Siri za kikao za Prof. Mkumbo zavuja kutaka ubunge wa Iramba

Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,891
1,211
Wiki mbili zilizopita Katibu mkuu wa Wizara ya Maji ilisemekana aliitisha kikao cha kuwarubuni wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutangaza nia mapema ya kugombea ubunge lakini Prof Mkumbo alikana kwa kutohusika na hili jambo na kuwahakikishia umma kuwa ilikuwa ni namna mojawapo ya kumchafua kisiasa. Je leo atapinga hiyo siyo sauti yake?

Leo kikao chao walichofanya kimevuja ambapo ilikuwa *tarehe 7 April 2020 akiwa na baadhi ya wajumbe 70 wa Mkutano mkuu wa CCM wilaya*.
Labda kwa kumsaidia vizuri apitie Kanuni za Uongozi na maadili ya CCM Toleo la 2017 aya ya 6 kifungu cha 1 kipengele cha ¡ hadi ¡¡¡ pamoja na kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya dola kanuni ya 26 kifungu cha 5 na 6.

Kikao chake cha siri kilijikita kwenye kutangaza nia mapema ilihali chama cha mapinduzi hakijaruhusu wanachama kutangaza nia ya kugombea nafasi yeyote.

Licha ya kutangaza nia aliahidi baadhi ya sera atakazozifanyia kazi baada ya kuchagiliwa kama sekta ya miundombinu, ajira kwa vijana na kuwaletea wananchi maji ambayo kasisitiza ni kero ya kudumu na yeye ni muarobaini.

Kupitia wadhifa wake wa ukatibu amekuwa akiwaaminisha wananchi kuwa yeye ndio anayetoa maji vilevile na kuwaaminisha kuwa yeye kila jambo linawezekana ndio maana akawa mteule wa Rais .

Akawaeleza sera za kugombea ubunge ni kujua kusoma na kuandika lakini yeye kapitiliza vigezo maana ni Profesa na amefundisha chuo kikuu kwa muda mrefu.

Kingine hakuacha kumsema hasimu wake ambaye ni Dr Mwigulu kuwa alitumia milioni 147 kuandika kwenye mawe kwa kutaka urais ukiwa ni utumiaji vibaya wa pesa wakati kwenye jimbo hajafanya chochote. Wakati sisi wananchi ndio tunajua Mwigulu katukuta wapi na sasa tuko wapi?. Hakuishia hapo akasema ubunge ukomo ni miaka 10 hii kaitolea wapi?.

Ninapata ukakasi na mkasi ya Prof Mkumbo kutaka ubunge kwa nguvu nyingi. Nafasi ya ukatibu mkuu ni nafasi muhimu na ni ya utekelezaji zaidi kuliko kufanya siasa. Ndio maana tunaona sasa anatumia nguvu kubwa kutafuta ubunge wakati tulitegemea aitendee kazi nafasi yake ya ukatibu mkuu wa wizara nyeti ya maji.

Ninapata maswali mengi huenda anatangaza nia mapema ya kugombea ubunge kwa sababu bado ana ugeni na chama maana Katibu alitoa ilani watu watangaze nia mpaka watakapotangaziwa. Kama siyo hilo basi Prof Mkumbo akili yake na mawazo yake ni kutaka ubunge wa Iramba magharibi ndio maana ikapelekea hadi wizara yake ikapata kasoro kwenye report za CAG.

Ndugu zangu wana Iramba kipindi hiki tunaweza kudanganywa na nyimbo nzuri na ahadi kedekede kwa watu wageni wenye ulafi wa ubunge. Naamini wote tunakiunga chama chetu kwa juhudi wanazozifanya hivyo yatupasa kuwa makini na watu wanaokuja kwa sura tofauti za kutulaghai.

Hili jimbo kwa miaka 10 limekuwa chini ya Dr Mwigulu na tumeona mambo mengi aliyoyafanya na yale ambayo hajayafanya. Hivyo tusubiri wakati ufike na sisi kama wananchi tunaamini chama hakitakuwa tayari kutupatia mgombea ambaye hakubaliki na jamii ya wana Iramba.

Rushwa ni adui wa haki hatutakubali kuruhusu watu wanaotumia nguvu nyingi kuutaka ubunge. *Naomba sisi kama wananchi na wanaCCM tuna imani na chama hakitakuwa tayari kuchafuliwa na kuharibiwa sifa nzuri iliyonayo kwa kutupatia mgombea wa ovyo ambaye hafuati taratibu, kanuni na sheria za chama. Tuheshimu sheria na kanuni za chama chetu*.

Mungu mbariki Rais wetu pamoja na wasaidizi wake vilevile tunawapongeza kwa namna wanavyopambana kuongoza taifa letu. Na tuendelee kuepushwa na corona ambayo limekuwa janga la dunia na tuendelee kujipa tahadhari zaidi tunazopewa na wataalamu na viongozi wetu.

Mimi wako
Kiboko.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_20200411-223717_1586633879491.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku mtaani mbona tunaishi tu kwa kupiga mishe mishe za hapa na pale?? Wengine njooni tu tujiajili huku sio lazima muwe Wabunge..

Mwigulu umeshakua mbunge kwa zaidi ya miaka kumi sasa, ni vyema ukaonyesha mfano kwa kujiajili kama wengine huku mtaani tena...
 
Back
Top Bottom