IOMBEENI CHADEMA IKUBALI MARIDHIANO

IOMBEENI CHADEMA IKUBALI MARIDHIANO

Scott junior

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2022
Posts
3,204
Reaction score
4,615
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukutana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki kupitia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Ikulu.

Akizungumza leo Agosti 12, 2026 na Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa Kilosa Mjini, Mkoani Morogoro, Hapi amewataka Maaskofu hao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili waondokane na pepo ya ukaidi na kuitikia wito wa kwenda kwenye meza ya maridhiano.

Hapi amesema Rais amekuwa akitoa nafasi kwa Vyama vya Siasa kukutana na kujadiliana kuhusu masuala ya Taifa, lakini CHADEMA hawajaitikia wito huo.

Amesema TEC imeonyesha mfano kwa kuitikia mwaliko wa Rais na kukutana naye, hivyo amewaomba Maaskofu kutumia nafasi yao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili nao wafunguke na kuona umuhimu wa mazungumzo.

“Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA, Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi.
#MillardAyoUPDATES
IMG_2507.png
 
CCM alishinda uchanguzi kwa haki (kulingana na maelezo ya tume ya uchaguzi)na CHADEMA hakuwa sehemu ya huo uchaguzi kwanini maridhiano?

Watu waliokufa sio wanachama wa CHADEMA ni raia tu ambao wana vyama na wasio kuwa navyo kwanini wanalazimisha maridhiano ya CHADEMA vs CCM na sio maridhiano ya serikali na wananchi(familia zilizopoteza wapendwa wao)?

Kama ni maridhiano ya kisiasa basi CCM awatafute ACT-Wazalendo, CHAUMA na vyama vyote vilivyoshiriki uchanguzi ambao CCM alitangazwa mshindi kwa kishindo.

Samia hebu tafuta washauri wazuri acha kulea upumbavu.Watu walikufa hamtaki kufanya toba kwa hizo damu zilizo mwagika kutwa kukimbizana na viongozi wa CHADEMA wasio na hatia mnadhani hizo damu zitatulia sio?(hii nchi haiwezi kurudi kama mwanzo bila toba ya kweli)
 
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukutana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki kupitia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Ikulu.

Akizungumza leo Agosti 12, 2026 na Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa Kilosa Mjini, Mkoani Morogoro, Hapi amewataka Maaskofu hao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili waondokane na pepo ya ukaidi na kuitikia wito wa kwenda kwenye meza ya maridhiano.

Hapi amesema Rais amekuwa akitoa nafasi kwa Vyama vya Siasa kukutana na kujadiliana kuhusu masuala ya Taifa, lakini CHADEMA hawajaitikia wito huo.

Amesema TEC imeonyesha mfano kwa kuitikia mwaliko wa Rais na kukutana naye, hivyo amewaomba Maaskofu kutumia nafasi yao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili nao wafunguke na kuona umuhimu wa mazungumzo.

“Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA, Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi.
#MillardAyoUPDATESView attachment 3648958
zezeta lililotukana wazee kuwa wakae kimya muda wao umeisha leo linatoa ombi la maombezi, kwani hili zezeta limeshindwa kukaa na chaumma,Act ya zito aliyesema chama chake pekee ndio kinawezafanya maandamano na wale wajinga kumi na nne.
 
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukutana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki kupitia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Ikulu.

Akizungumza leo Agosti 12, 2026 na Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa Kilosa Mjini, Mkoani Morogoro, Hapi amewataka Maaskofu hao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili waondokane na pepo ya ukaidi na kuitikia wito wa kwenda kwenye meza ya maridhiano.

Hapi amesema Rais amekuwa akitoa nafasi kwa Vyama vya Siasa kukutana na kujadiliana kuhusu masuala ya Taifa, lakini CHADEMA hawajaitikia wito huo.

Amesema TEC imeonyesha mfano kwa kuitikia mwaliko wa Rais na kukutana naye, hivyo amewaomba Maaskofu kutumia nafasi yao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili nao wafunguke na kuona umuhimu wa mazungumzo.

“Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA, Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi.
#MillardAyoUPDATESView attachment 3648958
Hapa ndio nimejua kwa nini sura za viongozi wa TEC wakati wanatoka kwenye huo Mwaliko zilikuwa zimenuna!
 
Back
Top Bottom