GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

huyu jamaa mgonjwa sana ila hawataki kusema ukweli hawa ccm

halafu tatizo jingine ni kuwa huyu jamaa ni mbishi sana haskilizi ushauri wa daktari wake.
 
hhhee wallah u have mad my day people khaaaa...........:lol::lol::lol::lol:
 
Kwa nini vyombo vya habari vya nje kama CNN, SKY NEWS, BBC, Aljazeera, ...., haviupi umuhimu uchaguzi mkuu wetu? Vyombo vyetu hapa hasa TVs zetu kwa CCM na serikali yake ni kama MBWA kwa CHATU. Tuliokuwa mbali na Jangwani hakuna tuliloambulia.
 
Ikulu pale ni mahara patakatifu - mtu anayesema uwongo lazima nguvu ya mungu ifanye kazi yake. na bado
 
Kwa nini vyombo vya habari vya nje kama CNN, SKY NEWS, BBC, Aljazeera, ...., haviupi umuhimu uchaguzi mkuu wetu? Vyombo vyetu hapa hasa TVs zetu kwa CCM na serikali yake ni kama MBWA kwa CHATU. Tuliokuwa mbali na Jangwani hakuna tuliloambulia.
Angalia you tube video...
 
Kwa nini vyombo vya habari vya nje kama CNN, SKY NEWS, BBC, Aljazeera, ...., haviupi umuhimu uchaguzi mkuu wetu? Vyombo vyetu hapa hasa TVs zetu kwa CCM na serikali yake ni kama MBWA kwa CHATU. Tuliokuwa mbali na Jangwani hakuna tuliloambulia.

mkuu nadhani hivyo vinajua uchaguzi wetu SIO HABARI manake mshindi ameshajulikana tayari........hakuna competition!
 
WATANZNIA tumewaeleza na tunarejea tena na tena, kuwa huyu mtu "anaumwa".. Anaumwa, iwe ni swaumu, kisukari, shinikizo (bp), msongo wa mawazo, uchovu nk nk..lakini kwa ufupi mhe. Rais wetu si mzima ANAUMWA na muitazame tu sura yake ...hii haitokani na swaumu na kama anashindwa kufunga ni vyema aache thawabu haiji kwa fungo ambayo mtu haiwezi au hana afya njema...ni mwema wlio karibu nae kama akina kinanana wakaacha propaganda, wamshauri safari hii ampumzike. Haiwezekani anawa anadondoka hovyo hivyo kama "mbayuwayu"..anaumwa.

kama ipo siri kati ya Daktari na mgonjwa (duty of secrecy) basi ingebakia siri na Kinana hakupaswa kusimama kueleza watazanaia kile kilichomwangusha kwani Kinana si Dktari wake na hana utaalamu wa kujibu kiufasaha kwa nini Swaumu ishushe Sukari kwa mtu ambae amezoe kufunga? ANAUMWA...kwa nini hiyo sukari iwe inashuka akiwa jukwaani tu tena anapowahutubia watanzania na sio sehemu nyingine huko nje anakoenda?

Mkuu hiyo picha uliyoweka hapo ina ujumbe mzito sana ikiangalia vizuri unaona kabisa Ben na JK wako tofauti sana.
 
mkuu nadhani hivyo vinajua uchaguzi wetu SIO HABARI manake mshindi ameshajulikana tayari........hakuna competition!

Kaizer ngoja nimwambie muhudumu akuongeze kopo lingine.. kwa kweli mie sina kabisa msisimko na huu uchaguzi. :mad2:
 
mkuu nadhani hivyo vinajua uchaguzi wetu SIO HABARI manake mshindi ameshajulikana tayari........hakuna competition!

Nakubaliana nawe Kaizer. Yaani hizi TVs zetu zilikuwa "live" kabisa pale lakini alipodondoka Rais wetu wakahamishia kamera zao mbali kwenye umati utadhani aliyedondoka ni Makamba au Msekwa kwa "uzee"!
 
Mara kwa kwanza wakatuambia Usongo wa Mawazo
Mara ya pili wakatuambia Uchovu
Mara ya tatu Sukari imezidi ---- mmhh kazi ipo, tuambieni ukweli tu tujue.
 
halafu walinzi wa bongo bana!!!!

mzee alilamba sakafu kabisa, jana nimeona wako karibu yake.
 
Kaizer ngoja nimwambie muhudumu akuongeze kopo lingine.. kwa kweli mie sina kabisa msisimko na huu uchaguzi. :mad2:

unajua MJ1 ingekuwa kuna watu wametoana ngeu, au waliofungwa gerezani au kuuwawa tayari hiyo kwao ingekuwan habari. Rejea attitude waliyo nayo wenzetu kuhusu Africa. Sasa hivi wamekomalia mafuriko huko Pakistan na vita y Afghanistan

Siku watu wakiuwawa au tukicharangana mapanga kama wenzetu, then hiyo itakuywa bonge la habari!

sasa nina KIU.....
 
