Kisa cha Jaji na profesa katika uchaguzi wa 1995

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
JAJI MARK BOMANI KATIKA KUMBUKUMBU ZA PROF. KIGHOMA MALIMA UCHAGUZI WA RAIS DODOMA 1995

Nimesoma makala ambayo imezunguka sana katika mitandao ya kijamii kuhusu Mark Bomani katika kinyang’anyiro cha Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM mwaka wa 1995.

Makala hii kila nikiisoma inanirudisha nyuma miaka 25 iliyopita wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi baada ya kurejeshwa mwaka wa 1992 na kwa hakika huishia kwa kucheka napomkumbuka Prof. Malima kwani ni kama vile namuona anavyonihadithia kwa staili yake ya hata jambo likiwa zito kiasi gani yeye atakuhadithia katika njia ya kukufanya wewe ucheke na nyie wasikilizaji wake mcheke pia.

Siku moja katika mazungumzo yetu alinihadithia jinsi siasa za Tanzania zinavyochezwa kwa ustadi wa hali ya juu kiasi ni watu wajanja sana ndiyo wanaweza kutambua na kutegua kitendawili pindi kinapomkabili.

Prof. Malima akanipa mfano wa Jaji Mark Bomani pamoja na yeye wa wanachama wengine wa CCM walipoomba uteuzi kuwa wagombea wa nafasi ya urais na majina yao yafikishwe Halmashauri Kuu ya CCM ili waingizwe kwenye mchakato.

Prof. Malima anasema yeye aliomba uteuzi ule kwa kughadhibishwa na gazeti moja lililoandika mbele kwa wino mweusi wa kukoza, ‘’Waislam Waiogopa Ikulu.’’

‘’Hivi hawa jamaa wanatudharau sana sisi,’’ Prof. Alisema huku anacheka.

Lakini gazeti lile lilikuwa limeandika ukweli.
Hapakuwa na Muislam yeyote aliyechukua fomu kuutaka urais.

Prof. Malima anasema, ‘’Pale pale nikamwambia dereva wangu akaiangalie gari ajaze mafuta safari Dodoma kwenda kuomba nafasi ya kugombea urais.’’

Prof. Malima mwenyewe alikuwa na historia ya kutukuka katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwani akiwa kijana mdogo na bingwa wa hesabu aliacha shule Mzumbe mwaka wa 1957 kurudi kijijini kwao Kisarawe kujiunga na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya uongozi wa Julius Nyerere.

Sasa ikiwa Malima hakuiogopa Government House ya Governor Edward Francis Twining na Special Branch yake vipi atishike na Ikulu ambayo anaijua ndani nje?

Wakati ule lile gazeti lilipotoka na maneno yale ya kuwabeza Waislam katika ukurasa wake wa mbele hapakuwa na hata Muislam mmoja aliyeomba nafasi ya kutaka achaguliwe kugombea urais.

Prof. Malima akaendelea kusema kuwa ‘’Mimi nikijua fika siwezi kuchaguliwa lakini nilitaka nitoe jibu kwa lile gazeti kuwa Waislam hatuiogopi Ikulu.’’

Ndani ya Bunge la Tanzania kulikuwa na kikundi cha Wabunge wamejichagua na kutengeneza genge ambalo kazi lililojipa ilikuwa ni kumzomea Prof. Malima ndani ya Bunge kwa kila atakalofanya.

Pamoja na Wabunge hawa walikuwapo pia na wahariri wa magazeti ambao wao kazi yao kuu ilikuwa ni kumuandika Prof. Malima kwa ubaya.

Katika hali hii Prof. Malima alikuwa anaijua hali vizuri sana.

Sasa tuje kwa Jaji Mark Bomani.

Baadhi ya wananchi na marafiki wa Mark Bomani walimwendea na kumuomba agombee urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na inasemekama walimshinikiza sana aombe nafasi hiyo na yeye hakutaka kuwavunja akiamini kuwa anaweza akatoa mchango katika ujenzi wa taifa la Tanzania akawakubalia.

Jaji Bomani hakuwa anafahamika sana katika duru za siasa lakini aliongoza kwa idadi ya wadhamini kwa nafasi ile akifuatiwa na John Malecela.

Prof. Malima akawa anasema, ‘’Wengi katika sisi tuliokwenda Dodoma kufanyiwa usaili ukinitoa mimi wakidhani kuwa zoezi lile lilikuwa linaendeshwa kwa umakini mkubwa na kuwa wagombea watakuwa na nafasi ya kujieleza na yule ambae ataonekana ana sifa zinazohitajika ndiyo atakuwa mshindi.’’

Baada ya kuingia Prof. Malima katika kinyang’anyiro kile cha urais akaongezeka Muislam mwingine – Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikwete katika maziko ya Benjamin Mkapa alisema alisukumwa kuingia kwenye kinyang’anyiro kile na iko siku ataeleza kisa hicho.

Leo baada ya zaidi ya miaka 25 ndiyo nami nimejifunza vipi siasa za Tanzania zinavyoendeshwa.

Prof. Malima amekuwa ndani ya chama kile toka enzi za TANU na nikisoma kumbukumbu zake na kufanya rejea katika mazungumzo yetu natembea katikati ya mistari ya maneno yake.

Kwa hakika nimejifunza mengi.

Nimeoona pia Prof. Malima na yeye kama binadamu amefunzwa mengi mengi ndani ya CCM.

Nimeweza kubaini kuwa kuna sifa za ziada mtu anatakiwa awe nazo ndipo achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.

Ikiwa mimi nimezitambua sifa hizi zisizoonekana kwa macho Prof. Malima yeye bila shaka alikuwa anazijua vizuri na alikuwa na uwezo wa kuziona kwa macho yake mawili.

Kuwa Jaji au Profesa si moja ya sifa za Urais.

Prof. Malima anasema alipofika chumba cha mapumziko kabla ya kuingia ndani kuhojiwa na Central Committeee alimkuta Jaji Mark Bomani keshafika zamani na mkononi ana makaratasi mengi anatalii.

Mkononi Jaji ana kalamu anapiga mstari hapa na pale anahangaika kuweka kila jambo mahali pake.

Wasukuma na Wazaramo ni watani.

Prof. akamuuliza Jaji katika njia ya utani, ‘’Jaji hiyo nini?’’

Jaji Bomani akamjibu, ‘’Hii hotuba yangu mbele ya Kamati.’’

Prof. akacheka sana.

Hapa nilipo ni kama vile namuona Prof. na kicheko chake nakisikia.

Prof. akamwambia Jaji kuwa hawana muda wa kusikiliza hotuba yake na atakuwa na bahati kubwa ikiwa atapewa dakika tatu.

Jaji Bomani alishtuka na Profesa alimuona kwa hakika kabisa Jaji alikuwa kashtuka kwani hakulitegemea hilo.

Iweje jambo muhimu na kubwa kama hili Kamati iwe haina muda wa kuwasikiliza?

Prof. Malima hakuwa na la zaidi la kuongeza alitulia tuli anamwangalia Jaji lakini ndani ya nafsi yake akimuhurumia sana na huruma yake Prof. Malima ilitokana na kuwa Jaji Bomani atavunjika moyo atakapotambua kuwa yeye hakuwa anajua siasa za Tanzania ngoma zinaporindima ni mtindo upi wa ngoma wachezaji hucheza.

Prof. Malima alikuwa anajua fika kuwa si yeye wala Mark Bomani watapitishwa, alikuwa anajua kuwa palitakiwa wawepo watu mfano wa wao ili ngoma inoge.

Prof. Malima aliingia kuhojiwa na kutoka muda mfupi.

Hapa kwenye mahojiano machozi yalinitoka kwa kucheka.

Prof. Malima alijaaliwa kipaji cha kuchekesha.

Hakukaa akiwa wima alimuaga mtani wake Jaji.

Jaji akamuuliza Prof, ‘’Husubiri matokeo?’’

Prof. Malima aliniambia alipigwa na mshangao mkubwa.

Central Committee iliwapitisha - Kikwete, Mkapa na Msuya kuwa majina yatakayokwenda mbele kwa uchaguzi wa jina moja la mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM.

Taarifa zinasema Jaji Mark Bomani aliumia sana kwa kukatwa jina lake.

