Inevitable
Member
- Apr 27, 2012
- 82
- 159
Jana, statement toka Ikulu ilieleza kuwa Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya mafao ya Pensheni, kama ilivyoombwa na chama cha wafanyakazi Tanzania (TUCTA) siku ya sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi, 2022), ambapo sasa amekubali ombi la kupandisha malipo ya mafao, kutoka 25% iliyokataliwa na wadau hadi 33.3%.
Ametaka TUCTA, wizara ya fedha na Chama cha Waajiri (ATE), kuendelea kushirikiana ili kukamilisha taratibu za malipo ya mkupuo huo wa asilimia 33.3% badala ya 25% iliyokataliwa mwaka 2018.
Kanuni za Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2018, ziliweka kikokotoo kimoja cha asilimia 25 ambacho kiliweka usawa kwa wastaafu wote kupata mafao yenye fomula moja, tofauti na awali kulipokuwa na fomula mbili.
Kikokotoo kipya kwenye kanuni kilikuwa ni asilimia 25 kwa mafao ya mkupuo na asilimia 75 inayobaki kulipwa kama pensheni ya mwezi kwa kila mwezi hadi mwanachama atakapofariki dunia.
Hata hivyo, katika kikokotoo hicho, umri wa kuishi ulikadiriwa kuwa ni miaka 12.5, ikiwa ni umri uliokadiriwa kuwa mwanachama ataishi baada ya kustaafu.
Kwa mujibu wa kikokotoo cha NSSF ambacho kimekuwapo kwenye kanuni za shirika hilo tangu mwaka 2014, mwanachama anapostaafu analipwa asilimia 25 ya mafao ya mkupuo na kilichobaki kinalipwa kama mshahara wa kila mwezi.
Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2018, imetaja jumla ya mafao saba ambayo ni manne ya muda mfupi (fao la upotevu wa ajira, fao la ugonjwa, fao la uzazi na mkopo wa nyumba) na matatu ya muda mrefu ambayo ni pensheni ya uzeeni, fao la ulemavu na fao la warithi.
Kwa hili, niseme Rais Samia na serikali yake wanastahili pongezi.