Kikao cha Magufuli na Lowassa chailainisha CHADEMA kutia mguu Kinondoni na Siha

*Taarifa kwa Umma*

Kufuatia kikao cha hivi karibuni baina ya Mheshimiwa Rais John Magufuli na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Lowassa, kinachofuatia sasa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi hawa wawili.

Ikumbukwe kwamba miongoni mwa hoja ambazo Mheshimiwa Lowassa alizibeba kwenda kuziwasilisha kwa Mheshimiwa Rais kwa niaba ya ukawa, pia lilikuwepo suala la ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea nchini.

Kwa mfano, katika mazungumzo yake na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Lowassa alimueleza Mh Rais juu ya kasoro nyingi zilizojitokeza kwenye chaguzi ndogo za udiwani katika kata 43 zilizomalizika hivi karibuni ambapo ukawa uliwasilisha rasmi kwa tume ya uchaguzi malalamiko yake dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa demokrasia vilivyojitokeza. Mheshimiwa Rais alimuahidi Mheshimiwa Lowassa kulishughulikia ili kuhakikisha kwamba suala la demokrasia ya vyama vingi linatekelezwa kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Kufuatia ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais, baadae Mheshimiwa Lowassa aliwasilisha taarifa hiyo kwa Kamati Kuu ya Chadema pamoja na mengine yaliyojiri katika kikao chake na Mheshimiwa Rais, ikulu Dar es salaam. Kufuatia hatua hiyo, Kamati Kuu ya Chadema kwa kauli moja imeridhia uamuzi wa Chama kusimamisha wagombea wake katika chaguzi ndogo za ubunge kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao kwa imani kwamba ahadi za Mheshimiwa Rais kwa Mheshimiwa Lowassa zitatekelezwa na vyombo husika.

Wana ukawa pamoja na wapenda demokrasia kwa ujumla wanaombwa kuwa watulivu na wenye subira katika kipindi hiki kuelekea tarehe ya chaguzi ndogo za ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha.
Usitulishe maneno ambayo Lowassa hakuyasema. Kwa nini Huwa mnapenda sana kupindisha maneno nyie bavicha?
 
Kijana usije kulisha watu taarifa potofu. Ukumbuke una legacy nzuri tu humu JF. Maana Ugonjwa wa uteuzi unawamaliza vijana wengi sana kiasi cha kuweka bondi akili zao.

Subiri irukwe na akina Polepole ndiyo tutajua niyakupikwa au kuna ukweli! Ila hizi chenga za kimesi mesi mwisho wa siku kuna kundi litasababisha penalti!
 
Mchambuzi umejijengea sifa kubwa sana humu miaka mingi lakini umekuwa very compromised hadi ni kama unashindwa kujenga hoja kwa uhuru kama zamani. Acha kupigania vyama mzee tumia kichwa chako kunyoosha siasa zetu bila kujali itikadi na miaka mingi uliheshimika kwa hilo.
Ajabu Ni kwamba chadema walimshambulia Mzee Lowassa kwa kwenda Ikulu bila kuwashirkisha. Mbowe akatamka bayana kuwa Lowassa alienda Ikulu kwa sababu zake binafsi Na kuwa aliyoyaongea Ni msimamo wake binafsi Na siyo chama. Lema Na Lissu wakambwatukia Lowassa. Leo hii tunaambiwa eti alienda akiwa Na Baraka za ukawa kuwasilisha hoja zao. Wakiitwa nyumbu wanakasirika!
 
Hapa kuna kitu haliko sawa unless kama tutatakiwa kulimeza kama zilivyo.
Mchambuzi hebu nieleweshe hapa

1) lowassa kaenda ikulu, peke yake, hakukua na muwakilsh mwingine je tutakuwa na hakika ipi kwamba yaliongelewa masuala ya demokrasia na sio ya familia?

2) kwann chadema walitoa kauli kinzani juu ya Lowassa kwenda ikulu. Huku viongozi wakilaan na baadae kamati kuu ikaja kmsafisha Lowassa,?

3) kwann kwenye taarifa ya ikulu hakuna kulipoongelea maswala haya ya nini hasa kilichompeleka Lowassa ikulu?

4) kwann lowassa aseme aliitwa kwenda kushawishiwa kurudi CCM na kwenye press release yake hakulisemea hili la demokrasia?
 
