Kikwete afagia tena ndani ya saa 24, Zamu hii amemng'oa Profesa Yadon Kohi

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
::>Amporomosha mkurugenzi mzito
::>Amrejesha jeshini, hofu yatawala

na mwandishi wetu

FAGIO la Rais Jakaya Kikwete, limefanya kazi tena katika muda usiozidi saa 24.

Zamu hii ameamua kumng’oa Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Technolojia (COSTECH), Profesa Yadon Kohi.

Profesa Kohi ambaye ni Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), jana alitaarifiwa rasmi kuwa, uteuzi wake umetenguliwa, na anapaswa kurejea jeshini.

Hatua hii ya Rais iliilazimu Bodi ya Wakurugenzi kukaa kwa dharura Dar es Salaam jana, na kumteua Dk. Rose Kingamkono, kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH. Dk. Rose alikuwa Mkurugenzi wa Utafiti kabla ya uteuzi huo.

Habari za nafasi ya Profesa Kohi kutenguliwa, zilianza kusambaa juzi jioni, lakini hakukuwapo chombo chochote huru cha kuzithibitisha, hadi jana, ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya COSTECH, Profesa Burton Mwamila, alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo fupi iliyokuwa na misitari mitano, ikiwa imeandikwa kwa Kiingereza, ilisomeka: “Tunapenda kuifahamisha jamii kuwa Dk. Rose Rita Kingamkono, ameteuliwa na Bodi ya COSTECH kama Kaimu Mkurugenzi kuanzia Desemba 7, 2007.

“Hii inatokana na uamuzi wa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kwamba Profesa Brigedia Jenerali Yodan Mtalima Kohi, arudi katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).”

Juzi Rais Kikwete alipangua safu ya wakurugenzi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, na kuteua wapya kushika nyadhifa hizo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema, mabadiliko hayo yalilenga kuleta ufanisi.

“Lengo la mabadiliko haya ni kuleta ufanisi katika utendaji wa idara zilizo chini ya wizara. Tulichelewa kufanya mabadiliko, kwa sababu umakini wa hali ya juu ulihitajika,” alisema Profesa Maghembe.

Katika mabadiliko hayo, Erasmus Tarimo, ambaye awali alikuwa Ofisa Wanyamapori Mkuu, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, kuchukua nafasi ya Emmanuel Severre, ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Severre, aliyekuwa akituhumiwa kwa kashfa nyingi, na akidaiwa kutamba kuwa yeye ni kisiki cha mpingo kwa hali yoyote asingeondolewa katika wizara hiyo.Mwaka jana, Waziri wa Mifugo, Anthony Diallo, alipoteuliwa kushika Wizara ya Maliasili na Utalii, Severre alikaririwa akitamba kuwa juhudi za kumng’oa alizokuwa ameanzisha Diallo zisingefua dafu. Na kweli Diallo aling’olewa na kumuacha Severre.

Kwa pande wa Profesa Kohi, kwa muda wa miaka 14 aliyoingoza COSTECH tangu mwaka 1993, ameelezwa kuwa ameshindwa kuifanya tume hiyo kutimiza malengo yake.

Inadaiwa kuwa alikuwa na safari nyingi za nje, huku uongozi wa tume hiyo uliokuwa chini yake, ukiwa unaingia mikataba na kampuni za simu kuvuna fedha kwa bei nafuu, hali iliyosababisha majengo ya COSTECH kupigwa rangi za kampuni moja ya simu. Baadaye rangi hizo zilifutwa.

Pia zipo tuhuma kuwa, magari ya COSTECH yalikuwa yakitumiwa na uongozi wa juu chini ya uongozi wa Profesa Kohi kwenda kuwindia wanyama pori, hali iliyomkera Rais Kikwete.

“Sayansi imedumaa nchini. Chini ya uongozi wake imekuwa ni semina, mikutano, safari, basi… hakuna utafiti unaofanywa, hatafuti fedha kwa ajili ya tume, kila kitu kinakwenda tu,” kilisema chanzo chetu.Mabadiliko yanayotokea sasa, yanadhihirisha kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa hivi karibuni katika Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM, mjini Dodoma, aliposema atahakikisha anasafisha uoza serikalini.Kwa kuonyesha kuwa amedhamiria kutenda anenayo, hivi karibuni ameunda kamati mbili za kuchunguza masuala mazito, likiwamo la kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond, na ile ya kuchunguza na kupitia sera na mikataba ya madini.

