Mwanajamii one nimekaa nikafikiria ulichoandika hapa imenilazimu nirudi kukujibu tena, hivi wewe mwanajamii one hii ni nadharia ya kusoma vitabuni tu au umewahi kuona mgonjwa ukiwa kama daktari? Ingekuwa hivyo basi wagonjwa kifafa wote wangekuwa walemavu na wenye makovu kichwani kutokana na kujibamiza kichwa wanapoanguka ghafla kama ulivyosema.
Ukweli ni kuwa wagonjwa wa kifafa hasa cha muda mrefu kama watu wazima huwa wanajua hiyo hali inapowatokea, huweza hata kuomba mkeka walale, au utaona anaondoka karibu na kitu cha hatari kama moto. Sasa kama hujataka kukubali matokeo kama alivyowahi kuomba kiti mwanza ukabaki kubishana kichwani mwako ukitaka kujikaza ndio mwili huanza kunyong'onyea hatimaye kuanguka. Alafu unasema huwa wanarusha miguu, na kutoa povu, tungeona miguu wapi wakati kamera zilihamishwa? tungeonaje povu wakati alizungukwa na TIS? Unajua kuna wagonjwa kifafa wengine huwaweza kuachia hata mkojo? na ukiona huyo utasema wote lazima wakojoe? Hujawa mkweli hapa ingawa hatu rule kuwa atakuwa na kifafa, lakini katika fani yako ulitakiwa uwe na list of possible diagnosis na zidhani katika hatua ya awali kama hii unaweza ku-rule out kifafa.
YouTube - Jk aanguka jangwani 2010