Kikao cha Magufuli na Lowassa chailainisha CHADEMA kutia mguu Kinondoni na Siha

Huu ni ushahidi wa wazi kuwa chadema ni wazushi na vigeugeu.
Ni ngumu sana kuwaamini kwa kauli na matamko yao
Mlichosikia ndicho size yenu mengine waachieni UKAWA kama Lowassa alitumwa au hakutumwa.
 
Labda wewe ndiye huna habari kuwa hilo limefanyika mara nyingi
Halijawahi kufanyika kailima amesema hivyo lkn hata mbowe amesema hakufanya hivyo kwa sababu anajua hawatachukua hatua yoyote kwa sab wanaipendelea ccm na akatoa mashart mtandaoni kuwa wawaite wajadili yaliyotokea la sivyo hawatashiriki uchaguzi kailima akajibu mitandaoni kama wao kuwa wana haki ya kususia lkn kwa kawaida barua nyingi au ripoti za kichama (chadema) husambazwa kwa wafuasi wake kupitia media n.k je umewahi kuona ripoti yoyote rasmi iliyosainiwa na viongozi wa chama inayolalamikia swala hilo kwenda tume? Walichofanya chadema ni kuripoti matukio ya walioshambuliwa polisi tu, picha za majeruhi na rb za reference zilitumwa mitandaoni.
 
Ukawa ulishampa Lowassa hoja za kuwasilisha kwa Rais magufuli kwa niaba yake kwa Muda mrefu na maombi ya appointment kuwasilishwa ikulu accordingly. Kilichotokea ni kwamba ikulu ilikaa kimya kwa Muda mrefu na kumuita Lowassa ghafla siku husika.
Kwaiyo Lema alivyomshambulia Lowassa alivyotoka tu ikulu alikuwa hajui kama alitumwa na Ukawa?
 
*Taarifa kwa Umma*

Kufuatia kikao cha hivi karibuni baina ya Mheshimiwa Rais John Magufuli na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Lowassa, kinachofuatia sasa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi hawa wawili.

Ikumbukwe kwamba miongoni mwa hoja ambazo Mheshimiwa Lowassa alizibeba kwenda kuziwasilisha kwa Mheshimiwa Rais kwa niaba ya ukawa, pia lilikuwepo suala la ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea nchini.

Kwa mfano, katika mazungumzo yake na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Lowassa alimueleza Mh Rais juu ya kasoro nyingi zilizojitokeza kwenye chaguzi ndogo za udiwani katika kata 43 zilizomalizika hivi karibuni ambapo ukawa uliwasilisha rasmi kwa tume ya uchaguzi malalamiko yake dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa demokrasia vilivyojitokeza. Mheshimiwa Rais alimuahidi Mheshimiwa Lowassa kulishughulikia ili kuhakikisha kwamba suala la demokrasia ya vyama vingi linatekelezwa kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Kufuatia ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais, baadae Mheshimiwa Lowassa aliwasilisha taarifa hiyo kwa Kamati Kuu ya Chadema pamoja na mengine yaliyojiri katika kikao chake na Mheshimiwa Rais, ikulu Dar es salaam. Kufuatia hatua hiyo, Kamati Kuu ya Chadema kwa kauli moja imeridhia uamuzi wa Chama kusimamisha wagombea wake katika chaguzi ndogo za ubunge kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao kwa imani kwamba ahadi za Mheshimiwa Rais kwa Mheshimiwa Lowassa zitatekelezwa na vyombo husika.

Wana ukawa pamoja na wapenda demokrasia kwa ujumla wanaombwa kuwa watulivu na wenye subira katika kipindi hiki kuelekea tarehe ya chaguzi ndogo za ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha.
Kwani si tuliambiwa alienda ikulu bila Mwenyekiti kuwa na taarifa kwa hyo hizo agenda alienda nazo yeye binafsi haa haa haa
 
Inashangaza kuona watu wanatetea wanachokifanya viongozi wa Chadema
Lowassa ni sumu mbona mnakuwa wagumu kuelewa???
Mbowe na chama chako acheni kuwatania wananchi
 
Back
Top Bottom