Kikwete afagia tena ndani ya saa 24, Zamu hii amemng'oa Profesa Yadon Kohi

Hii nchi yetu ya ajabu sana; juzi nimeona hata jezi za polisi zimewekwa nembo ya Celtel, sasa wewe umewahi kuona wapi duniani hii kama sio Tanzania tu? Nyie mliopo nje hebu tuambie inawezekana kweli uniform za jeshi zikawa na nembo ya kampuni ya biashara? Wapinzani wetu nao hamna kitu, jambo kama hawajaliona, nafikiri hata msemaji wa jeshi hawana!!

...Oh please dear God no!
 
Mzalendohalisi hata mimi ndio maana nilitaka kujua Research funding ya COSTECH. Maana mwanasayansi hata awe Genius vipi lakini usipompatia Research Facilities za maana na vitendea kazi vya kutosha haitosaidia kitu.
 
wapya23415treyzs2.jpg

Kipanya na Jakaya

Credit: Mjengwa blog
 
Serikali haijali utafiti, ndo maana hata COSTECH iko hoi. Kama haina bajeti ya kutosha huwezi kufanya chochote kwenye tasisi ya inayosimamia mambo ya sayansi na technolojia. Maendeleo ya sayansi huja kutokana na tafiti.Tafiti hazifanyiki bila pesa. Kwa wale mlio USA mnaweza kutupa ushahidi kwamba maendeleo ya USA pamoja na mambo mengine yanachangiwa na utafiti unaofanywa na vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za huko kama NSF. Kwa mfano, NGA, USA army wana invest sana kwenye utafiti kwa kutoa pesa za uhakika kwa vyuo vikuu na hasa kwa wanafunzi wa PhD na matokeo ya tafiti huwekwa katika vitendo. Sio hapa TZ ambapo tafiti zinawekwa tu kwenye Biblioteca, na makabatini.

Anyway, kukaa kwa Profesa Kohi muda mrefu pia ni tatizo ukiongeza na mambo ya bajeti.Taasisi kama NIMR inapata mapesa kibao ya utafiti kutoka kwa wadhili kama vile Bill gates kwenye mradi wa Malaria na taasisi nyingine zinazoshirikiana na NIMR kwa mambo ya utafi. Kwa hiyo sishangai NIMR is doing better than COSTECH.

Tatizo ni serikali yenyewe haitengi fedha za kutosha kwa ajili ya utafiti au kwenye taasisi zake za elimu ya juu kwa ajili ya utafiti. Naamini hata UDSM hawapati fungu ambalo ni maalumu kwa utafiti kutoka serikalini.

Nchi hii wanasiasa ndo wanatengewa mapesa ya kumwaga, kwa hiyo kipaumbele mara zote ni wanasiasa kwanza.
 
Halafu hivi hatuna Philanthropists wa kibongo kuchangia kwenye Tafiti mbalimbali za kisayansi?? Kama Bill & Melinda Gates Foundation au John D. and Catherine T. MacArthur Foundation.

Maana kila siku matajiri wetu na makampuni mbalimbali yanaongoza kuchangia mamilioni ya pesa kwenye Miss Tanzania Pageant, Soccer, na mashindano mbalimbali ya kucheza ndombolo ya kina Jobiso.
 
Halafu hivi hatuna Philanthropists wa kibongo kuchangia kwenye Tafiti mbalimbali za kisayansi?? Kama Bill & Melinda Gates Foundation au John D. and Catherine T. MacArthur Foundation.

Maana kila siku matajiri wetu na makampuni mbalimbalia yanaongoza kuchangia mamilioni ya pesa kwenye Miss Tanzania Pageant, Soccer, na mashindano mbalimbali ya kucheza ndombolo ya kina Jobiso.

Mkuu unajua tatizo letu hatujajua hata vipaumbele vyetu ni vipi.....na hawa 'matajiri' wanalenga sehemu ambazo zina tambulika kirahisi kwa uma ili wafikie malengo yao...sasa wakifund tafiti nadhani kwa level yetu ni wananchi wachache watakaovutiwa!
 
Taasisi kama NIMR inapata mapesa kibao ya utafiti kutoka kwa wadhili kama vile Bill gates kwenye mradi wa Malaria na taasisi nyingine zinazoshirikiana na NIMR kwa mambo ya utafi. Kwa hiyo sishangai NIMR is doing better than COSTECH.