Prof. Malima yeye njia nzima wakati anarudi Dar es Salaam ni kuwa kila akikumbuka aliyoyaona Dodoma yeye ilikuwa ni kucheka tu kwani yale yalimkumbusha yaliyomfika Chimwaga mwaka wa 1992 pale alipofanyiwa njama asichaguliwe NEC iliyokuwa na viti 20.

Huwezi kuchoka kumsikiliza Prof. Malima kwani alikuwa anajua mengi sana na akiyaeleza kwa namna ambayo ingawa mengi ni ya kusikitisha atakuacha taaban kwa kucheka.
 
Angalia picha:

Screenshot_20200918-223049~2.jpg
 
'Prof. Malima anasema yeye aliomba uteuzi ule kwa kughadhibishwa na gazeti moja lililoandika mbele kwa wino mweusi wa kukoza, ‘’Waislam Waiogopa Ikulu.’’

Nilitaka kushangaa makala isihusishe mambo ya ki-islam.
Na yeye tu alikuwa na bahati mbaya ya kuundiwa kundi la kuzomewa bungeni na kuundiwa njama za kumzuia kugombea U-Nec! Wakati huohuo kwenye kinyang'anyiro cha U-Rais Prof. akagadhibishwa na stori ya "Waislam waigopa Ikulu" hapohapo likaja wazo la kugombea Urais! hivyo tu ghafla. Inaonyesha Prof. alikuwa anaonewa sana.

Kabla ya wino wa "Waislam waiogopa ikulu" kukauka Kikwete akatia mguu, na hapa inaelezewa kana kwamba naye aligadhibishwa kwa nini Waislam waambiwe wanaiogopa Ikulu.

Sasa utajiuliza mwenyewe, kwa mikakati ile ya kampeni ya Kikwete ikiwemo kuzunguka na ndege akiwa na Bwana Edo kusaka wadhamini (jambo geni na la ajabu sana ndani ya Ccm nyakati zile), kambi zake kulala mahala pamoja nk ni kuwa alijistukiza kuchukua fomu. Mungu jalia Mzee wetu Kikwete asiondoke Duniani mapema, siku akiondoka utaona sarakasi za maandishi.
 
'Prof. Malima anasema yeye aliomba uteuzi ule kwa kughadhibishwa na gazeti moja lililoandika mbele kwa wino mweusi wa kukoza, ‘’Waislam Waiogopa Ikulu.’’

Nilitaka kushangaa makala isihusishe mambo ya ki-islam.
Mng"ato,
Ukiona makala imeandikwa kuna jina langu na Waislam hawamo jua hiyo si makala ya Mohamed Said.
 
'Prof. Malima anasema yeye aliomba uteuzi ule kwa kughadhibishwa na gazeti moja lililoandika mbele kwa wino mweusi wa kukoza, ‘’Waislam Waiogopa Ikulu.’’

Nilitaka kushangaa makala isihusishe mambo ya ki-islam.
Ndg hawezi kuandika makala bila kuhusisha uislam,huyu jamaa na ajenda zake za kidini bhana, kuna muda anaandika vitu unafurahia ila udini alionao unakera
 
Ndg Muddy hawezi kuandika makala bila kuhusisha uislam,huyu jamaa na ajenda zake za kidini bhana,Kuna muda anaandika vitu unafurahia ila udini alionao unakera
Red Label,
Kuna Professor wa African Studies katika siku tulipokutana alifurahi sana.

Akaniomba nihame hoteli twende nyumbani kwake.

Tulikuwa baada ya chakula cha usiku tunazungumza hadi usiku wa manane.

Anasema kama asingesoma kitabu cha Abdul Sykes asingejua kuwa Tanganyika kulikuwa na Waislam na hawa Waislam wamefanya makubwa katika kupigania uhuru.

Akanambia amefanya kazi AU Addis Ababa na Abuja na katika shughuli zake za kazi ametembelea balozi nyingi za Afrika duniani na kitu kilichomshangaza balozi za Tanzania Ulaya, Afrika na Asia hakuwahi kukuta maofisa Waislam.

Ikampitikia kuwa huenda Tanzania ni nchi ya Kikristo.

Alipokisoma kitabu cha Abdul Sykes ndipo akapata jibu.

Red Label haya aliyoona huyu profesa ndiyo udini.

