Kikwete a smart Man that I know

Kikwete a smart Man that I know

Huyu eddy si ni ndugu yenu huko Lumumba?? Kumbe bado mafisadi yamejaa CCM eeehh teh teh teh

Au ndio wale wa Madawa ya Kulevya ambao Rais ameapa kula nao sahani moja teh teh teh

Ndio maana nasema hivi Magufuli anakazi kubwa huyo Jamaa niGamba lkn ameanza kununa sasa hayuko peke yake kwenye maofisi
 
Last edited by a moderator:
Sasa mtu unapojiita mwanamabadiriko alafu unamsifia JK tukueleweje? Hivi hii nchi unafiki utaisha lini? Yani leo JK kawa mzuri? Ajabu hii hata shetani anatushangaa Watanzania kwa Unafiki!!
Mbona pia kamponda JK, eti kasafiri nje ya nchi mara nyingi zaidi, kuliko alivowatembelea wazazi wake huko kijijini kwao Msoga.
 
Mkuu, umeongea vema kabisa. Mafisadi wanaweweseka na wanatafuta pa kutokea ili kumchafua Magufuli. Hawatafanikiwa. Tunazidi kumuombea kwa Mungu ili ampe nguvu na utashi wa kupambana na mafisadi na kurekebisha mambo yote yaliyoporomoka wakati wa utawala wa Kikwete

JK kamwachia watu wake wale wale hata walinzi ni wale wale waliokuwa kwa JK , wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu wakuu, na sasa JK na Mkapa wapo busy kuhakikisha watu wao wanapenyezwa kwenye baraza la Mawaziri hivyo kuendeleza ule mfumo wa kizazi cha kutafuna pesa za umma kwa mbinu mbalimbali,Magufuli hataweza kufanikiwa ingawa atajaribu kidogo lakini huu mfumo chakachuaji utamkwamisha tu kwani wengi waliopewa dhamana ya kusimamia utendaji na wao ni vinara wa ufisadi.
 
Weka na mambo ambayo hayakutekelezeka,pia tuambie na ile speech yake juu ya esrow saga,ule ndio usmart?Usitutie hasira
 
Mfumo chakachuaji ni kikwazo kikubwa kwa dhamila ya Magufuli kutokana na wananchi kuamini cheo si dhamana tena bali cheo ni njia ya kupata Utajiri mkubwa, hivi sasa familia nyingi wanajiandaa kuwafanyia tafirija ndugu zao ambao watakuwa mawaziri na kuvikwaa vyeo wakiamini kuwa cheo ni njia ya kujikwamua binafsi si dhamana tena. Tanzania walipaswa wajifunze Africa kusini, Botswana na Namibia ambapo wafanyakazi wa umma wote wamejengewa mifumo bora ya kuwadhibiti na ufujaji wa pesa za umma pia wanapewa mikopo ya Nyumba na gari hivyo matukio ya ufisadi ni madogo sana ukilinganisha na Tanzania.
 
Weka na mambo ambayo hayakutekelezeka,pia tuambie na ile speech yake juu ya esrow saga,ule ndio usmart?Usitutie hasira

JK aliwahi kusema anawajua wauza unga wote kwa majina lakini aliogopa kuwataja mpaka ametoka ikulu hakukuwa na dalili ya kupungua kwa biashara hiyo.
 
Ndio maana nasema hivi Magufuli anakazi kubwa huyo Jamaa niGamba lkn ameanza kununa sasa hayuko peke yake kwenye maofisi

Ni vigumu Magufuli kufanikiwa kutokana na watendaji wengi wa Chini kuwa vinara wa ufisadi huku wananchi wakiwa chanzo cha ufisadi kutokana na kudai maendeleo , misaada pindi wawaonapo ndugu zao wamepewa vyeo na dhamana Fulani hivyo wengi hufanya ufisadi ili waonekane kuwa wanaendana na sura za vyeo vyao.
 
The Boss you mean Magufuli hua anaropoka kabla ya kupata professional advice ya jambo husika?
 
Last edited by a moderator:
Huu ulioandika ni upumbavu.

10 yrs kikwete kaimalizia angan kama popo na kwa gharama zakutisha- katutia hasara isiyo na kiwango.


This man (Maguful) ndo kwanza katoa hotuba na baraza lake hajaunda.


Why unampigia unajim as if ameshindwa utekelezaji kama alivyofeli mkwere

Elimu hoyoooo kabisa

Afya hovyoooo kabisa

Viwanda na biashara tumekuwa shamba la bibi kila kichaa anajivunia nakubebaba atakacho

Madawa ya kulevya ndo usiseme

Usmati wa mkwere upo wapi mpuuzi wewe zaid yakunua nakucheka hovyo tukiumizwa na makodi makubwa na yeye kukimbizia busha amerika baba zetu wakifia Muhombili


Grrrrrrrrrry this is a Stupidy thread so far to come accross my eyes.

