Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kumbuka hata Marekani ilimtumia gaidi Osama Bin Laden kuisambaratisha Urusi. Iwapo Lowassa ana uwezo wa kuisambaratisha CCM ni lazima CDM wamtumie! Lengo ni kuing'oa CCM madarakani! Siasa ni strategy na hii ni fursa nzuri ya CCM kufa hata kama ni kwa mbinu chafu! Mengine baadae!!
 
Hivi dr. Slaa na tundu lisu wamo kweli kwenye vikao hivyo? Lini gamba limekuwa kiwiliwili na lini fisadi limekuwa fukara hadi chadema/ukawa ikawa mtaji kwao?
 
Cdm fuatilien kisa cha mrema vyema mtajua kuwa nssr mageuza walikufa kabisa, na kama c fadhir za mkulu leo mbatia asingekuwa na chama..

Anyway ni kwel upinzani wa kwel utatoka ssm, bt si kwa edo, maana ni sawa na kuhamisha uchafu kutoka nyumba ya jiran uliokuwa nje ukauweka seblen kwako kisha kuweka mapambo mazr na kupiga pafum, kumbuka pafum ikiisha tu uchafu unatoa harufu

Hvyo kuwen makin na edo mnakwenda kukiua chama.. na kwa taarifa ccm haishindwi na ukawa wala na edo, may b uasi wa kweli ufanyike ila si wa kumfuata mtu ambae ni mwizi na fisadi wa kutupwa, hata mtt mdogo anajua hvyo..
 
Kila mbinu inaitajika kuikomboa Tanzania kutoka kwa ccm sasa unaangalia nani anayeweza kukusaidia katika vita yako ili ufanikishe lengo la kumpoteza adui yako katika wakati huu Wa kuitoa ccm madarakani yoyote anaitajika kwa sababu ccm ndio chama kilichokuwa kabla ya mfumo Wa vyama vingi kwa hiyo yoyote yule anaweza kuwa mswada kuitoa ccm
 
Mbowe ni kichwa sana namkubali sana kwa mipango na mbinu ni mtu wa level nyingine.
 
Furaha yangu ni kuona sisiem nayo inapumzika, tuona ukawa wanajipya gani
 
Hio kura yako haimake a difference...so we dont care
Si mlijidai.mnazuia mafuriko kwa mikono zuieni.sasa

Furiko gani CDM ni chama cha mafisadi?? Mbowe kapewa 10bil, na kila mbunge atapata 20mil toka Kwa edo. Mbona CCM ni sherehe tu sasa hivi. Upande wa ubunge mi niko UKAWA, ila Kwa rais ni DR wa ukweli
 
soma alama za nyakati mahitaji ya sasa ni nini? then utajua mbowe yupo sahihi ama lah, binafsi nampongeza toka bob makani marehemu amemkabidhi chama jamaa amepambana sana mpaka leo chadema ina taswira kubwa kwenye jamii
 
"Hatukujiunga na CHADEMA eti kwa sababu ulituahidi kazi, hapana tulijiunga na CHADEMA wakati mgumu kwa nchi yetu. Tulijiunga kwa kuwa tulitaka kuwa sehemu ya mapambano dhidi Rushwa, Ufisadi na Mafisadi.

Tuliingia CHADEMA kwa sababu tuliamini kile ambacho CHADEMA ilikisimamia na kukipigania, ndiyo maana tukawa sehemu ya mapambano.

Wewe Freeman Mbowe si sehemu ya Mapambo kwani umesharuhusu watu ambao tuliaminishwa kuwa ni mafisadi kuingia katika chama ambacho ndicho kilikuwa kimbilio la wananchi.

Wewe kaa na CHADEMA LOWASA yako Mimi nitabaki kuwa CHADEMA ASILIA.

Ni mimi mwana CHADEMA ASILIA

Mkuu Mwanga,
Heshima juu. Naomba unisaidie mambo yafuatayo kabla sijakujibu maswali yako.
1. Unajua msingi mkuu ama chanzo kikuu cha ufisadi?.

2. Unajua makusudi ya kuanzishwa kwa UKAWA?, na nini kinawaunganisha?.

Kama unaweza kunipa majibu ya haya maswali mawili kwa ufasaha na weledi, nadhani bandiko lako litakuwa halina mashiko sana
 
Furiko gani CDM ni chama cha mafisadi?? Mbowe kapewa 10bil, na kila mbunge atapata 20mil toka Kwa edo. Mbona CCM ni sherehe tu sasa hivi. Upande wa ubunge mi niko UKAWA, ila Kwa rais ni DR wa ukweli

Utapoteza kura yako bure
 
hivi mnajua garama alizotumia muamerika kupambana na Osama? je chadema wako tayari ku-incur hizo gharama? sidhani kama mfano wako ni relevant.
 
Hivi CHADEMA haina think tankers! Lowassa kuwa mgombea kupitia CHADEMA (sio UKAWA, UKAWA haipo kisheria)!! Miaka takriban 10 waliwaamisha watanzania kuwa Lowassa ni fisadi namba moja. Lema aliwahi kusema azomewe akipita. Leo, Lowasa msafi mno.

Watanzania si wajinga kiasi hicho, watawaadhibu mchana kweupe. Mmeisaidia CCM kushinda kwa urahisi sana. Mtahangaika kumsafisha Lowassa badala ya kumwombea kura. CCM watatembea na mchapakazi Magufuli wakiomba kura wala si kumsafisha.
Aibu kwa Lipumba, aliyewatangazia watanzania kuwa Lowassa alistahili kuwa jela badala ya kuwa mtaani akiomba ridhaa ya kuingia ikulu. Leo yuko kimya, kakutana na nguvu ya pesa uso kwa uso, kageuka urojo.
 
Back
Top Bottom