Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 260
Katika maadhimisho ya miaka 34 ya ccm jk alitoa hotuba inayogusa mambo mbalimbali,
1.Dowans,anasema eti hata yeye anashangazwa na hilo swala la dowans,kwa amiri jeshi mkuu,mwenye mamlaka kamili anatoa kauli ya ajabu,badala ya kueleza mikakati ya kuzuia uhaini na ubakaji uchumi,ni dhahiri amekosa uhalali wa kuwa rais
2.Mauaji ya arusha,et yalisababishwa na chama flani kwa malengo ya kisiasa,ikiwa hana uelewa wa kujua chanzo cha vurugu arusha,kuwa ni uchakachuaji wa meya,na ni vita kati ya haki na udhalimu,jambo ambalo kila mtu analijua,Jk kushindwa kuujua ukweli huu umekosa uhalali wa kuwa rais
Jk simamia haki na ukweli
saa ya ukombozi ni sasa
Kama ni kweli kaongea hivyo basi nchi hii haina kiongozi. Tuvumilie tu tupate kiongozi muafaka ifikapo 2015.
This is very strange!
A president, head of State, Chief in Command wenye kila resource mkononi mwake hajui nani anataka kuibia wananchi wake.
Kwenye kikao anachojisifu kukisimamia mwanachama wake (mwakyembe) kamtaja mmiliki kwa nini asimwite chemba kupata taarifa zaidi?
Kama ni kuua soo bora angesema "Nimesikia kuna watanzania wenzetu wanamasilahi kwenye Dowans, tunafuatilia ili kubaini ukweli ila wanapaswa kujua hii ninchi yetu sote, madhara ya kuihujumu wao hawawezi kusalimika"
Mie hata sijui kina nani wanamshauri cha kuongea
Hivi mtu akiiba gari akakuzia, wewe ukashikwa na hiyo Gari, utaachiwa kuwa nalo au utanyanganywa? na hela hurudishiwi na serikali/na mwenye gari aliyeibiwa.Ndo maana hata miye nasema hawa viongozi wetu mabwege issue simple wanazunguka mbuyu .ila hiyo hela ikilipwa mi nalia na WALOVUNJA MKATABA..Halafu mazee siko kwenye system nko bush .struggling like other village WALIPE WASILIPE HAINIPI HEADACHE huwa nachoka tu kila sku dowans dowans i get fedup
Nafedheheka kuwa mtanzania, kuwa sehemu ya kizazi hiki ambacho kinajisifia kwa kuwa inactive ktk fikra na vitendo; ambacho suluhisho lamatatizo yako ni kukubali yaishe, na kinamwachia mwenye nguvu aamue lini atatoa haki... Na aspoitoa basi, tukae tu...tutafanyaje. Huu ni unini jamani?! Hauna hata adjective yake, aaaaaagghhhhh!