Kikao cha siri cha WanaCCM "asilia" Jana usiku cha pale Dodoma huenda kikasaidia kupambana na wagombea "wa kupandikizwa"

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu ambao ni CCM asilia walikutana kwa siri jana usiku sehemu fulani pale Area C Dodoma kubuni mbinu za kushughulika na wagombea wa "kupandikizwa".

Wagombea wa kupandikizwa wako wa aina mbili.

Moja, ni wale ambao wana uswahiba na Mwenyekiti lkn hawana mvuto wala hawajulikani majimbo wanakotumwa kugombea. Mf. Prof. Kitila kugombea Ubungo, na prof. Kabudi kugombea Kilosa.

Pili, ni wale waliotoka vyama vingine na kupewa feva ya kugombea bila kupingwa ndani ya ccm.

Haya mawili yamewaumiza Sana wanaCCM wapiganaji na wafia chama. Na Kuna mengi yamepangwa tuombe Mungu yafanikiwe. Muda utaongea.

CCM tuko pamoja lkn hatuna umoja.
 
Mkuu Wewe naye eti unafanya propaganda, huu ni upuuzi kama wa mtoto wa chekechea,CCM ni taasisi sio Saccos kama chadema
 
Meko ameiweka CCM kiganjani. Analotaka ndilo linafanyika.
Ili kuwadhibiti wenye dhamira ya kumnyima kura pale Dodoma jana, wajumbe wa mkutano mkuu toka kila mkoa walitakiwa kupiga kura na kuziweka sanduku moja.
Hii ingesaidia kubaini ni mkoa gani umemkataa.
 
Mkuu Wewe naye eti unafanya propaganda, huu ni upuuzi kama wa mtoto wa chekechea,CCM ni taasisi sio Saccos kama chadema

Huyo mleta hoja kaoongea ukweli ambao kwa viongozi madictator haupaswi kusikika. Kinachofanyika hivi sasa ni hofu dhidi ya mwenyekiti, kwani ana kofia nyingine ambayo ni rahisi kuitumia kwa mwanachama yoyote, asiyekubali kutii hata mambo yasiyo na maslahi kwa chama. Kwa sasa wanaccm wameanza kujua vyema hatari ya kofia mbili, kwani wameona zinaweza vipi kutumika vibaya hata dhidi yao.
 
Waache walielie tu
Wamechelewa sana, kati ya 2015 na 2017 ndio lilikua dirisha pekee la kumdhibiti Magufuli. Kwasasa wavumilie tu, ikifika 2025 CCM kitakua chama tofauti kabisa, siasa kali za chuki ndio patakua nyumbani kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…