GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Jana kule Mwanza Kirumba alitaka kuendelea kuhutubia lakini wasaidizi wake wakamwambia muda umekwisha " Naambiwa muda umekwisha" alisema! Muda umekwisha? There is more than meets the eye on our President's state of health.
 
Mara kwa kwanza wakatuambia Usongo wa Mawazo
Mara ya pili wakatuambia Uchovu
Mara ya tatu Sukari imezidi ---- mmhh kazi ipo, tuambieni ukweli tu tujue.


Yamesemwa na daktari haya?:confused2:
 
Ina maana Kikwete karithi.

Kama ume "pruvu"anacho,basi karithi.Eti wenyewe wanasema baada ya kuona umati mkubwa vile,alichanganyikiwa na kupoteza fahamu sababu ya furaha. Lakini ukifuatilia ile hotuba yake utagundua kuwa jf ndo inamuumiza akili, pale alipoanza tu kuiponda eti inapoteza watu ndo, mara "CHALI"
 
Tukiacha ushabiki ni kweli daktari wa Rais wetu anastahili kuwajibika kama si kuwajibishwa. Mambo yote yaliyosemwa kama ni funga, sukari, uchovu n.k daktari angepaswa kuyajua na tahadhari zote za kidaktari zikachukuliwa siyo kuacha Rais wetu akaadhirika.
 
Ila usikose kupiga kura,PLEASE!

Najua kuwa kupiga kura ni mojawapo ya njia za kulelta mabadiliko lakini kwa hali ilivyo sio siri bado nashindana na roho yangu niende nisiende maana kusema kweli hali yangu inatia shaka. Na hali hii si kwa peke yangu ni watu wengi tu nimewasikia wamekata tamaa kuwa hata wakipiga kura, wasipige bado atashinda mtu ambaye wao hawadhani kama anawezakuwa kiongozi wao mzuri. Leo asubuhi imenibidi nijivike cheo cha mama Dr. Lwakatare ili kujaribu kumconvince dereva tax asiache kupiga kura baada ya kunijuza dhamira yake yeye juu ya kutokupiga kura. Inataka moyo.
 
kwani watanzania wangapi wanafunga na wanafanya kazi nzito na hawaanguki kama yeye.....
 
Hii inashangaza sana. Hebu sote tuwe makini na tujiulize maswali haya?

1. Huyu ni Rais wa nne Tanzania Bara, je wale watatu waliopita walianguka mara ngapi?
2. Kwani wao hawakuwa na kazi nzito kama yeye JK kwa sasa?
3. Awamu ya pili alikuwa ni his ex Mzee Mwinyi, na alikuwa ni moslem!! Je alianguka mara ngapi jukwaani au popote au hata kuzimia?
4. Huyu Rais wetu JK ameshaanguka mara nne public, na hatujui private ni mara ngapi?? Je hatujaweza kuona kuwa kuna hutilafu kubwa sana katika mwili wake na afya kwa ujumla?
5.Saumu ya masaa machache haiwezi kabisa kumwangusha mtu mwenye afya yake. Ninafahamu daku huliwa usiku, say kama hata amekula daku saa 2 mbili usiku, bado ana uwezo wa kushinda njaa kwa masaa mengi sana. Mbona wakristu wakifunga ni say kuanzia saa mbili usiku baada ya dinner na hakuna cha daku na bado hata hawasinzii ofisini? Tuwe tunajadili masuala kwa upana!! Afya ya huyu mheshimiwa ni zaidi ya ujuavyo!!
6. Ni kweli Dr. Slaa alianguka bafuni Mwanza na kuvunjika mkono, kumbuka kuwa mahoteli mengi yanatumia tiles za bafuni imara kiasi gani? Tena ukizingatia ni za China mara nyingi? Ile ilikuwa ni accident, hii ya JK si accident, ni madhaifu ya afya yake.

Watanzania wote, ni vema tufumbue macho na kuvaa kiona mbali kuhusu afya ya huyu mtukufu wetu!! Ifahamike kuwa ugonjwa hauombwi na kila mtu angefurahi kama asingeugua, ila basi unapoumwa ni vema ukaweka wazi, hata kama si details but tunajua kabisa huyu ndugu pengine ana low/High BP/Sugar and many other serious illiness!! Kulikoni kujitafutia visingizio lukuki, mara saumu kali, mara alisafiri mno hajapumzika ndiyo maana mwili umeishiwa nguvu, etc, etc. Hivi kweli kama unajua kuwa huna stamina ya kustahimili kazi nyingi ni kwa nini usi-delegate? (Hapa ni kwasafari zaidi).

