Kikwete alijua na kuruhusu jengo la ubalozi Italy kununuliwa

ANIKA ALIVYOSHIRIKI KATIKA MCHAKATO KIPINDI AKIWA WAZIRI MAMBO YA NJE, ASEMA ALIKUTANA NA MAMA MWENYE NYUMBA NA KUAGIZA ALIPWE DOLA MILIONI MOJA HARAKA, AKAMPA OFA KUJA MBUGA YA NGORONGORO
Tausi Ally
ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Rais Jakaya Kikwete wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alifahamu kuwepo kwa rasimu mbili za mikataba ya ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania, Italia.

Profesa Mahalu alisema hayo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Ilvin Mgeta wakati akitoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60 pamoja na aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin.

Akiongozwa na wakili wake, Mabere Marando, Profesa Mahalu aliitambua barua ya Februari 20, 2002 ambayo ilikuwa ikieleza kuwa matayarisho yote ya ununuzi wa jengo la ubalozi huko Italia yamekamilika ikiwa ni pamoja na rasimu mbili za mikataba.

Mahalu alidai kuwa katika mchakato wa ununuzi wa jengo hilo wakati yeye akiwa Balozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kulikuwa na rasimu mbili za mikataba na kwamba aliwahi kuwasiliana na wizara hiyo juu ya mikataba hiyo.

Alidai kuwa Desemba 2001, Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikwenda Rome, Italia kwenye Mkutano wa SADC na alipokuwa huko, ubalozi ulifanya mpango atembelee jengo hilo lililopendekezwa kununuliwa kwa ajili ya ofisi ya ubalozi.

“Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia ilifanya mipango yote kwa kumpa utaratibu na usalama Kikwete ambapo alikwenda kutembelea jengo hilo na kukutana na mama mwenye jengo,” alidai Profesa Mahalu.

Alidai kuwa kabla ya mazungumzo na mwenye nyumba, mtoto wa mama huyo, Alberto alimtembeza Kikwete kwenye jengo hilo ndani na nje na baadaye mazungumzo hayo yaliendelea.

Balozi Mahalu alisema baadaye mazungumzo kati ya Kikwete na mama huyo yaliendelea na Alberto alikuwa akitafsiri, kwa sababu mama yake hakufahamu lugha ya Kiingereza.

Profesa Mahalu alidai kuwa katika mazungumzo hayo, Kikwete alimwuliza mama huyo: “Hivi ni kwa nini kunakuwa na mikataba miwili?” na mama huyo alimjibu kuwa hiyo ni kawaida kwa Italia ukitaka kununua jengo kwa bei nafuu.

Profesa Mahalu aliendelea kudai kuwa baada ya kupewa jibu hilo, Kikwete hakuzungumza tena zaidi ya kucheka na kwamba mwenye jengo alimkumbusha kuhusu malipo ya awali ya dola milioni moja za Marekani ambapo aliafiki na kuahidi kuwa zingelipwa kabla ya mwisho wa mwaka 2001.
Profesa Mahalu alidai pia kwamba Kikwete alimweleza mama huyo kuwa atalishughulikia suala hilo baada ya kurejea Dar es Salaam na kumshukuru kwa kuwauzia jengo zuri.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Profesa Mahalu alidai kuwa baada ya Kikwete kusema maneno hayo, alimgeukia na kumwambia: “Costa ni vizuri tupate hela tumlipe huyu mama watu wengine wasije wakachukua hili jengo.”

Profesa Mahalu alidai kuwa baada ya Kikwete kumshukuru mama huyo kwa ukarimu wake, alimkaribisha Tanzania awe mgeni wa Wizara ya Mambo ya Nje yeye na mumewe na kwamba watampeleka Ngorongoro.

“Tulipokuwa njiani tukirudi hotelini alipofikia Kikwete akiwa kwenye gari alimpigia simu Kibero akimuagiza afanye utaratibu wa kulipa Dola milioni moja kama malipo ya awali ya jengo hilo,” alidai Profesa Mahalu.

Alidai kuwa baadaye alimwagiza (Profesa Mahalu) aje Dar es Salaam kufuatilia mpango huo wa malipo ya awali ya ununuzi wa jengo hilo.

Awali, Profesa Mahalu akiongozwa na Wakili Alex Mgongolwa alidai kuwa anaitambua ripoti ya uthamini wa jengo hilo la ubalozi nchini Italia uliofanywa na Kimweri kutoka Wizara ya Ujenzi aliyekwenda Rome Julai 15 hadi 26, 2001 kwamba jengo lilikuwa na gharama ya Sh6 bilioni.