Matukio hayo mawili, yametengeneza hofu kubwa na kusababisha kihoro kutawala miongoni mwa watendaji wa Serikali. Hii ilithibitika wakati mkurugeni mmoja alipopigiwa simu kutoa maoni yake jana: “Sina la kuzungumza. We niache tu, huwezi kujua labda kesho ni mimi. Ngoja tuone kwanza mzunguko unakwendaje.”

Source: Mtanzania newspaper
 
Sasa Sayansi itaendelea vipi wakati hakuna pesa za Kufanya Research. Ningependa kujua bajeti ya COSTECH na Taasisi ya Taifa ya Utafiki wa Kisayansi.
 
Danganya toto hiyo, aanze na mawaziri wanao/waliohujumu Uchumi kwa kuwafukuza na kuwafungulia mashtaka, kinyume na hapo anaendelea kutupaka Watz mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kutoa kafara "Dagaa" badala ya "Samaki"
 
1. Nadhani Hawa Wakurungenzi walikaa mda mrefu mno (14 years) wakajisahau. It is better to have Performance Assessment in every 5 years kama Mkurugenzi hana jipya alilodeliver- then wabadilishwe! Hii ya kusubiri 14 years is too late!

2. Jengo ya COSTECH Vodacom walilipiga rangi- sii heshima kwa nchi yetu. Ni jukumu la serikali kupiga rangi na kukarabati majengo yake.

3. Dr. Kingamkono huyu mama sii alikuwepo Chakula na Lishe- wakampiga vita ndo akaenda COSTECH? Ni mama makini anavyoonekana!

4. JK nafikiri sasa ameamua, tusubiri huenda tukaona mengi!
 
mmewahi kusikia revolving door? kama kweli si awatimue tu hata wale wa maliasili wataenda kuibukia kwingine; msishangae Severe akapangiwa deski kwenye ofisi ya Waziri Mkuu au Makamu wa Rais.. au hata Ikulu kwenyewe.. msifanye mchezo
 
Mugo"The Great";108074 said:
Danganya toto hiyo, aanze na mawaziri wanao/waliohujumu Uchumi kwa kuwafukuza na kuwafungulia mashtaka, kinyume na hapo anaendelea kutupaka Watz mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kutoa kafara "Dagaa" badala ya "Samaki"

Precisely! Aanze na big players, hawa samaki ndogondogo zitajirekebisha wakiona wakuu wao wanavyoshughulikiwa kikamilifu! Hii approach, always works!
 
subirini wiki ijayo... ! especially ile wiki aidha ya Krismasi au mara baada ya mwaka mpya.. labda atafanya kweli. Ila msishangae watu wakianza kujiuzulu wenyewe kabla ya panga kuwafikia. Next week mtu asipojiuzulu..
 
Hii nchi yetu ya ajabu sana; juzi nimeona hata jezi za polisi zimewekwa nembo ya Celtel, sasa wewe umewahi kuona wapi duniani hii kama sio Tanzania tu? Nyie mliopo nje hebu tuambie inawezekana kweli uniform za jeshi zikawa na nembo ya kampuni ya biashara? Wapinzani wetu nao hamna kitu, jambo kama hawajaliona, nafikiri hata msemaji wa jeshi hawana!!
 
pia si shangai na haya mabadiliko maana hawa wagonjwa (viongozi)wameugua kwa muda mrefu kwa hiyo hata wakifa (kutolewa)hakuna wa kulia wala kuuzunika
 
subirini wiki ijayo... ! especially ile wiki aidha ya Krismasi au mara baada ya mwaka mpya.. labda atafanya kweli. Ila msishangae watu wakianza kujiuzulu wenyewe kabla ya panga kuwafikia. Next week mtu asipojiuzulu..

Mmeshaanza tena mambo ya sheikh Yahaya!
 
LAkini all in all, walao ameonyesha kuwa anaweza kufanya kitu na ni clear signal kwa walio juu zaidi kuwa chochote kinaweza kutokea
 
yeah, unajua upande mmoja tunashukuru, binafsi mpaka pale watakapoanza kuachia ngazi na siyo kuzungushwa toka upande mmoja kwenda upande mwingine..
 
