Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Kufuatia kikao cha hivi karibuni baina ya Mheshimiwa Rais John Magufuli na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Lowassa, kinachofuatia sasa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi hawa wawili.
Ikumbukwe kwamba miongoni mwa hoja ambazo Mheshimiwa Lowassa alizibeba kwenda kuziwasilisha kwa Mheshimiwa Rais kwa niaba ya ukawa, pia lilikuwepo suala la ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea nchini.
Kwa mfano, katika mazungumzo yake na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Lowassa alimueleza Mh Rais juu ya kasoro nyingi zilizojitokeza kwenye chaguzi ndogo za udiwani katika kata 43 zilizomalizika hivi karibuni ambapo ukawa uliwasilisha rasmi kwa tume ya uchaguzi malalamiko yake dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa demokrasia vilivyojitokeza. Mheshimiwa Rais alimuahidi Mheshimiwa Lowassa kulishughulikia ili kuhakikisha kwamba suala la demokrasia ya vyama vingi linatekelezwa kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Kufuatia ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais, baadae Mheshimiwa Lowassa aliwasilisha taarifa hiyo kwa Kamati Kuu ya Chadema pamoja na mengine yaliyojiri katika kikao chake na Mheshimiwa Rais, ikulu Dar es salaam. Kufuatia hatua hiyo, Kamati Kuu ya Chadema kwa kauli moja imeridhia uamuzi wa Chama kusimamisha wagombea wake katika chaguzi ndogo za ubunge kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao kwa imani kwamba ahadi za Mheshimiwa Rais kwa Mheshimiwa Lowassa zitatekelezwa na vyombo husika.
Wana ukawa pamoja na wapenda demokrasia kwa ujumla wanaombwa kuwa watulivu na wenye subira katika kipindi hiki kuelekea tarehe ya chaguzi ndogo za ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha.