MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,588
Ongea na Mtikila nasikia anajipanga kwenda mahakamani kudai mahakama imuombe kupumzika hawezi kuendelea na madaraka kwa sababu ya ugonjwa.
na mimi nililiona hili. jf inamuumiza kichwa sana huyu mzee.
mwaka huu ataona cha mtema kuni.
halafu mzimu wa wafanya kazi unamuandama sana. mara baada ya kuinuka na kurudi jukwaani hiyo juzi kubwa lilikwa ni wafanya kazi
jana mwanza akalieleza kwa kirefu anaona aibu kusema mdomo umemponza
hahahaha, katu simpi kura hata ajiangushe mara mia na kuzimia kwa masaa 24 simwonei huruma huyu, kura yangu ina nguvu!
Mkuu Masa, mbona hii picha inaonesha kama vile jamaa kapandisha kenchi? Si unakumbuka kale ka uongojwa ambako nyama zinavyozidi kupungua mabega yatengeneza inverted V inaoyoelekea kule ambako wanaoenda hawarudi?
Ha ha mkuu, ingekuwa wapiga kura wanaambilika tungempumzisha kiulaini, thorugh votes hapo october!! Tatizo ni kwamba, wazalendo wengi wenye kuelewa mambo hawapigi kura!! Je hali yake kiafya inaweza kutumiwa kama kigezo na kitumike kwenye kampeni za wapinzani? Naamini ingekuwa ni mgombea wa upinzani ameangauka basi ssm wangetumia hicho kama kigezo!! Au vipi wakuu??
Jamaa ana wake wangapi vile? Na anadunda kama kawaida. Sijui kama Bilal na boss wake wanaweza KUNYAKUA hata futi moja ........
Yaani nchi masikini hata Rais wake anakuwa hoi? CCM, we deserve better jamani.
Mkuu acha tu! Hahahahahaha
Hebu check hapa anacheza kiduku
Du! Naanza kuamini kwamba Jangwani kuna nguvu ya Upako wa Mungu. Atokaye kwa kina Sangoma S/wanga, B/moyo, Tanga na Pemba asitie mguu kamwe
Hakuna uchawi. Isipokuwa JK anapenda kusafiri mno. ndiyo maana anachoka. Rest & Restoration ni mojawapo ya vitu vinavyopima mafanikio ya mtu. Kwa hili JK hajafanikiwa kwa afya yake. Anafikiri ujiko kuzururazurura. Hata ziara zinazo hitaji wakuu wa wilaya tu, yeye yumo!!!!!!!
Tukiacha ushabiki ni kweli daktari wa Rais wetu anastahili kuwajibika kama si kuwajibishwa. Mambo yote yaliyosemwa kama ni funga, sukari, uchovu n.k daktari angepaswa kuyajua na tahadhari zote za kidaktari zikachukuliwa siyo kuacha Rais wetu akaadhirika.