Hii taasisi inaongozwa na kichwa makini sana Dr. Mwele Malecela, ambaye ameweza kuwa-convince Billl na Melinda, kwamba anaweza kufanya utafiti wa kweli, na pia ni mumainifu wa mapesa yao wanayompa, sasa haya ni matatizo makubwa yanayotusumbua kwenye utafiti bongo, mana htuaminiki na mara nyingi uwezo hatuna wa kisayansi kuweza kufanya utafiti,

Dr. Mwele, ambaye pia ni rais wa dunia wa utafiti wake, pia hufundisha special classes huko US na Europe, kuhusiana na utafiti wake, ndio mana hata kule Atlanta CDC, waliamua kumpa access ya anything kuhuisiana na shughuli zake za kisayansi, na pia mara nyingi kuna watu babu kubwa kama kina Andrew Young na Jesse Jackson ambao humsaidia ku-lobby kwa serikali ya US kuhusiana na shughuli zake, lakini cha msingi ni uwezo wa utafiti na uaminifu, na pia dedication kwa hiyo shughuli maana huyu mkali sometimes huenda kuishi Songea maporini huko mwisho wa dunia kufuatilia mbu, sasa hawa makanali wa jeshi wataweza vipi hayo? ndio maan tunashindwa!

huko NIMR, Dr. Mwele amepigwa majungu weee, fitina weee, mpaka kutumiwa majambazi, lakini haikusaidia kitu.

Mungu Aibariki Bongo Yetu!
 
Halafu hivi hatuna Philanthropists wa kibongo kuchangia kwenye Tafiti mbalimbali za kisayansi?? Kama Bill & Melinda Gates Foundation au John D. and Catherine T. MacArthur Foundation.

Maana kila siku watu wanachangia mamilioni ya pesa kwenye Miss Tanzania Pageant, Soccer, na mashindano mbalimbali ya kucheza ndombolo ya kina Jobiso.

GQ,
Ndio maana tuna safari ndefu. Matajiri wetu bado hawaja gundua njia mbalimbali zakuchangia kwenye jamii. Ukweli ni kwamba kutoa mchango kwenye kuendeleza tafiti za kisayansi ni mmoja ya njia muhimu ya ku give-back-to-the-community. Leo hii biotechnology is taking over the World, kuanzia madawa mpaka vyakula. Bongo watu wameshaanza kubeza organic food, kila mtu anataka kuku mnene bila ya kujua kwamba ameumuliwa kwa madawa. Sasa agencies kama COSTECH ndio ambao wangeweza kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa organic food and the like. Lakini kwa sababu funds za research hazitoshi, ndio hivyo tena inakuwa mzozo. Unafikiri kwa nini obisity imeanza kuingia africa?
 
Mfano hapa US wana National Science Foundation (NSF) ambayo iko funded heavily na US Federal Govt na pia watu binafsi na taasisi nyingine mbalimbali nao huchangia. Hii Taasisi imeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kisayansi na teknolojia hapa US. Wao wana-fund kuanzia High School, Undergrads level, Grad level, PhDs na mpaka private individuals. Actually nawashukuru sana kwani mimi pia nilishakuwa mmoja wa recepients wa grants za NSF.

Lakini nchini kwetu nadhani kama wengi mnavyosema Scientific Researches sio priority, wanasiasa wetu wako tayari kutumia mabilioni ya shilingi kwenye longolongo za kisiasa lakini wanatoa pesa kiduchu kwenye mambo yatakaloliletea Taifa manuafaa makubwa sana.
 
Taasisi kama NIMR inapata mapesa kibao ya utafiti kutoka kwa wadhili kama vile Bill gates kwenye mradi wa Malaria na taasisi nyingine zinazoshirikiana na NIMR kwa mambo ya utafi. Kwa hiyo sishangai NIMR is doing better than COSTECH.

