Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Wadau nimefurahi sana kwa maamuzi magumu yaliyochukuliwa na viongozi wa CHADEMA na hatimaye UKAWA itakavyokuwa kwa kukubali ujio mpya wa Wana CCM wakiongozwa na mwamba wa Kaskazini Edward Lowassa.

Furaha hii ni kutokana na namna ambavyo wafuasi wa Lowassa wamekuwa wakifaidi maisha hapa Tanzania, tofauti na CHADEMA na CUF za zamani ambazo wafuasi wake wamekuwa wakiishi kwa kufunga mikanda wakati nchi yetu inarasilimali nyingi sana, uthubutu wa kutumia rasilimali nyingi hizi sasa ni ruksa kwani utajiri ambao umekuwa ukihubirinu na Lowassa sasa umepata mahali halisi pa kuuthibisha, na watu lazima wajengewe hamasi ya kuwa matajiri na siyo kukumbatia umaskini .
 
Mkuu adui wa nchi yetu sio Lowasa

Sio membe

Sio Kikwete

Sio Mwigulu

Adui yetu ni Mfumo wa CCM...Hicho tu

Failure ziko ngapi kweye uchumi wetu...Is it about Lowasa au mismanagement ya mfumo wa serikali ya CCM

I believe you are learned enough.......Our goal is to take out CCM.....Baada ya hapo ni effectivenesss ya serikali ya UKAWA kuweka uwajibikaji

Sijui kwa nini hisia zinawafanya washindwe kufikiria sawa sawa inatisha
 
Kama kweli CHADEMA kwisha kazi. Wamejipeleka kaburini huku wakiona na kutizama. Inatia huruma kwa Watanzania waliokuwa na matumaini kwa chama chao cha CHADEMA. Watakimbilia wapi??? Sitashangaa wakirudi kwa CCM ambao wameonyesha kuanza vita dhidi ya ufisadi kwa kumuengua Lowasa kwenye kugombea urais wa nchi.

Haturudi ccm kwani tumeshaona jinsi mnavyotuona wananchi wapuuzi mkishapata chenu!Sasa lazima muondoke maana nchi hii siyo yenu peke yenu

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hata Marekani ilimtumia gaidi Osama Bin Laden kuisambaratisha Urusi. Iwapo Lowassa ana uwezo wa kuisambaratisha CCM ni lazima CDM wamtumie! Lengo ni kuing'oa CCM madarakani! Siasa ni strategy na hii ni fursa nzuri ya CCM kufa hata kama ni kwa mbinu chafu!
 
Ni hivi mkakati wa kuiondoa Chama cha kikabila na kugawa watanzania kikanda ni lazima kuondoke. Walifika mbali mpaka Riziwani Jakaya Mrisho Kikwete akaandika wazi Facebook kuwa mpaka aingie kaburini hakuna rais kaskazini, Na ni waambie si kaskazini tu mkakati ni kuwa hakuna raisi kutoka kanda ya Nyanda za juu kusini hasa Mbeya na Mkoa wa Kagera, Na hii imejitokeza wazi kabisa hata katika kuteua waandamizi wa serikali. Sasa mtakula matapishi yenu. Na ufisadi wa familia hii ndiyo tutaanza nao.
 
Kaka muda ni dawa tunasubiri.Lakini nasikia mwenye nyumba yuko njiani kurudi na kesho Richmond itakuwa Kisutu.

Kaka VITA imeanza na wapiganapo Tembo NYASI ndizo ziumiazo...

sasa mkuu wakifanya hivyo ndio safi kabisa katika siasa
 
Ccm Msimlumu LOWASA aliwapa muda mwingi mngeweza kumfuata na kumaliza hasira zake. hamkufanya hivyo mmekuwa kama wanyama hata busara mlikosa. sasa leo anaondoka.......... kweli CCM haiwezi kunijali mimi
 
Lowassa akihudhuria kikao Kamati kuu CHADEMA

View attachment 271482
Waziri Mkuu Mstaafu wa JMT Mh. Edward Ngoyai Lowassa, akisalimiana na viongozi na wanachama wa CHADEMA

View attachment 271483
Waziri Mkuu Mstaafu wa JMT Mh. Edward Ngoyai Lowassa akiwa Meza Kuu na viogozi wa CHADEMA
...hakika Lowassa is an amazing drifter.....sasa naamini ccm itaondoka madarakani this time around.....hakika hata yale mauzauza ya richmond aliyokaa nayo Lowassa tangu 2008 sasa yataibuka....this is an amazing game....