Hawa ndo wanastahili kushinda Facebook kwanini utukane matosi?Jenga hoja
 
Bwana mdogo weka akiba ya maneno Magufuli ni mCCM labda kama umeanza kuijua CCM baada ya magufuli kuwa Rais vinginevyo....baada ya muda kupita kwa kuona aibu unaweza kuja na ID mpya kumwaga povu CCM niile ile sikiliza watu atakao wateua kwenye Baraza la Mawaziri ndo utaelewa

Ni kweli kabsa hakutakuwa na jipya Magufuli atakuwa akitoa maagizo lakini utekelezaji utakuwa mgumu, JK na Mkapa wamepenyeza watu wao kwenye baraza lake mawaziri na mfumo kubakia ule ule hivyo kuendeleza uchakachuaji na ufisadi kama kawaida.
 
Mimi nadhani ni mapema mno kutoa hukumu kwa raisi aliyepo madarakani kwani HATA kazi bado haijanza......
Tumesikia mipango na sera kipindi CHA kampeni na kwa sera hizo nzuri zenye kuleta tumaini jipya tukaamua kumpa KURA zetu....
Tunachokingoja sasa ni utekelezaji wa Yale aliyokuwa akituhubiria........lakini yeye kama yeye hawezi kuyafanya peke yake Bali atahitaji msaada kutoka kwenye timu yake....na wananchi kwa ujumla......
Anachotakiwa sasa ni kuwa makini katika uteuzi wa balaza la mawaziri.....
Nadhani kwa tuliowengi nyota njema ndio itaanza kuonekana hapo......kuanzia hapo ndio tutaanza kubashiri safari hii inayoitwa kuwa ni ya mabadiliko ya kweli......

TUMPE MUDA....
 
Ni kweli kabsa hakutakuwa na jipya Magufuli atakuwa akitoa maagizo lakini utekelezaji utakuwa mgumu, JK na Mkapa wamepenyeza watu wao kwenye baraza lake mawaziri na mfumo kubakia ule ule hivyo kuendeleza uchakachuaji na ufisadi kama kawaida.

Huo ubashiri wako hakuna mantiki......kusema kuwa hakutakuwa na jipya katika uongozi huu MPYA ni kuonyesha dhahiri kuwa bado akili imenasa kwenye Tope la kampeni.....
 
Nitabakia mpinzani daima mpaka pale ccm itapoondoka. Mfumo ccm umeota mizizi, mtu mmoja aitwae Pombe hawezi ufumua. Naamini maendeleo yatakuja kwa kutoruhusu chama kimoja kudumu madarakani muda mrefu.

Mkuu na huu ndo ukwel!
Na wakiona kakomaa wana mkolimba!

Mshikaji wangu mbunge, anasema watu wamemaindi kuwachukulia hela zao! Eti katudhulumu sasa ataona! !
I was like what? ??????
Nikamuuliza sasa mtamfanya nini? Anasema yaache hivo hivo kwa sasa! Nikaishia duuuuh! ! !
 
Samahani mkuu,
Mchakato wa ujenzi wa mahakama maalum ya mafisadi na majizi umefikia wapi?

Mahakama ya ufisadi aliitumia kama mbinu ya kusaka kura lakini chombo kama Mahakama huundwa na Katiba hawezi kuunda Mahakama pasipo kuitumia katiba mpya, na endapo ataanzisha hiyo Mahakama aanze na kesi ya zile billion 250 zilizolipwa makandarasi hewa wizara ya Ujenzi, aliyenunua kivuko Feki cha 1978 kwa billion 8 wakati kivuko kipya cha Azam ni billion 5 tu, ianze na kesi ya escrow, Buzwagi, mabehewa feki, mikataba ya Gesi, uagizaji sukari nje, Mabilioni yaliyopotea kwenye ukarabati wa reli ya kati, chenji ya Rada, zile billion 6 zilizoliwa na akina Warioba kwenye mchakato wa katiba,pia Mabilioni chenji bunge la rasmu ya katiba pesa ambayo ilipeperushwa na Sita. Magufuli akiweza kuanza na haya nina hakika atakaa ikulu mpaka anakuwa mzee kama mseveni na Mugabe wa Zimbabwe.
 
Nitabakia mpinzani daima mpaka pale ccm itapoondoka. Mfumo ccm umeota mizizi, mtu mmoja aitwae Pombe hawezi ufumua. Naamini maendeleo yatakuja kwa kutoruhusu chama kimoja kudumu madarakani muda mrefu.

Siddhani kama naweza kusupport serikali ya ccm kwani kopo la chooni huwezi kunywea maji wala juice hata uliosheje! hivo magufuli hawezi kuibadilisha ccm dawa yake ni kuing'oa tu!
 