Pole Rais, pole sana, weka wazi afya yako ilii tukuombee. Ugonjwa ni jambo la kawaida!!Hakuna atakayekunyang'anya hicho kitu eti kwa kuwa umeweka bayana afya yako. Mtasema pengine ugonjwa ni siri ya Dr. na Mgojwa, ni kweli ila magonjwa kama lilivyo general si siri, pengine details zake ndiyo siri. Kwani nini bwana!! Mimi nitasema tu, mbona hata wenye ukimwi wameamua kuvunja ukimya siku hizi na hawaogopi? Sembuse wewe mheshimiwa ambaye tatizo lako ni la kawaida si ukimwi??!!

Dr. wa Rais, tafadhali eleza report ya kiukweli, not propaganda!! Ugonjwa hauna propaganda!! Au ikiwezekana apumzike, bado ataendelea kupata maisha bora kama Rais mtaafu tu na aweze kuishi maisha marefu. Msimchoshe tafadhadhali. Mpeni ushauri wa ukweli.

Daktari wa Rais ana wajibu wa kuwaeleza watanzania juu ya afya ya rais wetu.
 
Huku kuanguka anguka ni 'events' au ni 'trend'? Nakumbuka kuna 'mtabiri' alidai hakuna uchaguzi mwaka huu!
 
Hapo bado hajaingia ikulu hhalafu ana kazi nyingi mpaka anaanguka.akishaingia je?
 
najua kuwa kupiga kura ni mojawapo ya njia za kulelta mabadiliko lakini kwa hali ilivyo sio siri bado nashindana na roho yangu niende nisiende maana kusema kweli hali yangu inatia shaka. Na hali hii si kwa peke yangu ni watu wengi tu nimewasikia wamekata tamaa kuwa hata wakipiga kura, wasipige bado atashinda mtu ambaye wao hawadhani kama anawezakuwa kiongozi wao mzuri. Leo asubuhi imenibidi nijivike cheo cha mama dr. Lwakatare ili kujaribu kumconvince dereva tax asiache kupiga kura baada ya kunijuza dhamira yake yeye juu ya kutokupiga kura. Inataka moyo.
usijali we piga tu halafu tuone. Uliwahi kusikia kuwa sisimizi kameza dafu?
 
Kama ume "pruvu"anacho,basi karithi.Eti wenyewe wanasema baada ya kuona umati mkubwa vile,alichanganyikiwa na kupoteza fahamu sababu ya furaha. Lakini ukifuatilia ile hotuba yake utagundua kuwa jf ndo inamuumiza akili, pale alipoanza tu kuiponda eti inapoteza watu ndo, mara "CHALI"

na mimi nililiona hili. jf inamuumiza kichwa sana huyu mzee.

mwaka huu ataona cha mtema kuni.
halafu mzimu wa wafanya kazi unamuandama sana. mara baada ya kuinuka na kurudi jukwaani hiyo juzi kubwa lilikwa ni wafanya kazi
jana mwanza akalieleza kwa kirefu anaona aibu kusema mdomo umemponza

hahahaha, katu simpi kura hata ajiangushe mara mia na kuzimia kwa masaa 24 simwonei huruma huyu, kura yangu ina nguvu!
 
narudia kusema kuwa hata ajiangushe mara mia
katu simpi kura yangu huyu, na wala sitamwonea huruma kwa kujiangusha angusha
 
Nimemsikia akisema "AISEE" na kisha akarudi maneno aliyokuwa ameshayasema ndo akala mweleka. Sijui aliposema aisee alikuwa ameona nini huyu mkuu wa kaya. Mambo ya Sheikh Yahaya maana aliwaambia mwaka huu hakuna uchaguzi wao wamempuuza "mshauri wao" wa mambo ya "ufundi". Inawezekana sheikh Yahaya amejitoa kwenye kamati ya ufundi baada ya "utabiri wake" kupuuzwa ndo maana haya yamempata mkulu. Hahahahaaaaa
 
Kudondoka mara 3 si jambo la mzaha, Nchi za wenzetu huu ni uthibitisho tosha - tunataka mtu mwenye afya 100% kutumikia wananchi kwa miaka 5 ijayo na si vinginevyo. Tunataka majibu ya kina hapa msizunguke mbuyu.
 
nimemsikia akisema "aisee" na kisha akarudi maneno aliyokuwa ameshayasema ndo akala mweleka. Sijui aliposema aisee alikuwa ameona nini huyu mkuu wa kaya. Mambo ya sheikh yahaya maana aliwaambia mwaka huu hakuna uchaguzi wao wamempuuza "mshauri wao" wa mambo ya "ufundi". Inawezekana sheikh yahaya amejitoa kwenye kamati ya ufundi baada ya "utabiri wake" kupuuzwa ndo maana haya yamempata mkulu. Hahahahaaaaa

"aisee....."
 
Back
Top Bottom