Sorry, Rostam ni Jambazi, ni wazi kwa wakati wa sasa hata watoto wadogo wanamjua Rostam na ushenzi wake katika taifa hili lilojaa ufisadi.
Kwahiyo Hoja ni kwamba:
Bora Jambazi kuliko JK, Kwanini?
Rostam tushamjua ni
jambazi kwahiyo yeyote popote akimwona ni sawa na uko stand umemwona kibaka unayemjua, la kwanza kama sio kuiarifu dola basi ni kutafuta upenyo wa kukwepa kukabwa muda uendapo. Tofauti yake na JK ni kwamba kwasababu JK ni prezidaa aliyependwa na ambaye bado baadhi ya watanzania wasiomjua ukweli wake wanampenda
wanamkubatia kwa nguvu zao zote kwamba atawaokoa hata kama ni baada ya muda fulani wa vita aijuayo yeye mwenyewe, kinachotokea akumbatiwapo anapata nafasi nzuri tena ya kirahisi sana
kuwanyonya damu wananchi kwa ulaini wakidhani anakusanya nguvu za kupambana na majambazi kumbe anakusanya nguvu za kiume pamoja na wenzake kuwajaza mimba watoto wetu mashuleni. Sijasema yeye binafsi kamjaza mwanafunzi mimba, nikipata ushahidi kuhusu hilo nitalileta, ninachosema kiongozi wa serikali akimjaza mwanafunzi mimba kisha serikali ikamtetea ama ikakaa kimya ni serikali hiyo imemjaza mimba mwanafunzi huyo, maanake JK.
Nikimaliza kutetea kichwa changu cha habari naomba niende haraka kwenye hoja yangu ya msingi. Machache niliyoyaona kwa akili yangu mtindi ni kuhusu hotuba ya prezidaa iliyoandaliwa kwa usanii mkubwa. Nimeitafakari kwa muda hotuba hii ya Mh. Msanii wetu kwa muda nikiwa na hasira ambazo ningetamani wabunge wangekuwa nazo wangetoka nje ya ukumbi, tofauti yake walishangilia, labda kama walikuwa wanatimiza wajibu kumshangilia mkuu wa nchi.
Nadhani wote tutakubaliana vyema kwamba siku kadhaa kabla ya prezidaa kuhutubu bungeni wananchi walikuwa na hamu sana ya kujua atachosema na ilifikia hata vyombo vya habari kujaribu kujadili hili kuhusu anatakiwa awaambie nini watanzania ama watanzania wanataraji nini kutoka kwake. Kuna baadhi vilimtetea na kuna baadhi vilimpa ukweli anatakiwa aseme nini, ilifikia chombo chetu cha umma TBC kumleta aliyeitwa mwandishi mwandamizi Jimmy Mdoe kutoa maoni yake. Naye alitema pumba zake kupitia TV kwamba tusijibaraguze sana kuhusu hiyo hotuba hasa kuhusu swala la EPA ambalo alisema Rais anaweza hata asiliongelee, mimi nilihisi mazingira ya kutupumbaza ili tupanue midomo kupokea chakula kabla hata hatujajua ni chakula gani tutachopewa.
Ni mambo ya kushangaza sana tena ya kusikitisha aliyoyaongea prezidaa wetu kulingana na yaliyokuwa yanatarajiwa, ni hotuba iliyoandaliwa kwa usanii mkubwa baada ya kujua wadanganyika wanataka nini. Wengi walisema atazoza sana mambo ya nje ili kutupoteza, akajitahidi kuzoza sana mambo ya ndani kwa upotoshaji mkubwa.
Mimi binafsi nilitaka kujua sana kuhusu EPA na Zanzibar muafaka na nchi ama si nchi, nitayasemea haya kwa ufupi. Jambo la kwanza katika yote ni kwamba prezidaa aliyagawa mambo nyeti kwake katika vifungu na kuyapa vichwa vya habari, niligundua kwamba si swala la EPA au Zanzibar zilokuwa mada muhimu katika mahubiri yake kuwavua upya watanzania. Suala la EPA liliingia kwenye mada ya Uchumi wa nchi hii na halikuwa suala nyeti maana aliliingiza katika maongezi ya kawaida kabisa tena akiliongelea kwa njia rahisi sana kwamba sisi tunajipa presha bure kwa yasiyotuhusu. Naandika kwa machungu mengi ninapokumbuka Rais wa nchi hii alithubutu kuongea wazi kwamba zile pesa hazikuwa zetu na hazina mwenye kuzidai kwa sasa, nilijiuliza, Je,...
unclaimed funds zinaruhusiwa kuiba? Tena aliongeza wazimu mwingine juu yake kwamba shida kubwa imetokea kwa kuwa ilijulikana, kama isingejulikana isingekuwa shida maana hakuna anayedai hizo pesa na sio zetu. Wabunge wakapiga makofi...My God...! Huu sasa sio usanii bali ni ufedhuli uliopita kipimo, ni jambo la kutisha kwa prezidaa kuthubutu kuongea haya mbele ya bunge na wananchi kwa ujumla, ni muhuni wa kutupa huyu,
hafai, ni wa kuogopa kama ukoma...! Ati akasema kwa sauti ndogo kwamba kuna walionyang'anywa passport na wengine kufilisiwa, nilimshangaa sana kwasababu passport za Tanzania hazihitaji jitihada kuzipata, hata kwa wauza gahwa mitaani ukitaka utazipata, kikubwa pesa yako tu. Kingine sio kazi mtu kutoka nje ya Tanzania, sio kupitia vichochoroni bali kwa njia halali, wengi wanaelewa nisemacho kwahiyo sina haja ya kufafanua. Akasema kuna waliofilisiwa hawana chochote kwa sasa, kama imeweza kujulikana wazi kuhusu mipango thabiti ya hawa mafisadi kupanga kuiba na kuficha mali zao, itashindikana kujua mambo yanapokuwa magumu na ikabidi kunyang'anyana kile walichokificha? nashangaa sana lakini naamini wachimbuaji wataleta ukweli sio siku mingi, hili kwa akili yangu mtindi naamini
prezidaa kadanganya, tutajua mengi siku si nyingi. Alimaliza kwa kuonyesha wazi kwamba shida yake sio majambazi kwakuwa pesa walikwiba zilikuwa zinaelea tuu na kuna zingine pia, la msingi warudishe hadi Octoba vinginevyo watangulie mahakamani. Ukishindwa kurudisha 50,000 pesa ya Saccos ama Pride uliyokopa haichukui muda wao kukutembelea na kuchukua vimeza vyako kufidia deni. Inasikitisha kuona majambazi wanaotunyanyasa wanapewa muda kurudisha pesa walizoiba, naamini wasipolipa wataundiwa tume ambayo itachunguza kama wanaweza kulipa lini au mwaka gani.
Uongo mwiingine, pesa zimerudi lakini hata JK hajaziona, ati zimewekwa akaunti maalum maana hazitakiwi kuchanganywa lakini yeye binafsi hajaziona.
Huu ni ushenzi mkubwa usioweza kuvumilika maana tumefikia kudanganywa wazi huku tukishangilia na kuona juhudi mahususi za prezidaa kuwaficha majambazi na kupambana na dagaa kwa kuwafunga miaka 240 jela. Sitaki kuongea sana maana nimepata moyo nilipogundua wadanganyika wameshtuka na sasa wanaona hotuba yake ilikuwa usanii, natamani kuona wabunge wakipiga kura ya kutokuwa na imani na prezidaa maana Tanzania itakuwa imeamka na tutasonga mbele na prezidaa atayeheshimu matakwa ya wananchi.
Kuhusu Zanzibar, huyu prezidaa ni mtu wa ajabu sana maana nadhani yeye binafsi amezembea kisha akaona madhara yalotokana na kusubiri muda mrefu bila kushughulikia suala la zanzibar. Katuorodheshea mambo mengi ambayo kamati alizounda zimefanya kuhusu zanzibar lakini hakuna la ajabu alilosema kuhusu nini hatima ya hayo yote wala yataisha lini, nionacho mimi hapa ni usanii ule ule wa kuona kuna kazi inafanyika tangu alipoingia madarakani hadi atakapotolewa kama sio kutoka wakati utakapofika. Sina imani yeyote na huyu mjamaa kwa sasa, ni msanii asiyeishiwa maneno tena huyasemea mambo mazito kama utani wa kijiwe cha kahawa, anaonekana ni mtu yule yule wa kijiweni ambaye hakufaa kupewa nchi hii kwa imani tuliyoionyesha. Kwanini yaliyofanywa yawe siri?
Kwanini kila siku kwenye TV watuonyeshe jinsi miradi ya barabara na PADEP inavyokwenda wasiongee hata siku moja kuhusu nini kimefanyika kuhusu kuusafisha muungano wetu uliojaa matope sasa? Kuna siri gani sasa? Tatizo...! Nisemacho hapa tena ni lazima serikali hata kama basi upumbavu umewakaba wajifunze kuweka wazi mambo fulani kuondoa stress iliyoko kwa wananchi kwamba serikali ni ya kifedhuli, kwanini hawaoni haya?
Mwisho niishie kusema
"usipokubali kuliwa, hutakula" Hii ni kauli aliyoitoa JK wakati akihutubia hiyo majuzi. Wabunge walicheka sana, kisha akarudia tena halafu akacheka sana, akasema "
sikumaanisha hayo" kwa kumtaja mbunge mmoja mswahilina kana kwamba yeye (mbunge) ndio alitafsiri tofauti, kisha akasema sina maana ya mbunge huyo (jina nimelisahau), kisha akarudia tena "
KUBALI KULIWA ILI ULE"
Nilimwelewa hivi; Kwa wanaojua saikolojia ya kuzaliwa hapa kuna mawili,
aidha Kikwete ni muhuni wa kutupa kwa kuongea maneno kama haya akiwa prezidaa wazi akimaanisha lolote kisha kuyarudia, kucheka na kurudia tena haswa ukilinganisha na hali iliyokuwepo, ama Kikwete ni jambazi mkubwa kwa kumaanisha kwamba tusitegemee kula kama hatutakubali kuliwa. Sasa tumeliwa sana, TUTAKULA LINI??? Yawezekana pia kwamba alihofia kuwa amebuma step kuongea hivyo, kwahiyo akatafakari kwanza, lakini ubongo wake ulielemewa kwamba wakati anatafakari lazima avunge hotuba, kwahiyo akajikuta anarudia anacheka kisha anarudia (
reflex action). Je, kama ndivyo alitafakari nini? Hapa nako kuna mawili, aidha alijikumbuka madhambi yake ya kuwala *#%$@#(ke) zetu ili waweze kumla faranga zake ambazo kawaida ni kodi zetu, ama alikumbuka madhambi yake ya kuwala watanzania akiwaahidi kuja kula mafanikio baadaye uchumi wa mafisadi ukitengemaa. Yote mawili yanaonyesha Kikwete ni mhuni wa kutupa au ni jambazi wa kuogopa maana fikra kuhusu dhambi zake zilimtoa kwa muda nje kabisa ya hotuba iliyokuwa inasikilizwa na viongozi wote na mamillioni ya wananchi kwa hamu kubwa ya kupata ukombozi kutoka kwa Fisi anayeaminika kuwa kondoo mnyenyekevu na mtulivu.
Niishie kusema hasira niliyonayo kwa sasa ingekuwa inafaa kuambukiza, ningeacha kazi niliyonayo nianze kuwaambukiza watanzania wote hasira zangu wafanye wafanyalo maana sasa mbele kote ni giza na tunaenda shimoni. Kama ni suala la Mungu nadhani kwa sasa ameacha mambo yawe hovyo ili tuanze upya wakati mwingine, natabiri kasheshe kutokukoma tangu sasa hadi tutapojua mustakabali wetu.
Mungu ibariki Afrika na Tanzania, ila tunaomba ruhusa uwalaani mafisadi wote kulingana na uwajuavyo wewe...!