Mimi nadhani ni mapema mno kutoa hukumu kwa raisi aliyepo madarakani kwani HATA kazi bado haijanza......
Tumesikia mipango na sera kipindi CHA kampeni na kwa sera hizo nzuri zenye kuleta tumaini jipya tukaamua kumpa KURA zetu....
Tunachokingoja sasa ni utekelezaji wa Yale aliyokuwa akituhubiria........lakini yeye kama yeye hawezi kuyafanya peke yake Bali atahitaji msaada kutoka kwenye timu yake....na wananchi kwa ujumla......
Anachotakiwa sasa ni kuwa makini katika uteuzi wa balaza la mawaziri.....
Nadhani kwa tuliowengi nyota njema ndio itaanza kuonekana hapo......kuanzia hapo ndio tutaanza kubashiri safari hii inayoitwa kuwa ni ya mabadiliko ya kweli......

TUMPE MUDA....

Uteuzi wa mwanasheria mkuu na naibu spika ni kiashiria cha baraza la mawaziri kuwa na mawaziri wale wale yaani ccm ile ile ya mbele kwa mbele isiyojali shida za wengi.
 
Jana nimesikiliza hotuba hotuba ya Magufuli nikalinganisha na za JK, kuna jambo moja interesting. Hotuba ya JPM ilikuwa ni thesis kuliko speech, ililenga zaidi kuoanisha na akili za watanzania walio wengi, yaani was too theoretical.

Wakati JK akisema ataanzisha mradi Fulani atakwambia na pesa kapata wapi, mfano aliposema ujenzi wa daraja la kigamboni alisema NSSF ndo watakaotoa pesa na ndio watakuwa wamiliki wa mradi husika. Aliposema ataibadili Kawe alisema NHC ndo wasimamizi na wamiliki wa ule mradi na pesa watapata kutoka exim bank china. Aliposema atajenga bandari mpya ya bagamoyo ni uwekezaji kati ya china Tanzania na oman, JK aliamini zaidi katika FDI.

Sasa jana tuliambiwa ufufuaji wa viwanda hapo ilipaswa kusema je ni merger and acquisition au ni business repurchase? Mtu ukishamuuzia gari na akakulipa badae ukalitaka atakuuzia kwa bei atakayotaka yeye. Kuhusu mashamba yapo mashamba wenyeji walishalima na kujenga makazi je utawafurumusha urejeshe shamba? yapo mashamba hati zilishakopewa bank hayo itakuwaje?

Kusema kuwa tuna ng'ombe wengi basi tutengeneze viatu tuvae wenyewe, hii haingii akilini, kiatu cha pure leather English boot kinauzwa zaidi ya laki nne, nani mswahili yuko tayari kununua hicho kiatu? Hebu tujiulize hizi ngozi huwa zinaenda wapi? sijawahi sikia fuso la ngozi limekamatwa mpakani hivyo haziuzwi kwa magendo.

Amekiri mwenyewe kuwa mkulima wa pamba anatozwa shuru tozo kodi zaidi ya 26 huu ni unyonyaji wa waziwazi, lakini nani kaweka haya maushuru ushuru kama yeye anavyoyaita? anadhani hayapo kisheria? anadhani akina mbowe hawayaoni? mbona hawapeleki miswaada bungeni kuyaondoa? ukweli there is a chain of bureaucracy.

Machoweza kusema hotuba ya mkuu yalikuwa maono, sasa magufuli anahitaji wataalam wa uchumi na biashara ili waweze kutransform maono yake into practice.
Afadhali na wewe umemuona, kaanza kwa kufuta ada na michango ambayo inakadiriwa kuwa billion 200 hakusema atatoa wapi fedha za pengo hili. Akazungumzia PAYE asiseme pesa ziko wapi huku akikiri matarajio ya mapato tra yamekuwa hayafikiwi. Ukimsikiliza vyema mwanzoni anapondea mafunzo nje kwa kusema wataalam waje kufundisha hapa ila wakati anazungumzia sekta ya afya anasema anasema watu wakasome nje ili watu watibiwe hapa. NAMI NIMALIZIE KAMA YEYE NA KADHALIKA NA KADHALIKA, MAANA KALIPENDA KWELI NENO HILO
 
Mkuu na huu ndo ukwel!
Na wakiona kakomaa wana mkolimba!

Mshikaji wangu mbunge, anasema watu wamemaindi kuwachukulia hela zao! Eti katudhulumu sasa ataona! !
I was like what? ??????
Nikamuuliza sasa mtamfanya nini? Anasema yaache hivo hivo kwa sasa! Nikaishia duuuuh! ! !
Ndio Pombe ajue, mfumo ccm ni mzito sana, alishindwa Nyerere, anaanzisha viwanda huku watu wanamhujumu, mwenyewe kakimbia ikulu.
 
Back
Top Bottom