RC Gambo, vigogo CCM Arusha waitisha kikao cha siri kupanga mbinu chafu

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
87
280
Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Arusha wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo wamefanya kikao cha siri chenye lengo la kupanga mbinu za kuwathibiti wagombea ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.

Viongozi waliotajwa kushiriki kikao hicho ni pamoja na mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Arusha, Zelothe Stephen,katibu wa Ccm ,Musa Matoroka,katibu mwenezi wa Ccm wilaya ya Arusha, Abraham Mollel sanjari na mtumishi mmoja wa ngazi za juu katika ofisi ya halmashauri ya jiji la Arusha ambaye jina lake bado halijafahamika.

Wengine ni pamoja na katibu mwenezi wa Ccm wilayani Arusha,Abraham Mollel sanjari na mwenyekiti wa Ccm wilayani Arusha,Richard Masawe.

Viongozi hao wakiongozwa na Gambo wanadaiwa kukutana Jana majira ya saa mbili usiku ambapo walifanya kikao hicho kilichomaliza majira ya saa nne usiku katika hoteli ya Moshono Lounge iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha.

Chanzo cha habari katika eneo hilo kimeeleza kwamba lengo la kikao hicho lilikuwa ni kupanga mikakati ya kuwachafua baadhi ya wagombea ubunge walioonyesha nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa mkakati mwingine ulioelezwa kupangwa ndani ya kikao hicho ni pamoja na kuyawekea vikwazo majina ya wagombea hao kwenye kamati ya siasa ngazi na wilaya na mkoa.

Hatahivyo,taarifa hizo zinakuja zikiwa ni siku chache baada ya uongozi wa Ccm mkoa wa Arusha kuwaita makatibu wa Uvccm ngazi ya kata wilayani Arusha kwa lengo la kunusuru mpasuko ulioibuka ndani ya chama hicho.

Makatibu hao waliitwa na mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Arusha (Zelothe) hivi karibuni huku akiwaangukia na kuwaomba wawatulize vijana wa jumuiya hiyo ambao wamekuwa na mgogoro na mkuu wa mkoa wa Arusha, Gambo.

Mbali na viongozi hao pia viongozi wa Uwt ngazi ya kata na wilaya waliitwa mbele ya chama hicho kama njia mojawapo ya kuwasihi wamalize tofauti baina yao na Gambo.

Hivi karibuni Gambo aliamuru kukamatwa na kada maarufu wa chama hicho,Bernard Kassano maarufu kama Trump baada ya kudaiwa kumtolea maneno makali kupitia mitandao ya kijamii .

Hatahivyo, kada huyo alishikiliwa kwa siku 9 na jeshi la polisi mkoani Arusha kabla ya kuachiwa kwa dhamana jambo ambalo lilipelekea vijana na wanachama wa Ccm kumtuhumu Gambo kusababisha mpasuko ndani ya Ccm mkoa wa Arusha.

Mwisho.

IMG_20200417_170437_286.JPG
IMG_20200417_170341_408.JPG
IMG_20200417_170502_906.JPG
IMG_20200417_170410_954.JPG
IMG_20200417_165840_218.JPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnaweweseeka, mnamchafua Gambo, mbona hata hajatangaza Nia? Mna waswas na kazi alizofanya. Na kiukweli ameisimamia vyema ilani ya chama Cha mapinduzi.

Na kuhusu huyo Trump hata Kama ni kada wa CCM hakuna aliye juu ya Sheria, Kama katenda kosa mnayaka aachwe? Kumbukeni CCM Kuna demokrasia lakini pia Sheria za nchi zinafatwa.

Kusema kwamba eti Gambo kaamuru Trump akamatwe ni nonsense, si kwa serkali hii ya Magu.

Acheni majungu, mwacheni jembe na viongozi wa chama wapige kazi. Tenaa mkumbuke kwa nafasi ya Gambo automatically anaingia kwenye kamati ya siasa ya chama.

KUMBUKA CORONA IPO, TUNAWE MIKONO KWA MAJI TIRIRISHI NA SABUNI NA TUFATE USHAURI WOTE TUNAOPEWA NA WATAALAM WETU WA AFYA.

Hivi kuwekwa mahabusu magereza siku 8 si kukamatwa? Tena bila kosa!!! ccm hoyee
 
Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Arusha wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo wamefanya kikao cha siri chenye lengo la kupanga mbinu za kuwathibiti wagombea ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.

Viongozi waliotajwa kushiriki kikao hicho ni pamoja na mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Arusha, Zelothe Stephen,katibu wa Ccm ,Musa Matoroka,katibu mwenezi wa Ccm wilaya ya Arusha, Abraham Mollel sanjari na mtumishi mmoja wa ngazi za juu katika ofisi ya halmashauri ya jiji la Arusha ambaye jina lake bado halijafahamika.

Wengine ni pamoja na katibu mwenezi wa Ccm wilayani Arusha,Abraham Mollel sanjari na mwenyekiti wa Ccm wilayani Arusha,Richard Masawe.

Viongozi hao wakiongozwa na Gambo wanadaiwa kukutana Jana majira ya saa mbili usiku ambapo walifanya kikao hicho kilichomaliza majira ya saa nne usiku katika hoteli ya Moshono Lounge iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha.

Chanzo cha habari katika eneo hilo kimeeleza kwamba lengo la kikao hicho lilikuwa ni kupanga mikakati ya kuwachafua baadhi ya wagombea ubunge walioonyesha nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa mkakati mwingine ulioelezwa kupangwa ndani ya kikao hicho ni pamoja na kuyawekea vikwazo majina ya wagombea hao kwenye kamati ya siasa ngazi na wilaya na mkoa.

Hatahivyo,taarifa hizo zinakuja zikiwa ni siku chache baada ya uongozi wa Ccm mkoa wa Arusha kuwaita makatibu wa Uvccm ngazi ya kata wilayani Arusha kwa lengo la kunusuru mpasuko ulioibuka ndani ya chama hicho.

Makatibu hao waliitwa na mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Arusha (Zelothe) hivi karibuni huku akiwaangukia na kuwaomba wawatulize vijana wa jumuiya hiyo ambao wamekuwa na mgogoro na mkuu wa mkoa wa Arusha, Gambo.

Mbali na viongozi hao pia viongozi wa Uwt ngazi ya kata na wilaya waliitwa mbele ya chama hicho kama njia mojawapo ya kuwasihi wamalize tofauti baina yao na Gambo.

Hivi karibuni Gambo aliamuru kukamatwa na kada maarufu wa chama hicho,Bernard Kassano maarufu kama Trump baada ya kudaiwa kumtolea maneno makali kupitia mitandao ya kijamii .

Hatahivyo, kada huyo alishikiliwa kwa siku 9 na jeshi la polisi mkoani Arusha kabla ya kuachiwa kwa dhamana jambo ambalo lilipelekea vijana na wanachama wa Ccm kumtuhumu Gambo kusababisha mpasuko ndani ya Ccm mkoa wa Arusha.

Mwisho.

View attachment 1421800View attachment 1421801View attachment 1421802View attachment 1421803View attachment 1421804

Sent using Jamii Forums mobile app
mbona wote wana sura za kijambazi?
 
Back
Top Bottom