Udini ni kwa wafuasi wa dini moja kuhodhi kila fursa katika nchi na kuwaweka wengine pembeni.

Udini si kuandika historia ya Waislam.

Hivi ushajiuliza kwa nini historia ya TANU na uhuru na Tanganyika ilipoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni (1981) ilipotoshwa pakubwa?

Nakuomba unapotaka kunitaja kwa jina usiniite Muddy tumia jina langu Mohamed.
 
Jaji Mark Bomani alikuwa kwenye tume ya taifa ya uchaguzi, kitendo cha yeye kuchukua fomu na huku akiwajua kuwa alikuwa kwenye nafasi hiyo nyeti kilitosha kabisa kumwengua ni kama aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, msajili wa vyama vya siasa Christopher Liundi wote walipotaka kugombea uongozi kupitia CCM walitoswa .
 
Na sababu ni hiyo hiyo, hawawezi kumruhusu mtengeneza sumu atumie sumu hiyo hiyo aliyoitengeneza kuwanywesha wenzake walioshiriki naye kuitengeneza, wenzie wote wanajua fika kuwa huyu ni muuaji mwenzetu, hivyo lazima wakudhibiti ili usije kuwaangamiza wao.
 
JAJI MARK BOMANI KATIKA KUMBUKUMBU ZA PROF. KIGHOMA MALIMA UCHAGUZI WA RAIS DODOMA 1995

Nimesoma makala ambayo imezunguka sana katika mitandao ya kijamii kuhusu Mark Bomani katika kinyang’anyiro cha Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM mwaka wa 1995.

Makala hii kila nikiisoma inanirudisha nyuma miaka 25 iliyopita wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi baada ya kurejeshwa mwaka wa 1992 na kwa hakika huishia kwa kucheka napomkumbuka Prof. Malima kwani ni kama vile namuona anavyonihadithia kwa staili yake ya hata jambo likiwa zito kiasi gani yeye atakuhadithia katika njia ya kukufanya wewe ucheke na nyie wasikilizaji wake mcheke pia.

Siku moja katika mazungumzo yetu alinihadithia jinsi siasa za Tanzania zinavyochezwa kwa ustadi wa hali ya juu kiasi ni watu wajanja sana ndiyo wanaweza kutambua na kutegua kitendawili pindi kinapomkabili.

Prof. Malima akanipa mfano wa Jaji Mark Bomani pamoja na yeye wa wanachama wengine wa CCM walipoomba uteuzi kuwa wagombea wa nafasi ya urais na majina yao yafikishwe Halmashauri Kuu ya CCM ili waingizwe kwenye mchakato.

Prof. Malima anasema yeye aliomba uteuzi ule kwa kughadhibishwa na gazeti moja lililoandika mbele kwa wino mweusi wa kukoza, ‘’Waislam Waiogopa Ikulu.’’

‘’Hivi hawa jamaa wanatudharau sana sisi,’’ Prof. Alisema huku anacheka.

Lakini gazeti lile lilikuwa limeandika ukweli.
Hapakuwa na Muislam yeyote aliyechukua fomu kuutaka urais.

Prof. Malima anasema, ‘’Pale pale nikamwambia dereva wangu akaiangalie gari ajaze mafuta safari Dodoma kwenda kuomba nafasi ya kugombea urais.’’

Prof. Malima mwenyewe alikuwa na historia ya kutukuka katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwani akiwa kijana mdogo na bingwa wa hesabu aliacha shule Mzumbe mwaka wa 1957 kurudi kijijini kwao Kisarawe kujiunga na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya uongozi wa Julius Nyerere.

Sasa ikiwa Malima hakuiogopa Government House ya Governor Edward Francis Twining na Special Branch yake vipi atishike na Ikulu ambayo anaijua ndani nje?

Wakati ule lile gazeti lilipotoka na maneno yale ya kuwabeza Waislam katika ukurasa wake wa mbele hapakuwa na hata Muislam mmoja aliyeomba nafasi ya kutaka achaguliwe kugombea urais.

Prof. Malima akaendelea kusema kuwa ‘’Mimi nikijua fika siwezi kuchaguliwa lakini nilitaka nitoe jibu kwa lile gazeti kuwa Waislam hatuiogopi Ikulu.’’

