uni
Najua hapa kijijini kwetu kuna uhuru wa kuongea bila kuvunja sheria za kijiji nami natumia uhuru huo huo,Langu moja tu ni kuhusu hizi fake ID. Wote tunatumia fake ID na zinasaidia mambo mengi,zinafanya mtu unatoa lolote la moyoni bila kujali lakini kuna watu wanazo Id mbili mbili sio shida kwakuwa sheria za kijiji zinaruhusu
Sasa hili la mwanaume kutumia ID ya kike linamaanisha nini? Humu ndani kama jina la kijiji linavyojieleza watu wanajenga mahusiano,wanatengeneza urafiki,sasa kama mwanaume unapotumia ID ya kike unataka kutuambia nini? kwamba unafurahi wanaume wanavyokutongoza? au unafurahia unavyotoa maada kama mwanamke na watu wanavyotoa maoni yao,furaha inakuwa wapi haswa? sijui kama kua wanawake wanatumia ID ya kiume pia ila nauliza tu kwa wanaume wenzangu hili mnalichukuliaje?
Uhuru unapopitiliza madhara yake ndiyo haya sijui mpaka mtu unatumia ID ya kike unakuwa umefikiria nini?