Ajabu Ni kwamba chadema walimshambulia Mzee Lowassa kwa kwenda Ikulu bila kuwashirkisha. Mbowe akatamka bayana kuwa Lowassa alienda Ikulu kwa sababu zake binafsi Na kuwa aliyoyaongea Ni msimamo wake binafsi Na siyo chama. Lema Na Lissu wakambwatukia Lowassa. Leo hii tunaambiwa eti alienda akiwa Na Baraka za ukawa kuwasilisha hoja zao. Wakiitwa nyumbu wanakasirika!
Wengine tunakosa hata cha kusema. Viongozi wakubwa wote walitoa matamko baada tu ya kusikia lowasa alikuwa ikulu ....nukuu zipo alafu zinakuja hadithi za ajabu!! Huu uzi hata kama utaboreshwa lakini tayari watu wamenukuu ....aibu tupu kwa chama tulichokiona kama mbadala halisi kwa CCM ....Chadema safisheni hiyo nyumba yenu kabla hamjavuliwa nguo zaidi ....badala ya kutuona sisi wakosoaji ni wabaya mtusaidie tukinyooshe hiki chama ili tufikie malengo ya kuitoa CCM madarakani. Chadema ya sasa imebinafsishwa na hizi sarakasi ni kielelezo kikuu. Acheni kuwalea wapinzani hawatobadilika zaidi ya kufurahia ruzuku.
 
Naona hapa CDM wamepigwa chenga ya mwili.Sidhani kama kuna makubaliano yeyote yatakayotekelezwa.Hapa wameingizwa tu kwenye uchaguzi ili ionekane Demokrasia ipo lkn hakuna jipya.Jinsi uchaguzi mdogo ulivyokuwa na huu utakuwa hivyo hivyo
 
Kwa hiyo alienda bila ya nyinyi kuwa na taarifa. Halaf mkamuita ajieleze. Akayasema hayo, basi mkamshukuru kafanya jambo zuri. Kwa nini hakuwataarifu kama lilikuwa ni suala hilo, mpaka mka-panic? Ataendelea kuwapoteza.
 
Ajabu Ni kwamba chadema walimshambulia Mzee Lowassa kwa kwenda Ikulu bila kuwashirkisha. Mbowe akatamka bayana kuwa Lowassa alienda Ikulu kwa sababu zake binafsi Na kuwa aliyoyaongea Ni msimamo wake binafsi Na siyo chama. Lema Na Lissu wakambwatukia Lowassa. Leo hii tunaambiwa eti alienda akiwa Na Baraka za ukawa kuwasilisha hoja zao. Wakiitwa nyumbu wanakasirika!
Wewe ndio ulielewa hivyo wenye akili zao waliisoma statement ya Mbowe between the lines.
 
Wengine tunakosa hata cha kusema. Viongozi wakubwa wote walitoa matamko baada tu ya kusikia lowasa alikuwa ikulu ....nukuu zipo alafu zinakuja hadithi za ajabu!! Huu uzi hata kama utaboreshwa lakini tayari watu wamenukuu ....aibu tupu kwa chama tulichokiona kama mbadala halisi kwa CCM ....Chadema safisheni hiyo nyumba yenu kabla hamjavuliwa nguo zaidi ....badala ya kutuona sisi wakosoaji ni wabaya mtusaidie tukinyooshe hiki chama ili tufikie malengo ya kuitoa CCM madarakani. Chadema ya sasa imebinafsishwa na hizi sarakasi ni kielelezo kikuu. Acheni kuwalea wapinzani hawatobadilika zaidi ya kufurahia ruzuku.
Polepole aliutangazia umma trh 18 jana kuwa kuna viongozi 20 wa Chadema watahamia CCM na nukuu zipo halafu zinakuja hadithi za ajabu ajabu. Hahahaa
FB_IMG_1511331350206.jpg
 
Ukawa ulishampa Lowassa hoja za kuwasilisha kwa Rais magufuli kwa niaba yake kwa Muda mrefu na maombi ya appointment kuwasilishwa ikulu accordingly. Kilichotokea ni kwamba ikulu ilikaa kimya kwa Muda mrefu na kumuita Lowassa ghafla siku husika.

Kuna kitu hapa sijaelewa...Unapozungumzia UKAWA unamaanisha Chadema? Yani kamati kuu ya chadema imekubaliana na Lowassa kwa niaba ya ukawa?
 
Polepole aliutangazia umma trh 18 jana kuwa kuna viongozi 20 wa Chadema watahamia CCM na nukuu zipo halafu zinakuja hadithi za ajabu ajabu. HahahaaView attachment 679530
Mkuu hapa tunajadili Chama ambacho tulitegemea sasa hivi ndio kiwe dira ya siasa zetu na si hayo mambo ya CCM. Kama hata wewe huoni tatizo basi tusubiri miujiza kuwabadili fikra viongozi wenu!!
 
Ukawa ulishampa Lowassa hoja za kuwasilisha kwa Rais magufuli kwa niaba yake kwa Muda mrefu na maombi ya appointment kuwasilishwa ikulu accordingly. Kilichotokea ni kwamba ikulu ilikaa kimya kwa Muda mrefu na kumuita Lowassa ghafla siku husika.

Kama ndivyo mbona walimtuhumu hadharani kuwa hakwenda kuwakilisha Chama na yale walikuwa mawazo binafsi hadi kuitishwa kwa kikao cha dharura cha KK.
Wajipange vizuri mambo yatawezekana.
 
Back
Top Bottom