Kikao cha CCM ikulu ya Dodoma muda huu kupitia mapendekezo ya PAC

Kikao cha CCM ikulu ya Dodoma muda huu kupitia mapendekezo ya PAC

Vijana wetu wamekosa mikopo vyuo vikuu,lakini pesa zimeshikwa na watu wachache na tunawaonea aibu.
ndio maana huwa napenda sana sheria za uchina,haya tuyaonayo Tanzania hayawezi tokea uchina na hata kama yakitokea wahusika hawawezi pewa nafasi ya kutembea ktk hii dunia

KAribu sana mkuu....Ndiyo maana nasema sisi tuende mbali ya Uchina...kutokana na ukubwa wa tatizo wahusika wakamatwe, washitakiwe , wafiliziwe, na kisha wachomwe sindano ya 'theodani' wapumzike. haya yafanyike ndani ya siku mbili. Nimelazimika kweli kusema haya kutokana na uchungu nilionao.
 
Dogo usipende kutafuta umaarufu kwa kutaja majina makubwa ya watu!!! Weka ushahidi wapi Pinda kaomba kusaidiwa.....

Kumbuka: Wote tuko Dodoma na hatuyaoni hayo unayo ropoka..

Kuna waliomwona akienda Msalani kujisaidia,we ulimwona?
 
Msishangae ndio michezo yakidumu pia msishangae kesho kusiwepo mtu yoyote atakae chukuliwa hatua ndio kidumu bana na ndio faida yetu yakuweka kidumu baadala yakuweka vyama venye mapenzi ya kweli nawananchi wake
 
Tulia comrade harakati zote za kuzuia ripoti isiingie bungeni anafanya nani na kwanini? unaweza ukaishi Nyumba moja usijue kinachoendelea kulingana na status yako...

inawezekana status yako ni Kama tambara la deki unaishia mlangoni tu

Kula five mkuu!akili za kitoto naye anajiona kakuwa!
 
Hizo akili za inzi usihangaike nazo mkuu tuelekeze macho na masikio kwa dubu wanaomaliza watu wetu ....

we MTU hela za kuhonga watu 100 kila MTU milioni unatoa wapi? halafu unafanya hayo watu wako wanakufa bila dawa kweli??

kwakweli hili swala limenikinaisha Sana wapigwe tu mbwa mwitu hao....

Mkuu mbinu za ukinyonga umezipatia wapi?

Mahakama na huyu wakili wa ipitiel wamefanya nambo ya maana sana.

Kama Kashilila kakataa kupokea barua hiyo wakili abandike hapo kwenye lango kuu la kuingia viwanja vya bunge.

Mahakama nayo naishauri isiachie hukumu yake hapa tu. Iweke zuio kwa nchi wafadhili zikomeshe kutokutoa misaada ili misaada ya kimaendeleo iendelee kuja dawa zijae mahospitalini.

Pia mahakama ihakikishe inaweka zuio la ziada kwa nchi wafadhili ilisiweze kufikiria kuweka vikwazo zaidi hasa kufungia akaunti za vigogo zilizo huko kwenye nchi zao. Maana tishio hilo haliepukiki kama ESCROW itagonga mwamba. Kwenda kutibiwa huko nchi za wahisani kwa vigogo inaweza ikawa shughuli pale watakapo zuiliwa kuingia nchi hizo za wafadhili. So mahakama ihakikishe haya yote yanawekewa zuio.
 
Wakuu,

CCM wamekutana kwa dharura muda huu katika ukumbi wa ikulu ya Dodoma.

Agenda kuu ni kupitia ripoti nzima na MAPENDEKEZO ya PAC, Wanataka kupitia mapendekezo ya PAC mapema na kulekezana namna ya kuokoa, pia ripoti waliyogawa kwa wajumbe haina vielelezo kwa ajili ya rejea. Mbali na bank statements ya Rugemarila, imefichwa ya Pap.

Wamewaita wajumbe wote wa CCM waliopo PAC ili watolee ufafanuzi wa mapendekezo hayo.

Wajumbe hao ni:

Zainab vullu, Ali Mohamed kessy, Jabir marombwa, Faida Bakari, Kangi Lugola, Deo filikunjombe.

Katika hatua nyingine Katibu wa bunge Mr Kashilila amegoma kupokea barua ya Mahakama.

Barua hiyo imeletwa kwa ndege ya kukodi,Wakili aliyefungua kesi anatoka kijiji kimoja na Pm, alikuwa NCCR Mageuzi zamani sasa yupo CCM.

Aden Rage hajaitwa?
 
Mkuu mbinu za ukinyonga umezipatia wapi?

Mahakama na huyu wakili wa ipitiel wamefanya nambo ya maana sana.

Kama Kashilila kakataa kupokea barua hiyo wakili abandike hapo kwenye lango kuu la kuingia viwanja vya bunge.

