Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

Mwanri anaendelea na wadhifa wake kama Naibu waziri TAMISEMI. Ila kwa sasa atakuwa chini ya Hawa Ghasia! (Mwanri chini ya Hawa Ghasia) kweli dunia imejaa vituko!

Ghasia anapwaya kila mahali lakini bado anabebwa tu,
Possibly jamaa anapiga hapa
 
Mwanzisha uzi lazima atakuwa ameathirika na bange za Mererani. Great Sinker indeed!
 
Namshauri Zito asiendele kujishikamanisha na hawa wanafiki akina Kigwangala na Makamba watu walimwambia aache kukaribiana nao yeye akadai hao ni wapiganaji walioweka maslahi ya vijana na taifa mbele lakini ndiyo wa kwanza kuisariti na pia kuipinga hoja yake ambayo ingeleta ukombozi halisi

Ninyi mnaofikiria kuwa Kigwangala anaweza kuwa Waziri nadhani hamjaweza kupata nafasi ya kumfahamu. Huyu bwana hana sifa hata ya kuwa diwani, hana busara wala uzalendo, amejengwa na unafiki na uwongo. January naye hana uzalendo hata kidogo, nadhani wengine mtakuwa mliiona ile email ya dada yake iliyokuwa ikimwombea hela kutoka kampuni ya madini impe dola milioni 2 ili afanyie kampeni ya ubunge kwa vile yeye ndiye atakuwa waziri wa madini na nishati. Ndiyo maana Zito anapokuwa na urafiki wa karibu na hawa Bwana, huwa tunapata maswali mengi sana maana haiwezekani Zito asiwe anawafahamu wanafiki na wapenda madaraka hawa.
 
Nafikiri kikubwa cha kusikitisha hapa ni kwa kutokupewa wizara kamili na kuwekwa chini ya mhe. huyu......... kazi ipo
 
Jk anazidi kuvunja record tena kama hili nililosoma hapa jf ni kweli. Sikusikiliza hilo baraza lake la mawaziri ila ninasoma hapa kuwa kuna waziri asiyekuwa na wizara maalamu ambaye ni mgonjwa mwandosya. Hii ni record mpya. JK na imani yake ya siasa za kuoneana huruma na kufarijiana ndio zimemfikisha hapa leo na kulipelekea taifa kuwa bovu kiasi hiki.

Mie nina amini suluhishi la matatizo ya watanzania ni kupata rais bora na si bora rais ambavyo kwa sasa invyoonekana.

Siasa zake hizo ndizo zimepelekea ufisadi kila kukicha na upungufu mkubwa wa maadili kwa watanzania ambao haujawahi kuonekana toka uhuru. Na kama kweli kabadilika awafilisi hao mafisadi ambao ameona hawafai kuwa kwenye cabinet wakati yeye mwenyewe ndiye aliwateua mwanzo.

KILIO CHA WATANZANIA NATUMAI SIO KUBADILISHIWA BARAZA LA MAWAZIRI BALI NI KUONDOKEWA NA BORA RAIS NA KUPATA RAIS BORA.
 
kweli kavunja itabidi tumpeleke guinness world records anafaa kuwa nominated kwenye viongozi wasioeleweka..
 
Nipo serious bwana!naomba unijibu mana kuna wakati nikifikilia sana
kuhusu yeye huwa machozi yananitoka!
wanaachwa watu zaidi yake kiutendaji,kwa nini tunafanyiwa ivyo?kwa
maslai ya nani hsa jamani?inatia uchungu sana.
Mungu tusaidie.

Wewe tulia hiyo ni chakula ya wakubwa
 
wazuri sana wakukosoa mlio wengi hata kuratibu mambo yenu binafsi huwa hamuwezi,punguzeni siasa wa tz fanyeni kazi!

Kwani wewe hapa umefanya nini?Maisha yako ya kila siku yanatawaliwa na siasa na cha kuangalia hapa sio watu waache siasa,bali siasa SAFI ndio inatakiwa.Kama watu wanaona maovu wasikosoe?
 
Mkubwa unanichekesha!! Kaunda baraza ZURI KABISA!!.... La watu ambao WENGI HUWAJUI!!! Kama huwajui, uzuri wa hilo baraza umeujuaje?? Acha utorozobi!!!

utorozobi live maana kaongea hata asichokijua yeye
 
Hili ndilo baraza lililokuwa linasukwa kwa week mbili? Unampaje unaibu waziri wa nishati na madini Steven Masele na kumuacha geologist Dr Peter Kafumu? Na Mwandosya afya yake inaendeleaje maana naona yumo kwa mtindo wa kizamani wa wizara isiyokuwa na kazi maalum?

Ukweli hili baraza litaharakisha kifo cha CCM. Limejaa wapambe na marafiki! Ni watu wachache sana watakaofanya kazi. Kwa mbunge yoyote wa CCM anayetamani kurudi bungeni 2015 basi aanze kufanya tararibu zingine. Hakuna namna, CCM itapata shida.

Pia, naomba ufafanuzi. Dr Hussein Mwinyi ni mbunge toka Zanzibar, sasa anasimamiaje wizara ya Afya ambayo sio ya muungano?

hilo nalo swali kaka ila tuone utendaji kazi utakuwaje
 
January Makamba a.k.a mathread aligushi na kuiba mtihani wa Form 4 pale Galanos. Rungu la necta likamuangukia lakini leo hii anatuongozea science na teknolojia. Hii nchi usanii mtupu na ninaamini kuwa hili baraza ni mpango wa Mungu kuiua kabisa ccm

Mkuu hapo kwenye
red; tuhuma nzito sana hizo. Tafadhali hebu fafanua kidogo kwa faida ya wasomaji na taifa kwa ujumla.
 
Leo Kama Jana wacha Rwanda Isonge mbele.... Tutakapoamka tutakuwa nchi ya dunia ya nne
 
Hawezi fakigio la chuma,
Aanze na Epa na Uda.
Vyote ni taasisis za serikali.
 
Namkubali sana huyu Mwanry yani Hawa Ghasia hakwalifai hata kidogo kua waziri then Mwanry awe naibu,kwa kweli KJ ni kituko sijawahi kuona mie kwenye hii miongo yangu michache hapa duniani
 
Uzoefu unaonyesha kuwa tangu JK ashike madaraka hajawahi kufanya maamuzi magumu kwa hiari yake!
 
Back
Top Bottom