.....sasa hakika naona upinzani wa kweli ukianza kutamalaki TZ....


...haya mambo ya kifisadi yametumika sana kisiasa TZ...mithili ya kutojua nani haswa wa kumshika mwenzake....na ndio maana hata ujio wa Lowassa chadema ni poa tu...nchi hii wengi ni wale wale...


....sasa naona mengi ya utawala wa JK yakiwekwa wazi na ujio wa Lowassa UKAWA...na hili ni jambo jema kwa umma wa watanzania ...kwa maana ya mbivu na mbichi kujulikana....

....Kete ya ufisadi ccm haitoweza kuwapeleka popote maana wote wameoza....hata Magufuli ana makesi tele ya kujibu akiwa kama waziri...mojawapo likiwa kuuza nyumba zetu....Hivyo hii kete ya ufisadi wala sasa itakua non issue (at least for the moment till 2015 elections)...


....Naona ule usemi wa Nyrere kuhusu upinzani wa kweli kwa ccm kutoka huko huko ccm ukiwadia sasa na hili ni jambo la kheri hakika kwa mustakabali wa taifa hili...


..Its time to remove ccm from power now.....maana wakati umewadia hakika...Haya yote yamepangwa yatokee...na yalitokea hata Kenya wakati wa kuitoa kanu madarakani....

....sasa ngoja nikawahi kadi yangu ya kupigia kura....maana better now than never....
 
Issue kubwa ni SSM iondoke madarakani kwanza mengine baadaye. Kwa kutumia mikakati yote inayowezekana tu basi. Nilifurahi sana siku ya kujiandikisha nilikuta 90% ni vijana. Kazi kubobewa ni kuwahamasisha kuwa kazi kubwa October ni kuchinja tu na si kukata. Kampeni kampeni jamani. Wenye ndugu hebu tutumie whatups na simu zote tupige kampeni tu. Tumechoka kulea umaskini hela yetu inaishia kuwalea wale serikali imewanyima fursa. Wao wanapeana uongozi na juzi eti anatakiwa membe ili eti alinde interest za familia fisadi. Mungu si athman akaangukia pua wa mwisho katika 5 with 120 votes. Aibu hii sasa ikamilishwe October.
 
Wakuu,

Nimepitia video ya Mwl. Nyerere akizungumzia kukatwa Lowassa na CC mwaka 1995.

Nyerere, alibainisha kwamba Lowassa amekatwa kwa hoja na sababu za msingi zilizoletwa na wajumbe. Na ikumbukwe Kingunge naye alikuwepo kwenye jopo la wakataji 1995.

Sasa kwa kuwa huyu mtu alionekana hana sifa toka 1995 za kuwa rais. Sasa alitegemea atapata?

Ni hayo tu.
Naomba nikuulize tu je kwa maoni ya Nyerere Kikwete alikuwa ana sifa za kuwa Rais? mbona amepewa huo Urais.
Pia ni vema ukakumbuka kauli hizi za Nyerere
1. Kiongozi Bora na mpinzani wa kweli atatoka ndani ya CCM
2. Wananchi wanahitaji mabadiriko kama wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM
 
Kweli chadema/ukawa mmenichanganya, hivi mhe. Tundu lisu yupo kweli? Mbona magamba na mafisadi ndiyo lulu chadema/ukawa? Hivi mmeandaa uongo gani tena kwetu wananchi?
 
Kweli Nyerere late Father of the National ni only Prophet. Alisema upinzani wa kweli utatoka CCM pale itakapopasuka vipandevipande
 
"Hatukujiunga na CHADEMA eti kwa sababu ulituahidi kazi, hapana tulijiunga na CHADEMA wakati mgumu kwa nchi yetu. Tulijiunga kwa kuwa tulitaka kuwa sehemu ya mapambano dhidi Rushwa, Ufisadi na Mafisadi.

Tuliingia CHADEMA kwa sababu tuliamini kile ambacho CHADEMA ilikisimamia na kukipigania, ndiyo maana tukawa sehemu ya mapambano.

Wewe Freeman Mbowe si sehemu ya Mapambo kwani umesharuhusu watu ambao tuliaminishwa kuwa ni mafisadi kuingia katika chama ambacho ndicho kilikuwa kimbilio la wananchi.

Wewe kaa na CHADEMA LOWASA yako Mimi nitabaki kuwa CHADEMA ASILIA.

Ni mimi mwana CHADEMA ASILIA
 
Back
Top Bottom