Pia alizitambua ripoti za uthamini wa jengo hilo ambazo ni ile ya mama mwenye nyumba ambayo ilionyesha kuwa jengo hilo lilikuwa na thamani Sh5.500 bilioni na ripoti ya uthamini iliyofanywa na Serikali ya Italia iliyoonyesha kuwa jengo lilikuwa na thamani ya Sh11.117 bilioni.

Hakimu Mgeta aliiahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kwa utetezi.

source mwananchi
 
Mimi simtetei Kikwete ila ninachoshwa na jinsi watu wanavyokosa yakusema hapa JF hata kufikia hatua ya kuleta vitu vya kuokoteza okoteza tu.... mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...
mkuu hizi habari hatujaziokoteza.....ubadhirifu umefanyika na waziri wa mambo ya nje alijua na aliona mikataba miwili miwili na akakubali baana ya kuambiwa ni taratibu za Italy kwa mjengo wa bei nafuu....kwanini haku take actuion haraka kipindi kile????
mahalu anatakiwa kujibu hoja kwa nn aliiba aache uhuni na ujanja unja
kamtaja aliekwua bos wake kuwa walishrikiana kwenye sakata hilo......haiwezekani ununuzi mkubwa wa balozi waziri wa mambo ya nje hasijue......
 
Dah...hii nouma! Ndio maana inakuwa ngumu kwa JK kushughulikia suala la ufisadi kwa dhati kwa sababu kila jambo na yeye au marafiki zake wa karibu wanakuwa implicated!
 
Watu mnachekesha kweli eti waziri wa mambo ya nje a take action, mlitaka achukue action gani? Awaambie wasinunue jengo? kwa mnajili gani? yeye mthamini majengo? yeye Kikwete ndio aliyetafuta hiyo nyumba? yeye ndiye aliyepokea hizo pesa?

Na hiyo dummy cheque kwani iliandikwa na Jakaya?

Hebu toeni pumba zenu hapa!
 
Dr. Slaa alisema itafika wakati hii nchi haitatawalika.........wakabisha. :smash::smash::smash::smash:
 
Nakumbuka JK alishaombwa na wakili wa Mahalu Marando Mabere atoe maelezo kwa maandishi kama ushahidi JK alikataa huku Mzee mkapa aliwasilisha maelezo yake sasa hebu toone leo mambo yatakuwaje.
 
Huyo wakili aliyemwambia Mahalu amtaje raisi kwenye issue ya wizi mjanja sasa anataka mzazi aende lupango apate mpunga kenye kuomba rufaa.............Mawakili mbingu hawataiona ona mzee mzima anavyo mchinjia baharini Prof Mahalu mchana peupe.....kisa mpunga tu! mzazi Mabere Marando hiyo noma kaka

Mahalu mzazi hapo hutoki andaa mpunga wa kukatia rufaa.
 
Kesi inayoondelea mahakamani dhidi ya aliekuwa balozi wa Tanzania mjini Roma Prof Mahalu; leo katika utetezi wake kasema kuwa Raisi Kikwete by then waziri wa mambo ya nje alifahamu na kubariki ununuzi wa jengo la ubalozi wetu Italy ambalo lilipelekea aliyekuwa balozi wa wakati huo Prof Mahalu kushtakiwa kwa kuliingizia taifa hasara ya mamilioni ya Euro....

Prof mahalu katika utetezi wake kasema Kikwete alipokuwa waziri wa mambo nje mnamo mwaka 2001 alitembelea nchini Italy na kukagua mjengo huo.....na aliuliza iweje ununuzi wa jengo uwe na mikataba miwili akaambiwa ni kawaida kwa ununuzi wa majengo ya bei nafuu kama lile......

Wakuu, kwa bahati naifahamu sana hii kesi kabla hata ya kufikishwa mahakamani na kwamba Mahalu alifungua kesi kusema vyombo vya habari vimemkashifu kusema kwamba atashitakiwa kwa kununua kuwa na mikataba miwili ya jengo moja, mkataba mmoja ukiwa wa kughushi. Kesi hizo zilipoteza maana baada ya TAKUKURU kumfikisha mahakamani.