Mahakama nayo naishauri isiachie hukumu yake hapa tu. Iweke zuio kwa nchi wafadhili zikomeshe kutokutoa misaada ili misaada ya kimaendeleo iendelee kuja dawa zijae mahospitalini.

Pia mahakama ihakikishe inaweka zuio la ziada kwa nchi wafadhili iliziweze kufikiria kuweka vikwazo zaidi hasa kufungia akaunti za vigogo zilizo huko kwenye nchi zao. Maana tishio hilo haliepukiki kama ESCROW itagonga mwamba. Kwenda kutibiwa huko nchi za wahisani kwa vigogo inaweza ikawa shughuli pale watakapo zuiliwa kuingia nchi hizo za wafadhili. So mahakama ihakikishe haya yote yanawekewa zuio.


Ukinyonga Wa nini?
 
Hizo akili za inzi usihangaike nazo mkuu tuelekeze macho na masikio kwa dubu wanaomaliza watu wetu ....

we MTU hela za kuhonga watu 100 kila MTU milioni unatoa wapi? halafu unafanya hayo watu wako wanakufa bila dawa kweli??

kwakweli hili swala limenikinaisha Sana wapigwe tu mbwa mwitu hao....

Kwakweli inasikitisha kabisa halafu anaye jiita waziri mkuu anatoa mazingira ya bunge kuingiliwa kazi yake! Wakili wa PAP ametumia mwanya wa bar aka za pinda juu ya Mahakama! Tusubiri kesho hiyo tujionee wezi wakiwekwa hadharani!
 
Pinda anahangaika sana, kwanini asiachie ngazi kama Lowassa kupisha aibu ya Serikali yake? Kama kiranja mkuu wa shughuli za serikali alishindwa vipi kujua kuwa zile zilikuwa fedha za walipa kodi wa Tanzania? anahangaika sana kutumia mahakama na mbinu chafu za kuzima mijadala kwa kuhofia nini? 8 B alizomegewa kwaajili ya Kampeni ya urais hakujua?

Pinda hawezi kujitoa kwenye hii court injunction maana yeye ndio aliandaa mazingira toka mwanzo mbele ya bunge! Report isipo somwa na kujadiliwa laana hiko juu yake!
 
Kwakweli inasikitisha kabisa halafu anaye jiita waziri mkuu anatoa mazingira ya bunge kuingiliwa kazi yake! Wakili wa PAP ametumia mwanya wa bar aka za pinda juu ya Mahakama! Tusubiri kesho hiyo tujionee wezi wakiwekwa hadharani!


Mbona Lowassa alijiondokea bila kikwazo iweje hawa waitie nchi kwenye machafuko? kwa lipi walilonalo??

yaani waziri mkuu mzima unatumia mpaka wahuni kisa kulinda cheo??

Pinda nimemdharau Sana....
 
Na wazidi kuvurugana. Pesa yetu hii ya PAYE iweje waone ni kawaida tu kutunyonya jasho letu?

Saa imewadia.
 
Mbona Lowassa alijiondokea bila kikwazo iweje hawa waitie nchi kwenye machafuko? kwa lipi walilonalo??

yaani waziri mkuu mzima unatumia mpaka wahuni kisa kulinda cheo??

Pinda nimemdharau Sana....

Yani Mimi kanikera sana tena sana huyu jamaa!
 
nimependa maelezo yako ila hapo mwishoni ndo umekua mnafiki.. Huyo wakili aliyeleta hiyo barua na ndege ya kukodi kwanini usiseme zamani alikua nccr na sasa yuko chadema(marando)? Jaman mbona unafiki unawazidi mnashindwa kuinena kweli tupu?

ndugu yangu usihangaike, huyu yeriko ni malaya wa kisiasa ni lazima afanye hivyo ama sivyo hata lipwa dau lake na hao mabwana zake
 
Watanzania wakiichagua CCM 2015 itadhihirika wazi wazi kuwa tumelogwa.

Kasha ya Escrow inatosha kabisa kuiangusha CCM.

Kama ilivyoandikwa "enyi wagalatia msio na akili ni nani aliyewaloga?" Wagalatia 3:1

Sasa nauliza enyi Watanzania msio na akili ni nani aliyewaloga mpaka kashfa zinapita bila kuichukulia hatua CCM.

Ilibidi miji yote tuandamane mpaka CCM ing'oke Mara moja. Tusipofanya hivyo tumelogwa.
 
Leo hadi wafia chama na wenyewe wameamka nimeamini ule usemi usemao hata nyie msipo sifu na kuimba basi milima na mawe yatasifu na kuimba. Hii ni ishara mbaya sana kwa watawala wakiendelea kushupaza shingo zao hakika zitavunjika
 
Back
Top Bottom