Ndani ya Bunge la Tanzania kulikuwa na kikundi cha Wabunge wamejichagua na kutengeneza genge ambalo kazi lililojipa ilikuwa ni kumzomea Prof. Malima ndani ya Bunge kwa kila atakalofanya.

Pamoja na Wabunge hawa walikuwapo pia na wahariri wa magazeti ambao wao kazi yao kuu ilikuwa ni kumuandika Prof. Malima kwa ubaya.

Katika hali hii Prof. Malima alikuwa anaijua hali vizuri sana.

Sasa tuje kwa Jaji Mark Bomani.

Baadhi ya wananchi na marafiki wa Mark Bomani walimwendea na kumuomba agombee urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na inasemekama walimshinikiza sana aombe nafasi hiyo na yeye hakutaka kuwavunja akiamini kuwa anaweza akatoa mchango katika ujenzi wa taifa la Tanzania akawakubalia.

Jaji Bomani hakuwa anafahamika sana katika duru za siasa lakini aliongoza kwa idadi ya wadhamini kwa nafasi ile akifuatiwa na John Malecela.

Prof. Malima akawa anasema, ‘’Wengi katika sisi tuliokwenda Dodoma kufanyiwa usaili ukinitoa mimi wakidhani kuwa zoezi lile lilikuwa linaendeshwa kwa umakini mkubwa na kuwa wagombea watakuwa na nafasi ya kujieleza na yule ambae ataonekana ana sifa zinazohitajika ndiyo atakuwa mshindi.’’

Baada ya kuingia Prof. Malima katika kinyang’anyiro kile cha urais akaongezeka Muislam mwingine – Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikwete katika maziko ya Benjamin Mkapa alisema alisukumwa kuingia kwenye kinyang’anyiro kile na iko siku ataeleza kisa hicho.

Leo baada ya zaidi ya miaka 25 ndiyo nami nimejifunza vipi siasa za Tanzania zinavyoendeshwa.

Prof. Malima amekuwa ndani ya chama kile toka enzi za TANU na nikisoma kumbukumbu zake na kufanya rejea katika mazungumzo yetu natembea katikati ya mistari ya maneno yake.

Kwa hakika nimejifunza mengi.

Nimeoona pia Prof. Malima na yeye kama binadamu amefunzwa mengi mengi ndani ya CCM.

Nimeweza kubaini kuwa kuna sifa za ziada mtu anatakiwa awe nazo ndipo achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.

Ikiwa mimi nimezitambua sifa hizi zisizoonekana kwa macho Prof. Malima yeye bila shaka alikuwa anazijua vizuri na alikuwa na uwezo wa kuziona kwa macho yake mawili.

Kuwa Jaji au Profesa si moja ya sifa za Urais.

Prof. Malima anasema alipofika chumba cha mapumziko kabla ya kuingia ndani kuhojiwa na Central Committeee alimkuta Jaji Mark Bomani keshafika zamani na mkononi ana makaratasi mengi anatalii.

Mkononi Jaji ana kalamu anapiga mstari hapa na pale anahangaika kuweka kila jambo mahali pake.

Wasukuma na Wazaramo ni watani.

Prof. akamuuliza Jaji katika njia ya utani, ‘’Jaji hiyo nini?’’

Jaji Bomani akamjibu, ‘’Hii hotuba yangu mbele ya Kamati.’’

Prof. akacheka sana.

Hapa nilipo ni kama vile namuona Prof. na kicheko chake nakisikia.

Prof. akamwambia Jaji kuwa hawana muda wa kusikiliza hotuba yake na atakuwa na bahati kubwa ikiwa atapewa dakika tatu.

Jaji Bomani alishtuka na Profesa alimuona kwa hakika kabisa Jaji alikuwa kashtuka kwani hakulitegemea hilo.

Iweje jambo muhimu na kubwa kama hili Kamati iwe haina muda wa kuwasikiliza?

Prof. Malima hakuwa na la zaidi la kuongeza alitulia tuli anamwangalia Jaji lakini ndani ya nafsi yake akimuhurumia sana na huruma yake Prof. Malima ilitokana na kuwa Jaji Bomani atavunjika moyo atakapotambua kuwa yeye hakuwa anajua siasa za Tanzania ngoma zinaporindima ni mtindo upi wa ngoma wachezaji hucheza.