Sasa naona hapa Profesa wa Sheria, na wanasheria wake wanacheza na saikolojia ya watu na si sheria ambayo ameifundisha kwa umahiri mkubwa kwa miaka mingi. Haihitaji utaalamu wa sheria kujua kwamba kesi iliyopo mahakamani si ya UNUNUZI WA JENGO, maamuzi ya ununuzi wa jengo ni halali na ununuzi wa jengo ni halali ila tatizo ambalo ndiyo msingi wa kesi ni kuwapo mikataba miwili, ambayo kisheria ni kosa la jinai. Mwanasheria wa Italia aliyefika Tanzania na kutoa ushahidi na baadaye kutoa ushahidi kwa njia ya mtandao (ilileta utata, mahakama ikahalalisha) na mara zote alisisitiza kwamba mkataba mmoja ambao ni wa Euro milioni 3 ulikua batili na hautambuliki na serikali ya Italia.

Hakuna nchi yoyote inayoweza kuhalalisha jambo ambalo Profesa wa Sheria, Costa Mahalu anajaribu kuuaminisha umma kwamba waliweka mikataba miwili ili kupata unafuu. Tujiulize, unafuu wa nini? Hivi anataka kutuambia kwamba akiwa Mwanasheria na MWanadiplomasia, alikuwa akishirikiana na raia wa Italia kukwepa kodi ya Italia? ama anataka kutuaminisha nini? anawafundisha nini raia wa kawaida wanaobanwa na TRA kulipa kodi wanapouza ama kununua majengo na rasilimali nyingine? je, haiwezi kuwa mgogoro wa Kidiplomasia kama Tanzania kupitia balozi wake inaanika utaratibu wa kughushi? je, wakaguzi wa mahesabu wa Tanzania wataandika nini katika vitabu vyao?

Ushiriki wa Kikwete:
Kikwete kama binaamu anaweza kuwa na mapungufu yake mengi jambo ambalo hapa si mahala pake, lakini hebu tuangalie maelezo ya Mahalu ambayo yanashabikiwa kwamba "amemlipua Kikwete". Mahalu anasema, Kikwete alicheka alipoambiwa kwamba kuna mikataba miwili na kwamba hakusema chochote. Sasa jamani wakuu wangu, hivi taratibu za kazi, na kama mwanasheria makini Mahalu anahalalishiwa kughushi kwa Waziri wake (JK) kucheka? Kwamba Kikwete alijua na aliliambia Bunge kwamba jengo la ubalozi limenunuliwa na utaratibu umefuatwa ni sawa kabisa maana yeye kama Waziri alimpa kibali (Power of Attorney) Balozi Mahalu. Sasa kwa Balozi kupewa kibali cha kununua jengo na kukabidhiwa Euro milioni 3, ilihalalisha kununua jengo kwa Euro milioni 1? ama alihalalishiwa kununua kwa milioni 3 na kuandaa mikataba miwili mmoja ukiwa wa kienyeji? Kwamba Waziri (JK) alimshukuru mama mwenye nyumba kwa kuwauzia jengo ambalo lilikuwa linagombewa na watu wengine ndio uhalali wa kughushi?

HATI YA KIAPO YA MKAPA.

Utetezi pekee ambao unaweza kumsaidia Mahalu (Kama mawakili wa serikali wakizembea) ni hati ya kiapo aliyoitoa Mkapa kwamba alitambua kuwapo kwa mikataba miwili. Kama Rais wa wakati huo, alikuwa na mamlaka makubwa na kwa urafiki wake na Mahalu, si ajabu Mkapa ndiye mhusika mkuu katika suala hili (na si JK) na itakumbukwa hata aliyekuwa Katibu Mkluu Kiongozi, Matern Lumbanga, alimkaba Mahalu na taarifa zinaonyesha kwamba Mahalu alikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Mkapa na kuwa alikuwa anamzunguka Waziri, Katibu Mkuu wake na hata Katibu Mkuu Kiongozi, na ndio maana Mkapa (ajabu sana) kama Rais Mstaafu amethubutu kuandika kiapo akitetea uhalifu (na watu wamekaa kimya) kwamba alitambua kuwapo mikataba miwili mmoja ukiwa wa kughushi. Kwa kuwa ni kazi kubwa kwa Rais Mstaafu kufikishwa mahakamani na kwa mazingira ya sasa ya kisiasa, hili linaweza kuwa sababu ya Mahalu kupona, lakini mazingira pia ya kisiasa yanaweza kumponza Mkapa na Mahalu wake, na baadaye Kikwete kama wanasheria wake na yeye mwenyewe hatakuwa makini. Lolote linaweza kutokea maana Tanzania hutokea mambo ambayo hayawezi kutokea popote duniani. Ikiwa kesi hii itaendekea hadi mabadiliko ya Katiba na pengine baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, hadithi inaweza kuwa nyingine maana matokeo ya uchaguzi pia yaweza kuwa chachu ya kesi hii na nyingine, kutegemeana na mshindi wa kiti cha urais.

Profesa Mahalu alidai kuwa katika mazungumzo hayo, Kikwete alimwuliza mama huyo: "Hivi ni kwa nini kunakuwa na mikataba miwili?" na mama huyo alimjibu kuwa hiyo ni kawaida kwa Italia ukitaka kununua jengo kwa bei nafuu.

Profesa Mahalu aliendelea kudai kuwa baada ya kupewa jibu hilo, Kikwete hakuzungumza tena zaidi ya kucheka na kwamba mwenye jengo alimkumbusha kuhusu malipo ya awali ya dola milioni moja za Marekani ambapo aliafiki na kuahidi kuwa zingelipwa kabla ya mwisho wa mwaka 2001.
Profesa Mahalu alidai pia kwamba Kikwete alimweleza mama huyo kuwa atalishughulikia suala hilo baada ya kurejea Dar es Salaam na kumshukuru kwa kuwauzia jengo zuri.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Profesa Mahalu alidai kuwa baada ya Kikwete kusema maneno hayo, alimgeukia na kumwambia: "Costa ni vizuri tupate hela tumlipe huyu mama watu wengine wasije wakachukua hili jengo."
 
Kwani ni nini kinazuia Mahakama/wakili wa Mahalu kumuita Kikwete kama key witness wa defense?

Mkuu, Kikwete ni shahidi upande wa serikali (mashitaka) na hati yake ya dhamana imetumika katika mashitaka maana ametoa kibali cha Euro milioni 3 na ununuzi ni milioni moja na ndio Thisday waliandika story kabla ya kesi ikisema, "Abuse of Power" kwamba Mahalu ametumia vibaya madaraka aliyopewa na Waziri
 
Huyo wakili aliyemwambia Mahalu amtaje raisi kwenye issue ya wizi mjanja sasa anataka mzazi aende lupango apate mpunga kenye kuomba rufaa.............Mawakili mbingu hawataiona ona mzee mzima anavyo mchinjia baharini Prof Mahalu mchana peupe.....kisa mpunga tu! mzazi Mabere Marando hiyo noma kaka

Mahalu mzazi hapo hutoki andaa mpunga wa kukatia rufaa.

Hv mkuu unajua taaluma ya prof Mahalu au umeamua kurukia?wanajua wafanyalo,sema labda kutokana maelekezo toka ngazi fulani itamlazimu prof kuonja hata mwaka kwa bifu lililojificha kati ya watatu hao!ila believe me,mema na mabaya yote ulipwa hapa hapa duniani.
 
Mahalu ni mwizi aliyekubuhu anatumia mgongo wa kujuana na Mkapa na Kikwete kujinasua na kesi mahakamani. Kwani uwizi wote unaofanyika hapa nchi kikwete anajua kwa kuwa ni Rais wa nchi? nonsenses zingine hazilingani na hadhi ya uprofesa.

Kumbe Mahalu 'aliiba' JK akiwa Rais?.....no wonder JK alisema hawajui wamiliki wa DOWANS
 
[h=3]KESI YA MAHALU:MKAPA AKUNJUA MAKUCHA[/h]
date.png
9:37 AM
user.png
Happiness Katabazi
comments.png
No comments

.UTETEZI WAKE WAMGUSA RAIS KIKWETE
.AUWASILISHA RASMI MAHAKAMANI DAR

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE utetezi wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, umetua rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam.


Mkapa ambaye ni shahidi wa pili wa kesi hiyo alitoa utetezi huo ambao unaweza kuandika historia mpya katika mwenendo wa kesi nchini, kupitia kiapo chake ambacho kimewasilishwa mahakamani na wakili wa mshtakiwa huyo, Mabere Marando.

Katika moja ya vipengele 13 vya kiapo hicho, pasipo kutaja jina, maelezo ya kiongozi huyo mstaafu yanamgusa Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati Mkapa akiwa madarakani alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Hiyo inakuwa ni mara ya kwanza kwa rais mstaafu, kutoa utetezi mahakamani kwa kesi inayomgusa mmoja wa waliokuwa wateule wake wakati akiwa madarakani.

Kesi hiyo Namba 1/2007 ambayo Mahalu anashtakiwa pamoja na Grace Martin inasikilizwa na Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilivin Mugeta.

Katika kesi hiyo, Mahalu na Martin wanatuhumiwa kwa wizi wa shilingi bilioni tatu katika ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Rome.

Katika hati ya kiapo chake cha Machi 31 mwaka huu, ambayo imeandaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Nyaraka (The Registration of Documents Act, Cap. 117 of 2002), Mkapa anaeleza kuwa kila kilichofanywa na Mahalu kilikuwa sahihi na kilikuwa na baraka ya serikali aliyokuwa akiingoza toka mwaka 1995-2005.

Ushahidi huo wa rais Mkapa ambao Tanzania Daima inayo nakala yake, umeorodhesha maelezo yake yaliyoainishwa katika vipengele 13.

Mkapa katika utetezi wake huo anadai kuwa mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo la ubalozi lililoko katika mtaa wa Vialle Cortina d'Ampezzo 185 mjini Rome ulizingatia sera ya serikali ya upatikanaji au ujenzi wa majengo ya kudumu ya ofisi na makazi na kwamba ulizingatia maslahi ya taifa.

Hati hiyo ya kiapo ambayo tayari wakili Marando amesema ameishaiwasilisha pia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Eliezer Feleshi, inaanza kwa kusema, "Mimi Benjamin Mkapa, mtu mzima, Mkristo, mkazi wa Dar es Salaam, ninaapa kama ifuatavyo, 'nilikuwa Rais mtendaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi viliwili mwaka 1995-2005 na nina uhakika wa yote haya nitakayosema ndani ya kiapo hiki.'

Katika kiapo hicho Mkapa anadai pia kuwa alifahamishwa na watendaji wa serikali aliyokuwa akiingoza jinsi mchakato uliofanyika na ripoti za uthamini wa serikali zilizotumika katika kufikia hatua ya kununua jengo hilo la ubalozi.

Anadai kuwa tathmini ya jengo hilo ambalo Mahalu anadaiwa kufanya udanganyifu na wizi kwa kulipa fedha kinyume na ilivyotajwa katika mkataba ambayo ilifanywa na serikali ya awamu ya tatu kupitia wizara mbili tofauti, Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Ardhi na Maendeleo Mijini.

Anaendelea kudai kuwa, anatambua kuwa ripoti ya serikali ya uthamini wa jengo hilo iliandaliwa na Wizara ya Ujenzi kwa kiwango cha dola za Marekani milioni tatu na Wizara ya Ardhi kwa thamani ya euro milioni 5.5.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ulikuwa wa aina mbili, mmoja ni rasmi na mwingine wa kibiashara na kuongeza kuwa kwa mujibu wa taratibu ya serikali ya Italia na kuwa hilo lilifanyika kwa baraka za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Utaratibu kama huo wa mikataba miwili ushawahi kufanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale ambapo ilionekana haja kwa kuzingatia maslahi ya taifa kwanza....na kuwa ni mimi ndiye niliyezindua jengo hilo la ubalozi Februari 23 mwaka 2003," anadai Mkapa.

Shahidi huyo wa Mahalu anadai pia kuwa kwa mujibu wa kiapo chake anakumbuka vyema taarifa ya serikali iliyotolewa bungeni Agosti 3 mwaka 2004 iliyosema na kuthibitisha kuwa taratibu zote zinazohusiana na manunuzi ya jengo kwa mujibu wa maelekezo ya serikali, zilifuatwa na kwamba muuzaji wa jengo hiilo alilipwa fedha zote.

Kumbukumbu ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kwamba, Agosti 3, 2004, Kikwete alitoa maelezo bungeni kuhusu utata uliokuwapo awali kuhusu ununuzi wa jengo hilo la ubalozi.

Kikwete katika maelezo yake hayo ambayo yako pia katika kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) anaeleza, "Mheshimiwa Naibu Spika mwaka 2001/02 wizara ilinunua jengo la ubalozi counsel katika ubalozi wa Rome katika jitihada za kuondokana na tatizo la kupanga majumba ya watu huko nje na pia kupunguza gharama za kuendelea kulipa pango la nyumba kila mwaka.

"Ununuzi wa jengo hili ulifuata taratibu zote za manunuzi ya majengo ya serikali kwa kuzishirikisha wizara za ujenzi, ardhi na maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Fedha.