Hii taasisi inaongozwa na kichwa makini sana Dr. Mwele Malecela, ambaye ameweza kuwa-convince Billl na Melinda, kwamba anaweza kufanya utafiti wa kweli, na pia ni mumainifu wa mapesa yao wanayompa, sasa haya ni matatizo makubwa yanayotusumbua kwenye utafiti bongo, mana htuaminiki na mara nyingi uwezo hatuna wa kisayansi kuweza kufanya utafiti,

Dr. Mwele, ambaye pia ni rais wa dunia wa utafiti wake, pia hufundisha special classes huko US na Europe, kuhusiana na utafiti wake, ndio mana hata kule Atlanta CDC, waliamua kumpa access ya anything kuhuisiana na shughuli zake za kisayansi, na pia mara nyingi kuna watu babu kubwa kama kina Andrew Young na Jesse Jackson ambao humsaidia ku-lobby kwa serikali ya US kuhusiana na shughuli zake, lakini cha msingi ni uwezo wa utafiti na uaminifu, na pia dedication kwa hiyo shughuli maana huyu mkali sometimes huenda kuishi Songea maporini huko mwisho wa dunia kufuatilia mbu, sasa hawa makanali wa jeshi wataweza vipi hayo? ndio maan tunashindwa!
huko NIMR, Dr. Mwele amepigwa majungu weee, fitina weee, mpaka kutumiwa majambazi, lakini haikusaidia kitu.

Mungu Aibariki Bongo Yetu!

Mkuu FMES, heshima mbele mkuu, on a light note, nilidhani makanali ni watu wa vita na wamezoea mazingira magumu ya maporini? LOL
 
Maana kila siku matajiri wetu na makampuni mbalimbali yanaongoza kuchangia mamilioni ya pesa kwenye Miss Tanzania pageant,Soccer,na mashindano mbalimbali ya kucheza ndombolo ya kina Jobiso.

Inabidi na nyie akina kaka/baba mpunguze kuangalia soccer, labda matajiri wata-diverge attention!
 
on a light note, nilidhani makanali ni watu wa vita na wamezoea mazingira magumu ya maporini? LOL

Mkuu heshima ikurudie, after 14 years ya uongozi uraiani? Mkuuu tulipitia JKT kwa hiyo we have an idea kidogo, huyu mkuu alipaswa tu kustaafishwa maaana hana jeshi tena akilini mwake, na itakuwa vigumu sana at this stage kumrudisha jeshini tena, kwa lugha za kijeshi anaitwa raia huyu!
 
Mkuu ndo kusema kuwa hapo 'kurudishwa jeshini' inaweza kuwa na maana zaidi ya moja? manake nadhani hapa changa la macho wanalotaka kututupia ni ile dhana kuwa mjeshi ni mjeshi tu huwa hastaafu...kwa hiyo kusema kuwa 'amerejeshwa jeshini' mi naona kama njia ya kusave his face....ama?
 
Inabidi na nyie akina kaka/baba mpunguze kuangalia soccer, labda matajiri wata-diverge attention!

siku hizi na kina mama wameanza kuwajua kina Ronaldinho na Beckham...kazi kweli mi huwa siangalii mpira peke yangu..

On the other hand mi nina wasi wasi na hii inaitwa 'gender' movement inayoangalia upande mmoja tu wa gender-sex tena basi females tu wenyewe wanaita women/female emancipation sijui.. kwa maoni yangu hili halipaswi kufanyika kwa kuwatoa kafara wanaume...wawezeshwe kusoma na kufikia malengo sawa sawa na wanaume, wapmbe kazi sawa na wanaume na uchaguzi usiangalie huyu ni mwanamke au la...
 
"Simba wa kuchorwa huyo"

SteveD.

Huyu cheka cheka (jina alilopewa na Dada AA) fagio lake halijafagia chochote ili kuzigusa nyoyo za Watanzania. Naona anataka kuleta usanii kama unaofanywa na TAKUKURU wa kuwaibua dagaa wadogo wadogo wala rushwa wakati mapapa wanaendelea kufanya vitu vyao.
 
siku hizi na kina mama wameanza kuwajua kina Ronaldinho na Beckham...kazi kweli mi huwa siangalii mpira peke yangu..

On the other hand mi nina wasi wasi na hii inaitwa 'gender' movement inayoangalia upande mmoja tu wa gender-sex tena basi females tu wenyewe wanaita women/female emancipation sijui.. kwa maoni yangu hili halipaswi kufanyika kwa kuwatoa kafara wanaume...wawezeshwe kusoma na kufikia malengo sawa sawa na wanaume, wapmbe kazi sawa na wanaume na uchaguzi usiangalie huyu ni mwanamke au la...