Prof. Malima alikuwa anajua fika kuwa si yeye wala Mark Bomani watapitishwa, alikuwa anajua kuwa palitakiwa wawepo watu mfano wa wao ili ngoma inoge.

Prof. Malima aliingia kuhojiwa na kutoka muda mfupi.

Hapa kwenye mahojiano machozi yalinitoka kwa kucheka.

Prof. Malima alijaaliwa kipaji cha kuchekesha.

Hakukaa akiwa wima alimuaga mtani wake Jaji.

Jaji akamuuliza Prof, ‘’Husubiri matokeo?’’

Prof. Malima aliniambia alipigwa na mshangao mkubwa.

Central Committee iliwapitisha - Kikwete, Mkapa na Msuya kuwa majina yatakayokwenda mbele kwa uchaguzi wa jina moja la mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM.

Taarifa zinasema Jaji Mark Bomani aliumia sana kwa kukatwa jina lake.

Prof. Malima yeye njia nzima wakati anarudi Dar es Salaam ni kuwa kila akikumbuka aliyoyaona Dodoma yeye ilikuwa ni kucheka tu kwani yale yalimkumbusha yaliyomfika Chimwaga mwaka wa 1992 pale alipofanyiwa njama asichaguliwe NEC iliyokuwa na viti 20.

Huwezi kuchoka kumsikiliza Prof. Malima kwani alikuwa anajua mengi sana na akiyaeleza kwa namna ambayo ingawa mengi ni ya kusikitisha atakuacha taaban kwa kucheka.
Dah wakati mwingine mnatulisha matango poli nyie wazee,kikeete na malima walikuwa wamejiandaa kwa kiwango cha juu sn cha kuutafuta urais,sio km unavyoyaka kutudanganya mzee mohamed kuwa waliingia kwa sbbu ya gazeti kusema ikulu waiogopa waislamu,na kikwete na kighoma hawakuwa waislamu pekee waliotia nia kugombea urais 1995,
Lkn pia baada ya malima kuwa ameukosa urais ccm,alihusishwa na chama furani kilichokuwa na misimamo na itikadi ya kiislamu
 
Ndg hawezi kuandika makala bila kuhusisha uislam,huyu jamaa na ajenda zake za kidini bhana, kuna muda anaandika vitu unafurahia ila udini alionao unakera
Mohaned said hana lolote,ni ablakadabla,kuna kachama fuani walihusishwa nako 1995 pamoja na akina malima
 
kwa hiyo jakaya alianza kushindana na mwinyi mda mrefu.umenichanganya
 
Red Label,
Kuna Professor wa African Studies katika siku tulipokutana alifurahi sana.

Akaniomba nihame hoteli twende nyumbani kwake.

Tulikuwa baada ya chakula cha usiku tunazungumza hadi usiku wa manane.

Anasema kama asingesoma kitabu cha Abdul Sykes asingejua kuwa Tanganyika kulikuwa na Waislam na hawa Waislam wamefanya makubwa katika kupigania uhuru.

Akanambia amefanya kazi AU Addis Ababa na Abuja na katika shughuli zake za kazi ametembelea balozi nyingi za Afrika duniani na kitu kilichomshangaza balozi za Tanzania Ulaya, Afrika na Asia hakuwahi kukuta maofisa Waislam.

Ikampitikia kuwa huenda Tanzania ni nchi ya Kikristo.

Alipokisoma kitabu cha Abdul Sykes ndipo akapata jibu.

Red Label haya aliyoona huyu profesa ndiyo udini.

Udini ni kwa wafuasi wa dini moja kuhodhi kila fursa katika nchi na kuwaweka wengine pembeni.

Udini si kuandika historia ya Waislam.

Hivi ushajiuliza kwa nini historia ya TANU na uhuru na Tanganyika ilipoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni (1981) ilipotoshwa pakubwa?

Nakuomba unapotaka kunitaja kwa jina usiniite Muddy tumia jina langu Mohamed.
Mzee mohamed wewe na udini,udini na wewe,hutufai wewe,kila jambo ni kulalamika tu,
 
Back
Top Bottom