Nakubaliana nawe Kaizer. Yaani hizi TVs zetu zilikuwa "live" kabisa pale lakini alipodondoka Rais wetu wakahamishia kamera zao mbali kwenye umati utadhani aliyedondoka ni Makamba au Msekwa kwa "uzee"!

Kiongozi mi nilicamp kabisa nikasahau kwa muda bia yangu lakini nikaishia kuona TOT na wanachi tu.....:confused2:
 
Hii inashangaza sana. Hebu sote tuwe makini na tujiulize maswali haya?

1. Huyu ni Rais wa nne Tanzania Bara, je wale watatu waliopita walianguka mara ngapi?
2. Kwani wao hawakuwa na kazi nzito kama yeye JK kwa sasa?
3. Awamu ya pili alikuwa ni his ex Mzee Mwinyi, na alikuwa ni moslem!! Je alianguka mara ngapi jukwaani au popote au hata kuzimia?
4. Huyu Rais wetu JK ameshaanguka mara nne public, na hatujui private ni mara ngapi?? Je hatujaweza kuona kuwa kuna hutilafu kubwa sana katika mwili wake na afya kwa ujumla?
5.Saumu ya masaa machache haiwezi kabisa kumwangusha mtu mwenye afya yake. Ninafahamu daku huliwa usiku, say kama hata amekula daku saa 2 mbili usiku, bado ana uwezo wa kushinda njaa kwa masaa mengi sana. Mbona wakristu wakifunga ni say kuanzia saa mbili usiku baada ya dinner na hakuna cha daku na bado hata hawasinzii ofisini? Tuwe tunajadili masuala kwa upana!! Afya ya huyu mheshimiwa ni zaidi ya ujuavyo!!
6. Ni kweli Dr. Slaa alianguka bafuni Mwanza na kuvunjika mkono, kumbuka kuwa mahoteli mengi yanatumia tiles za bafuni imara kiasi gani? Tena ukizingatia ni za China mara nyingi? Ile ilikuwa ni accident, hii ya JK si accident, ni madhaifu ya afya yake.

Watanzania wote, ni vema tufumbue macho na kuvaa kiona mbali kuhusu afya ya huyu mtukufu wetu!! Ifahamike kuwa ugonjwa hauombwi na kila mtu angefurahi kama asingeugua, ila basi unapoumwa ni vema ukaweka wazi, hata kama si details but tunajua kabisa huyu ndugu pengine ana low/High BP/Sugar and many other serious illiness!! Kulikoni kujitafutia visingizio lukuki, mara saumu kali, mara alisafiri mno hajapumzika ndiyo maana mwili umeishiwa nguvu, etc, etc. Hivi kweli kama unajua kuwa huna stamina ya kustahimili kazi nyingi ni kwa nini usi-delegate? (Hapa ni kwasafari zaidi).

Pole Rais, pole sana, weka wazi afya yako ilii tukuombee. Ugonjwa ni jambo la kawaida!!Hakuna atakayekunyang'anya hicho kitu eti kwa kuwa umeweka bayana afya yako. Mtasema pengine ugonjwa ni siri ya Dr. na Mgojwa, ni kweli ila magonjwa kama lilivyo general si siri, pengine details zake ndiyo siri. Kwani nini bwana!! Mimi nitasema tu, mbona hata wenye ukimwi wameamua kuvunja ukimya siku hizi na hawaogopi? Sembuse wewe mheshimiwa ambaye tatizo lako ni la kawaida si ukimwi??!!

Dr. wa Rais, tafadhali eleza report ya kiukweli, not propaganda!! Ugonjwa hauna propaganda!! Au ikiwezekana apumzike, bado ataendelea kupata maisha bora kama Rais mtaafu tu na aweze kuishi maisha marefu. Msimchoshe tafadhadhali. Mpeni ushauri wa ukweli.
 
Kiongozi mi nilicamp kabisa nikasahau kwa muda bia yangu lakini nikaishia kuona TOT na wanachi tu.....:confused2:
Halafu John Komba pamoja na unene, sukari na presha alionayo na mihangaiko yooote kwenye lile lori la TOT yeye haanguki! Kikwete wetu kuna kitu kinamsumbua ambacho ipo siku kitasemwa tu. Mwambieni Mtikila aende mahakamani. Afya ya JK, kwa mujibu wa KATIBA yetu ya JMT, inamwondolea sifa kuendelea kuwa Rais wetu.
 
Back
Top Bottom