Mahalu, Grace waachiwa huru, ndugu wamwaga machozi ya furaha

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015

Mahalu, Grace waachiwa huru, ndugu wamwaga machozi ya furaha​



FRIDAY MAY 07 2021​

professapic

Balozi Costa Mahalu akikumbatiana na mmoja wa ndugu zake mara baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuachia huru dhidi ya tuhuma za uhujumu uchumi. Picha na Maktaba.

Summary

  • Mashahidi saba wa Jamhuri waliosaidiwa na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani kuthibitisha kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania, Rome, nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Ofisa Utawala katika ubalozi huo, Grace Martin havikumshawishi hakimu kuwa wanadiplomasia hao walikuwa na hatia.


By James Magai
More by this Author

Mashahidi saba wa Jamhuri waliosaidiwa na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani kuthibitisha kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania, Rome, nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Ofisa Utawala katika ubalozi huo, Grace Martin havikumshawishi hakimu kuwa wanadiplomasia hao walikuwa na hatia.

Hatimaye Agosti 9, 2012 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimwachia huru Profesa Mahalu na Grace, ikisema kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha kuwa walitumia nyaraka za kughushi kwa nia ya kuipotosha Serikali inunue jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa bei iliyoongezwa kinyemela.

Baada ya kesi hiyo kuunguruma kwa miaka mitano, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ilvin Mugeta alisema ununuzi wa jengo hilo ulifuata taratibu zote za kiserikali na kwamba Profesa Mahalu alipata ruhusa na baraka zote za mamlaka ya nchi kununua jengo hilo kwa niaba ya Serikali.

Profesa Mahalu na Grace walishitakiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2007 kwa makosa sita, likiwamo la kula njama, kutumia nyaraka za ununuzi wa jengo la ubalozi kwa lengo ka kumdanganya mwajiri wao (Serikali) na wizi wa Euro 2,065,827 (zaidi ya Sh2.5 bilioni).

Kesi dhidi ya Profesa Mahalu ilikuwa imejipatia umaarufu na mvuto wa pekee tangu siku ya kwanza kwa kuwa ilimhusisha balozi, mwanasheria nguli na aliyewahi kuwa mkuu wa kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Upekee na mvuto wa kesi hiyo uliongezeka pale aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alipoorodheshwa kama mmoja wa mashahidi watakaomtetea Profesa Mahalu.

Related​



Bila kujali hadhi yake ya Rais mstaafu, Mkapa alipanda kizimbani kumtetea rafiki yake, Profesa Mahalu na kuchuana vikali na mawakili wa Serikali inayotokana na chama chake.

Katika ushahidi wake, Mkapa aliieleza mahakama kuwa alimfahamu Profesa Mahalu kuwa ni msomi mzuri, mwadilifu, mfanyakazi mwaminifu na kiongozi wa haki.

Kitendo cha Mkapa ambaye alielezwa kuwa mmoja wa marafiwalio karibu wa Profesa kumtetea kilimfanya avunje rekodi ya kuwa Rais wa kwanza mstaafu, si tu Tanzania bali kwa Afrika kusimama kizimbani kumtetea mteule wake.

Serikali ya Tanzana ilifanya uamuzi wa kununua jengo la ubalozi nchini Italia Septemba, 2001. Ununuzi wa jengo hilo ulifanywa kupitia mikataba miwili iliyofungwa siku moja ikiwa na bei tofauti.

Mkataba wa kwanza ulionesha kuwa bei ya kununulia jengo hilo ilikuwa Euro 1,032,913.80 wakati mkataba wa pili ulionesha bei ya jengo hilo ilikuwa Euro 3,098,741.40.

Ushahidi ulioletwa mahakamani unaonesha kuwa malipo ya bei ya ununuzi wa jengo hilo yalifanywa Septemba 2002 kupitia akaunti mbili tofauti, ya kwanza ikionesha malipo ya Euro 2,065,827.60 na malipo mengine ya Euro 1,032,913.80 yaliwekwa kwenye akaunti nyingine.

Ni kwa msingi wa mikataba hii miwili na tofauti ya malipo, Jamhuri iliamini kuwa kulikuwa na kughushi nyaraka na wizi wa fedha za Serikali Euro 2,065,827.60 na kuwashitaki wanadiplomasia hao.

Hukumu yasomwa

Akisoma hukumu yake, Mugeta alisema kuwa kesi ya Jamhuri ilijikita zaidi kwenye ushahidi wa mazingira na kwamba hapakuwa na ushahidi wa wazi kwamba washitakiwa waliiba pesa.

Alisema ingawa hakukuwa na shaka kuwa jengo hilo lilinunuliwa kupitia mikataba miwili, alikubaliana na upande wa utetezi kuwa utaratibu huo ulitumika kwa kuwa ulikwa sharti lililowekwa na muuzaji.

Muuzaji huyo aliiambia mahakama kuwa nchini Italia huo ulikuwa utaratibu wa kawaida kwamba mnunuzi atataka kuandaliwa mikataba miwili; mkataba rasmi ambao utasainiwa na kusajiliwa ukiwa na bei rasmi na mwingine utakaoonesha bei ya soko.

Kwa utaratibu huo, mkataba wa pili hufanywa bila kuhusisha usaidizi wa serikali na hata shahidi wa pili wa upande wa mashitaka alidai kuwa mikataba ya hivyo hufanywa kwa siri.

“Kutokana na maelezo hayo, itaonekana kwamba nadharia ya upande wa mashitaka kuhusu kula njama ilijengwa tu kwenye suala la kutumia mikataba miwili. Sitakuwa tayari kukubaliana na nadharia hiyo hadi pale nitakaposhawishiwa bila kuacha shaka kwamba matumizi ya mikataba miwili kununua jengo hilo ulitengeneza jinai,” alisema Mugeta.

Upande wa mashitaka ulidai pia Profesa Mahalu alitumia mikataba hiyo miwili bila ruhusa huku upande wa utetezi ukisisitiza kuwa alikuwa na baraka zote kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Matern Lumbanga ambaye alidai kuwa hakuwahi kutoa ruhusa hiyo.

“Nimesema kabla kuwa suala hilo halina mashiko kwa sasa. Suala kubwa ni kama kuingia katika mikataba miwili kulitengeneza kosa la jinai,” alisema.

Mugeta alisema kama Serikali ilikubali na kutuma pesa za kununulia jengo hilo ilimaanisha kuwa ilijiridhisha na kuridhika na taratibu zilizotumika kufikia makubaliano ya bei ya kununulia jengo hilo.

Alisema hapakuwa pia na ushahidi wa kuonesha kuwa pesa zilizolipwa ziliwarudia wanadiplomasia hao.

Alisema pia kuwa upande wa mashitaka unaweza kuwa kwa makusudi umekwepa kuleta mahakamani vielelezo vya muhimu vinavyothibitisha bei halali kuzuia bei iliyopendekezwa katika ripoti ya uthamini wa jengo iliyopendekezwa na ofisa wa Tanzania.

Mtaalamu wa uthamini majengo kutoka Tanzania alipelekwa Rome kukagua jengo hilo na kuonesha kuwa bei ya jengo hilo inaweza kufikia Euro 5 milioni.

Hakimu huyo alihoji kwa nini upande wa mashitaka haukuleta mahakamani ushahidi wa ripoti hiyo ya uthamini wa jengo lililotaka kununuliwa. “Kwa kushindwa kuleta ripoti hiyo, upande wa mashitaka umeshindwa kuleta nyaraka ya muhimu sana katika kuamua kesi hii.

Madai yao hayawezi kuthibitishwa na matumizi ya mikataba miwili, hayakutengeneza kosa la jinai katika kesi hii,” alisema Mugeta.

Upande wa mashtaka ulidai pia kuwa mwanadiplomasia huyo alitumia mikataba miwili kununua jengo hilo akijua kuwa sheria ya Tanzania haikumruhusu kutumia mikataba miwili kununa jengo hili lakini aliendelea kufanya malipo kwa nia ovu.

Hata hivyo, Mugeta aliikataa hoja hiyo na kukubaliana na upande wa utetezi kuwa Profesa Mahalu alipewa nguvu ya kisheria (power of attorney) kusimamia malipo ya fedha, yakiwemo ya ununuzi wa jengo la ubalozi.

Machozi ya furaha

Muda mfupi baada ya kuachiwa, Profesa Mahalu alisema: “Acha yaishie hapa. Sina nia yoyote ya kuishitaki Serikali kwa mashitaka ya kubambikiwa au kudai fidia,” alisema na kuongeza: “Nawashukuruni sana wote. Mungu siku zote huwatetea waliokandamizwa.

Siku zote haki hutoka kwa Mungu…na leo wote ni mashahidi Mungu amefanya haki itendeke,” alisema Profesa Mahalu, huku akijaribu kuficha furaha ya kuachiwa. Ndugu, jamaa na marafiki wa washitakiwa hao waliofurika katika chumba cha mahakama walishindwa kujizuia na kutiririkwa machozi ya furaha pale hakimu alipotangaza kuwa ndugu zao hawakuwa na hatia na wako huru.

Mke wa Profesa Mahalu, Vulfrida alibubujikwa machozi ya furaha nje ya mahakama na kumkumbatiwa mume wake, asiamini kilichotokea mahakamani.
 
Mtuhumiwa tajwa hawezi kuwa na kosa kwa kuwa alipata baraka zote toka kwa mteule na mamlaka husika. Hata kama kulikuwa na shaka kwenye ununuzi wa jengo? Ilibidi valuer acheze nafasi yake vizuri na kwa weledi na kikamilifu kwa kufata taratibu za kazi yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom