Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

kafieni na ubaguzi wenu huko, kwani hawa ghasia cy binadamu? Kuwa mnmke2
Wewe ndio ukafie mbali na Ujinga wako wa kufikiri,hapa hatutizami umwanamke au mwanaume issue kwetu ni Performance ya mtu sasa ujinsia unakuja vp hapa wéwe zero brain?
 
Hari mpya nguvu mpya kasi mpya next hari zaidi nguvu zaidi na kasi zaidi.tumedhubutu tumejaribu tumeweza na tunasonga mbele.maisha bora kwa kila mtanzania.IPI ILIYOFANIKIWA kama sio mambo ya kiswahili wenyewe upepo ukivuma wanasema baridi inapga hiyo
 
kafieni na ubaguzi wenu huko, kwani hawa ghasia cy binadamu? Kuwa mnmke2

naisi hujawapata wadau vizuri...hapa kwa HAWA GASIA NA WIZARA ALIYO PEWA TUMELIWA KABISA...
KAMA ALIWEZA KUA WAZIRI UTUMISHI NA TUKAWA NA WAFANYAKAZI HEWA KWA KUTOKUA NFUATILIAJI,JE HUKO AMBAPO FEDHA ZINA TAFUNWA NA MCHWA WA HALMASHAURI NA MIRADI HEWA ATAWEZA..?
KIUKWELI HUYU DADA NI BOGA HAWEZI CHOCHOTE....
 
wakati mheshimiwa rais jk akitangaza majina ya mawaziri wateule hapo jana alisisitiza juu ya kuwajibisha watendaji wote watakaobainika kufanya madudu yaliyopelekea mawaziri kuwajibishwa.

Pia katika hotuba ya makamu wa rais iliyoonekana kwenye T.V stations mbalimbali,naye pia alionekana kusisitiza juu ya kuwashughulikia mafisadi''mchwa'' katika halmashauri mbalimbali nchini.

Je Kauli hizi kutoka viongozi wa juu zinaashiria kwamba sasa tutarajie ile sera ya ''fagio la chuma'' kufanya kazi au ni kiini macho?

Wangesema nini na kufanya nini katika mazingira magumu ya kisiasa waliyo kuwa nayo.That is polotics.
 
Wataapishwa Jumatatu tarehe 8 Mei, 2012 saa 5.00 asubuhi katika viwanja vya Ikulu
Nani atamshauri Rais Kikwete asitumie fedha za wanyonge kwa kusherehesha tukio la kuwaapisha mawaziri na manaibu aliowateua?

Awaapishe ofisini kwake kwa zamu bila kufuja kodi zetu kwa maturubai, maua na kadhalika!
 
Nimekuwa nikijiuliza bila kuwa na majibu kazi ya hii wizara ni nini na je , waziri atakuwa na fungu lake la bajeti na ni la kazi gani?na je atakuwa anaenda bungeni?na je, atakuwa na jengo la wizara ,ukisitaajabu ya musa.....nawaombeni wenye uelewa waniwezeshe ili nitatue na huu ubishi hapa,
 
Hili ndilo baraza lililokuwa linasukwa kwa week mbili? Unampaje unaibu waziri wa nishati na madini Steven Masele na kumuacha geologist Dr Peter Kafumu?....
Mikataba ya kidhalimu na kifisadi ya Madini, inayosafirisha madini yetu kwenda nje ya nchi kila kukicha, huku watoto wetu wakikosa waalimu, madawati na vitabu vya kiada na ziada imehalalishwa na Daktari wa Jiolojia Dalali Petro Kafumu. Stahili yake ni kupelekwa jela, siyo kwenye Baraza la Mawaziri.
 
Nianze na kumpongeza Raisi kwa kubadilisha baraza la mawaziri, bila kuongelea ubora wa baraza la hilo ama mchakato wake, kwani huu ni mjadala mwingine na unaendelea. Mimi nianze na hili baraza tulionalo, maana ndio lishakuwa baraza sasa, na muda wake wa kazi ni miaka mitatu tu. Napata hofu kidogo mabadiliko haya maana sijasikia lengo haswa la baraza hili zaidi ya mabadiliko ya majina dhidi ya shutma za ubadhilifu. Nadhani, tunatakiwa kuwa na matarajio mpya ya kiutendaji au malengo, nami ndio nauliza tutarajie nini Toka baraza letu jipya? Je mabadiliko ya majina ndio lengo kuu?
 
Waliovikwa Mabomu ya mwanzo yamewalipukia, wanawavisha milipuko wengine, watajilipua baada ya miaka miwili. this time watajilipulia magogoniiiiiiiii, mfuatilieni mshkaji aliyeteuliwa ubunge na uwaziri kwa mpigo kutoka bwagamoyo.
 
Rais ameteua kwa kuangalia vigezo gani:baby: Mtu kama Hawa Ghasia ambaye hana uwezo wa kujibu hoja za maandamano ya wafanyakazi unamuweka wizara yenye matatizo makubwa kama TAMISEMI nini kitatokea, ushauri wa bure ulikuwa ni kumpandisha Agrey kuwa waziri kamili hilo ni Jembe.
Acha tuone hilo baraza lililosukwa kama litatusaidia.

Narudia tena Tanzania bado sana maisha haya ya viongozi kulindana mwisho utakuwa mmbaya.Hapa mawaziri ni Magufulu,Mwanry ,Mwakyembe na Tibaijuka wengine ni manung'anyembe Tz iko kazi na Kigoda Tena duuu.
 
Katika hali ya kawaida kuna maneno ama neno ambalo mtu unapolisikia linakupa matumaini ama faraja ambayo hukuwa ukiitazamia. Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi nadhani baada ya Bunge ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuja kuzungumza na wanahabari pamoja na mambo mengine mengi kubwa alilotaka yeye litufikie sisi wananchi ni "ubadilishwaji" wa Mawaziri ila yeye alituma neno "kusuka" neno ambalo binafsi lilinipa kufikiri mbali sana na kuwa na imani kubwa sana. Japo mpaka kesho sijapata kujua kauli ile ilitolewa kama Katibu wa Chama ama kiongozi mwandamizi Serikalini.

Neno kusuka natumai pasi na shaka waungwana kimtazamo, na kimaudhui linaweza tafsiriwa na kutolewa maana ambayo ni tofauti na lile Baraza lililotangazwa jana manake kwangu binafsi kitendo kile ni sawa na mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya. Kwa hali ya kawaida mtu anaweza sema Watanzania haturidhiki na labda tunahiatji kuongozwa na Malaika la hasha! Hatuwezi kuzunguzia yale yasiyowezekena hata kidogo.

Sintosita kumpongeza Raisi kwa kubadilisha Mawaziri nafasi zao na kuwapandisha wengine ngazi, na kuwateua wengine wapya ila vile vile kwa kuwafukuza wale watuhumiwa wa mali za uma Kisiasa manake sitaki kushangaa kama kesho nitasikia wamepewa nafasi nyingine. Ila langu kubwa ni je hayo yaliyofanyika ndiyo tuseme Amen, kwamba Baraza hilo ndilo la kutuvusha mpaka 2015 ama tutarajie mengine mbeleni??

Kimsingi wakati mwingine napata taabu kufahamu haya wayasababishayo Mawaziri ama iwe ni kutokana na watendaji wao wa chini ama ni kwa namna nyingine yeyote ile iwayo je tatizo kubwa huwa ni nini?? Naamini kabisa Mhe. Rais anaweza akaendelea na zoezi hili la kuhamisha Mawaziri Wizara mpaka mwisho wa dahari. Tatizo lililopo si wao tu bali mtu wa kuwakemea na kuwawajibisha pale inapobidi na kwa muda unaostahili. Sioni mantiki ya kulipaka Kaburi chokaa ilihali ndani ni mifupa imejaa.

Binafsi bado naamini "usukwaji" huu kama ulivyopata kuitwa unahitaji hierachy nzima iangalie Nchi ilipofikia na mahitaji ya Wananchi kwa ujumla. Ni kweli kwamba si Rais wala Waziri Mkuu wote wamechoka tena jana nilipomwona Mr. President kwa kweli kama si Nchi basi ni hao viongozi wanaopaswa kukusaidia ndio wanaokuchosha so do Pinda.

Bado Rais anahitaji kupata mtu mwenye uwezo wa kuwaambia hao Mawaziri waliobadilishwa "hili hapana" tena kwa kuwakemea ila kama mtaendela kusema "nadhani" hali itakuwa ile ile Old wine in a New Bottle.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki JF

MEITINYIKU L. Robinson
 
Kwanza Naanza kwa kumsaport,JK kwa huu uteuzi uliojaa BUSARA na HEKIMA. Pili,Kwa wale wafuatiliaji wazuri wa SIASA za TANZANIA na SHINYANGA mjini,hawatakuwa wameshangaa sana kwa huu uteuzi,zaidi ya KUSIFU.
MASELLE,ni NANI??Kwa wale tunaomfahamu tangu akiwa pale UDSM,tunamjua vyema..ni MCHAPAKAZI,HODARI,JASIRI na M-HEKIMA..katika maamuzi na vitendo vyake. Vitendo vyake vianaonekana katika muda mfupi aliokaa shy TOWN..ni kama miaka kumi. MAENDELEO yameonekana..na watu wameyasifu. PONGEZI KWAKO MASELLE...vijana tumuunge MKONO.
 
1. Mh.Maghufuli wizara ya Nishati na Madini

2. Mh. Mwakyembe wizara ya Ujenzi

3. Mh. Kagasheki wizara ya Uchukuzi

4. Mh.Simbachawene Afrika Mashariki

5. Mh. Pinda angerudishwa TAMISEMI

6. Mh. Sitta waziri Mkuu



Hebu mwanaJF nawe toa maoni yako namna ambavyo ungewapanga hawa na wengine katika baraza la mawaziri.
 
Back
Top Bottom