"...Jengo lilifanyiwa tathmini na wataalamu wetu na kukubaliana na ununuzi wa Euro 3,098,781.40 tarehe 6 Machi 2002 fedha za awamu ya kwanza katika ubalozi wa Rome zilipelekwa nazo zilikuwa shilingi 700,000,000 tarehe 28 Juni 2002 zilipelekwa shilingi 120, 000,000.

"Mwishoni mwa tarehe 26 Agosti mwaka 2002 zilipelekwa shilingi 1,000,000,000 jumla ya fedha zilizokuwa zimepelekwa zikafikia shilingi 2,900,000,000 na baada ya hapo ubalozi wetu ulitekeleza taratibu zote za ununuzi wa jengo na kumlipa mwenye nyuma kiasi hicho cha fedha," alieleza Kikwete.

Akimwelezea Mahalu katika utetezi wake, Mkapa alidai katika kipindi chote alichokuwa rais wa nchi alifanya kazi na mshtakiwa huyo katika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma na kwamba mshtakiwa huyo ni mtu wa tabia njema, mkweli, mwaminifu na mchapaji kazi.

Mkapa anahitimisha utetezi wake kwa kueleza kuwa, kutokana na mwenendo huo wa kutukuka, Rais wa Italia alimpatia moja ya tuzo za heshima yenye hadhi ya juu kabisa ya taifa hilo Profesa Mahalu, muda mrefu baada ya balozi huyo kuwa ameshaondoka nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha mahakamani ushahidi huo wa Mkapa jana, wakili Marando alisema mteja wake anakusudia kupeleka jumla ya mashahidi 10.

Mashahidi hao ni mteja wake (Mahalu), Mkapa, Rais Jakaya Kikwete, kwani wakati akinunua jengo hilo ndiye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ndiye alimpa mteja wake nguvu ya kisheria ya kuendelea na ununuzi wa jengo hilo, aliyekuwa waziri wa Ujenzi wa John Magufuli na mashahidi wengine na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba ambaye pia anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bil. 11.7.

Kuwasilishwa kwa hati ya kiapo cha Mkapa mahakamani hapo, kumekuja baada ya Hakimu Mkuu Mfawidhi Ilvin Mugeta kusema kuwa yeye ndiye amejipangia kusikiliza utetezi wa washtakiwa hao Aprili 28 mwaka huu.

Hatua ya Hakimu Mugeta kusikiliza utetezi huo inakuja baada ya Machi 28 mwaka huu, Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye ndiye aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo tangu awali kujitoa baada ya mawakili wa washtakiwa kuwasilisha sababu sita za kumwomba ajitoe kwa sababu kukosa imani naye Machi 25 mwaka huu.

Mapema mwaka 2007, Jamhuri kupitia mawakili wake toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincoln na Ponsian Lukosi iliwafikisha mahakamani hapo kwa mara ya kwanza washtakiwa hao kwa makosa ya uhujumu uchumi, wizi wa zaidi ya euro milioni mbili wakati wakisimamia ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Rome nchini Italia.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Mei 6 mwaka 2011.
 
Halafu wakuu, hivi kama iwe ni kweli Kikwete alishirikiana na Mahalu kuiba, huo unaweza kuwa utetezi? Nadhani hapa Mahalu na wanasheria, wangejikita kueleza uhalali wa kuwapo mikataba miwili kisheria na si waliruhusiwa na nani? Angalieni hata kesi ya mauaji ya kina Zombe, hakukua na uhalali wa eti Zombe alitoa amri ya kuua, sembuse wizi? hakuna amri ya mtu kutenda kosa la jinai. Kama unekamatwa jitetee, usiseme niliiba na Halisi, sasa Halisi akikamatwa wewe utaachiwa kweli kwa kusema "muliiba naye" ama "alituhusu", au kwa Mkapa kuhalalisha, hivi kweli inawezekana mtu kusema "nilimtuma mtu kuiba?" Afadhali ya kesi ya Mramba angalao anaweza kusema alifanya maamuzi kwa kutumia Notisi ya Gazeti la Serikali (GN) ambayo ni halali na ilielekeza kabisa kusamehe kodi kwa Alex Stewarts sasa hapa Mahalu yeye anasema kuna barua ya kuruhusu kununua jengo!!! si kuruhusu kughushi, anao hati ya idhini inayompa mamlaka ya kununua, si kughushi. Tusubiri labda atatoa ushahidi zaidi, maana anaendelea. Ila nina wasiwasi hata JF itajadiliwa mahakamani maana hii kesi ina maslahi na watu wengi sana ambao wanafanya kazi usiku na mchana.
 
Back
Top Bottom