Ila huyu Kohi ngoja apigwe chini, alikuwa amezidi shangingi la COSTECH kampa mkewe ndo lilikuwa gari la shamba, na mkewe yaani afadhali mama ANBEM, sema ni katika nyanja tofauti!

Yaani hadi wafanyakazi huwa anawashambulia kwa mateke na magumi! ambalo sijui naye ni njagu? make ule ubabe mmhh!!
 
Kwa pande wa Profesa Kohi, kwa muda wa miaka 14 aliyoingoza COSTECH tangu mwaka 1993,

Jamani jamani mweeeh! Yaaani kwenye sekta ya bureaucratic kuna mtu alikuwa bosi kwa miaka 14 in a roll? Tena shirika la serikali sio kwamba ni lake au anamiliki majority share?

Hivi ni kitu gani kitatu badilisha taifa hili uwezo wetu wa kufikiri na kuangalia ishu muhimu za taifa hili?

I mean I am lost!, 14 years, dude alikuwa bosi wa shirika moja la umma?
 
Hii nchi yetu ya ajabu sana; juzi nimeona hata jezi za polisi zimewekwa nembo ya Celtel, sasa wewe umewahi kuona wapi duniani hii kama sio Tanzania tu? Nyie mliopo nje hebu tuambie inawezekana kweli uniform za jeshi zikawa na nembo ya kampuni ya biashara? Wapinzani wetu nao hamna kitu, jambo kama hawajaliona, nafikiri hata msemaji wa jeshi hawana!!

What!

OMG, polisi wamevaa jezi zina nembo ya Celtel!

Only in Tanzania and some lost (and going to hell) countries
 
Kwa pande wa Profesa Kohi, kwa muda wa miaka 14 aliyoingoza COSTECH tangu mwaka 1993,

Jamani jamani mweeeh! Yaaani kwenye sekta ya bureaucratic kuna mtu alikuwa bosi kwa miaka 14 in a roll? Tena shirika la serikali sio kwamba ni lake au anamiliki majority share?

Hivi ni kitu gani kitatu badilisha taifa hili uwezo wetu wa kufikiri na kuangalia ishu muhimu za taifa hili?

I mean I am lost!, 14 years, dude alikuwa bosi wa shirika la umma?

Huyu hata jeshi kasahau, kule jeshini anaenda kusoma gazeti. Si afadhali angemwambia astaafu tu maana sasa ataendelea kututia hasara bure.
 
Dr. Kingamkono huyu mama sii alikuwepo Chakula na Lishe- wakampiga vita ndo akaenda COSTECH? Ni mama makini anavyoonekana!

You are right Mzalendohalisi. Ni kweli Dr. Rose kingamkono alishawahi kuwa Shilika la Chakula na Lishe (TFNC). Huyu mama ni mmoja wa underrated highly educated Tanzanians wanaotoa michango mikubwa katika taifa letu.

Hebu ngoja nizame kwenye bibliolateca (maktaba) yangu ili niwaletee her complete resume/CV yake.
 
1. Huyu Kohi ni mzima sana kichwani-(daktari wa binadamu, Brigedia wa jeshi, Profesa, na majuzi tu alipata degree ya sheria) he is a very intelligent person- sijui kwa nini leadership ilimshinda- may be he was starved of resources!

2. Nchi zingine Institutions kama COSTECH ndo kioo cha nchi ktk Inventions and Innovations- na hupata fungu tosha toka serikalini. Katika nchi zingine such councils provide funding for research to other institutions, NGOs etc. Sijui budget ya COSTECH- but if they were starved of resources- je angetafuta ufadhili? COTECH have so large mandate kisheria ila hawana pesa!

3. Kama JK amemwondoa- correspondingly- aongeze pesa za utafiti, naona aibu sana hata mgeni akija Tz akakuta jengo la COSTECH limepigwa rangi ya VODACOM- sidhani kama wanapewa pasa za kutosha hadi kuruhusu hali kama hii!

4. Sehemu zingine za Utafiti kama UD, MUHAS, NIMR(have world class research environment- I went there recently near Ocean Rd-I thought I was in the US!), have so good infrastructure- sasa kwa nini COSTECH wawe staved hadi VODACOM waje wapige rangi? Nenda hapo Kenya au Rwanda- mazingira yao are far better- yet COSTECH ndo anatakiwa atoe dira kwa hao wote- je itawezekana?

What is the main problem? Is this a Kohi factor- or more than that?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom