wa ununuzi wa rada, uliwahusisha watu wa madaraka na kada mbalimbali ambao ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair.


Blair anatajwa kuwa ndiye aliyemshawishi aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin Mkapa, kununua rada hiyo kutoka Kampuni ya kutengeneza silaha ya Uingereza BAE-Systems. Wakati huo aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa, Clare Short, alikataa katakata Tanzania, moja kati ya nchi masikini kabisa duniani, kutumia sh bilioni 40 kununua rada katikati ya umasikini unaonuka.


Hata hivyo chenji hiyo ya rada, zaidi ya sh bilioni 75 zimerejeshwa nchini baada ya hati ya makubaliano baina ya pande zinazohusika kusainiwa.


Hati hiyo ilisainiwa kati ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya Uuzaji wa Silaha ya Uingereza (BAE - System), Ofisi ya Uingereza ya Kupambana na Ufisadi (SFO) na Idara ya Kimataifa ya Misaada ya Maendeleo (DFID).


Chenge mwenyewe huko nyuma alipata kuzungumzia suala hilo na hasa, kumiliki kwake kwa akaunti ya fedha nyingi nje ya nchi inayohusishwa na mlungula wa ununuzi wa rada.


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Edward Hosea, alipata mara mbili kunukuliwa akisema Chenge hakuwa na kesi ya kujibu katika kashfa hiyo ya rada.


Kuhusu sakata la wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), iliyohusisha Kampuni ya Kagoda iliyochota sh bilioni 40, Rais Kikwete alisema suala haliko kwake bali mikononi mwa vyombo vya dola.


“Hili la Kagoda liko mikononi mwa vyombo vya dola, wanaendelee nalo,” alisema Rais Kikwete.

Hata hivyo Rais Kikwete alitamba kuwa serikali yake imejitahidi sana kupambana na rushwa kwa kuimarisha uwezo wa TAKUKURU.
hii inadhihirisha kuhusika kwake maana uchunguzi unaonyesha Mwizi au Mtenda kosa uwa hakubali mpaka kibano...this z what JK did.....kazi kwetu tulioibiwa....
 
Back
Top Bottom