Nakulilia
Nani amesema mama/dada zetu hawawezi kupenyeza kwenye mfumo dume? 4 of the top 5 directors wa COSTECH walikuwa wanaume. HKwa hiyo uteuzi wa mama Kingamkono ni moja ya ushahidi tosha kwamba wapo wakina mama wakali zaidi kwenye system yetu.

Staff.htm
 
Mzalendohalisi:
Hebu tufafanulie hiyo 'MUHAS' ni kitu gani.
Where did you go and got so much impressed to think that you were in the US, MUHAS or NIMR? What do you mean by infrastructure - equipment or what?

I would venture to state that National Institute of Medical Research is heavily funded from external sources, while COTECH is purely dependent on government subventions. And as we all know the vigogo's who decide have little regard for scientific research. That is a fact of our Tanzanian situation.
 
Taasisi kama NIMR inapata mapesa kibao ya utafiti kutoka kwa wadhili kama vile Bill gates kwenye mradi wa Malaria na taasisi nyingine zinazoshirikiana na NIMR kwa mambo ya utafi. Kwa hiyo sishangai NIMR is doing better than COSTECH.

Hii taasisi inaongozwa na kichwa makini sana Dr. Mwele Malecela, ambaye ameweza kuwa-convince Billl na Melinda, kwamba anaweza kufanya utafiti wa kweli, na pia ni mumainifu wa mapesa yao wanayompa, sasa haya ni matatizo makubwa yanayotusumbua kwenye utafiti bongo, mana htuaminiki na mara nyingi uwezo hatuna wa kisayansi kuweza kufanya utafiti,

Dr. Mwele, ambaye pia ni rais wa dunia wa utafiti wake, pia hufundisha special classes huko US na Europe, kuhusiana na utafiti wake, ndio mana hata kule Atlanta CDC, waliamua kumpa access ya anything kuhuisiana na shughuli zake za kisayansi, na pia mara nyingi kuna watu babu kubwa kama kina Andrew Young na Jesse Jackson ambao humsaidia ku-lobby kwa serikali ya US kuhusiana na shughuli zake, lakini cha msingi ni uwezo wa utafiti na uaminifu, na pia dedication kwa hiyo shughuli maana huyu mkali sometimes huenda kuishi Songea maporini huko mwisho wa dunia kufuatilia mbu, sasa hawa makanali wa jeshi wataweza vipi hayo? ndio maan tunashindwa!

huko NIMR, Dr. Mwele amepigwa majungu weee, fitina weee, mpaka kutumiwa majambazi, lakini haikusaidia kitu.

Mungu Aibariki Bongo Yetu!

No No; tusivungane hapa. Huo sio ukweli. Hiyo taasisi haiongozwi na huyo uliyemtaja. Hii haishughuliki na matende peke yake.
 
Hata hivyo taasisi zote za utafiti huku USA zinakuwa funded kutegemeana na utendaji wa wakurugenzi wake. Angalia mashirika kama REPOA, NIMR LHRC na hata Hakielimu yana fedha lukuki kutokana na utendaji wao. Hii COSTECH haiwezi kuwa na hela kama utendaji wake ndio huo tulioambiwa wa vikao na makongamano tu na kutumia magari ya shirika kwendea sokoni. Subirini muone mabadiliko atakayokuja nayo huyu mama.
 
Kwa pande wa Profesa Kohi, kwa muda wa miaka 14 aliyoingoza COSTECH tangu mwaka 1993,

Jamani jamani mweeeh! Yaaani kwenye sekta ya bureaucratic kuna mtu alikuwa bosi kwa miaka 14 in a roll? Tena shirika la serikali sio kwamba ni lake au anamiliki majority share?

Hivi ni kitu gani kitatu badilisha taifa hili uwezo wetu wa kufikiri na kuangalia ishu muhimu za taifa hili?

I mean I am lost!, 14 years, dude alikuwa bosi wa shirika moja la umma?

Mkuu ndio maana wanajisahau maana mtu anakaa kwenye nafasi yake hadi anafanana na hiyo ofisi. Huu ni ujinga sana inamaana kuwa kwa miaka yote hiyo serikali haikuwahi kujua kuwa hilo shirika halifanyi kitu? Unajua mfano kama Mgonja yeye aliazimwa benk kuu kwenda hazina mkataba wake naye ulishaisha siku nyingi ila sasa bado yupo tuu inamaana hamna watu wengine wanaoweza kuongoza bila wao?
 
Back
Top Bottom