Kikao cha CCM ikulu ya Dodoma muda huu kupitia mapendekezo ya PAC

Kikao cha CCM ikulu ya Dodoma muda huu kupitia mapendekezo ya PAC

Yericko Nyerere

Platinum Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,519
Wakuu,

CCM wamekutana kwa dharura muda huu katika ukumbi wa ikulu ya Dodoma.

Agenda kuu ni kupitia ripoti nzima na MAPENDEKEZO ya PAC, Wanataka kupitia mapendekezo ya PAC mapema na kulekezana namna ya kuokoa, pia ripoti waliyogawa kwa wajumbe haina vielelezo kwa ajili ya rejea. Mbali na bank statements ya Rugemarila, imefichwa ya Pap.

Wamewaita wajumbe wote wa CCM waliopo PAC ili watolee ufafanuzi wa mapendekezo hayo.

Wajumbe hao ni:

Zainab vullu, Ali Mohamed kessy, Jabir marombwa, Faida Bakari, Kangi Lugola, Deo filikunjombe.

Katika hatua nyingine Katibu wa bunge Mr Kashilila amegoma kupokea barua ya Mahakama.

Barua hiyo imeletwa kwa ndege ya kukodi,Wakili aliyefungua kesi anatoka kijiji kimoja na Pm, alikuwa NCCR Mageuzi zamani sasa yupo CCM.

UPDATES
Mwelekeo ni kuokoa chama na serikali, wametoka dk hii kikao kimeisha, wajumbe Wa pac walioitwa Wali escape (walitia ngumu, walifika na kutoka)

Wabunge Wa ccm wameambiwa kuwa imara na kushikamana Kwa maslahi ya Chama, AG na Muhongo walikuwa wanawapa somo, January Makamba amemshutumu waziri mkuu kwa kuzembea,

Wamekubaliana kwa kauli moja kuwakabili UKAWA.
 
Wakuu,

Ccm wamekutana kwa dharura muda huu katika ukumbi wa ikulu ya Dodoma,

Agenda kuu ni kupitia ripoti nzima na MAPENDEKEZO ya PAC,

Wamewaida wajumbe wote wa PAC ili watolee ufafanuzi wa mapendekezo hayo.

Eee Mungu wa yakobo na isaka tenda haki. Sasa chama kinawaitaje pac? kwani pac ni ccm?naje pac inawajibika kwa ccm hafi waitwe na hicho chama? Naje kweli pac zito wamekubali kuingia kwa hicho kikao cha pukoo wa panya? Nani wakunijibia maswali haya. Ee Mungu tuokoe cc watz
 
Zainab vullu, Ali Mohamed kessy, Jabir marombwa, Faida Bakari, Kangi Lugola, Deo filikunjomb

wasiwasi wangu wasije wakawekewa POLONIUM-210
 
Wanatapa tapa sana lakini mioyo wa Watanzania inasubiri kesho ili ijulikane mbivu mbivu.
 
Wakuu,

Ccm wamekutana kwa dharura muda huu katika ukumbi wa ikulu ya Dodoma,

Agenda kuu ni kupitia ripoti nzima na MAPENDEKEZO ya PAC,

Wamewaida wajumbe wote wa PAC ili watolee ufafanuzi wa mapendekezo hayo.

Wajumbe hao ni:

Zainab vullu, Ali Mohamed kessy, Jabir marombwa, Faida Bakari, Kangi Lugola, Deo filikunjomb
Nani anasimamia kikao? Nchi iko kwenye dharura!
 
Hivi kwanini Ccm inatumia nguvu kubwa hivyo kuwa tetea wezi? Kuna siri gani hapo kati kati? Hivi Mwalimu Nyerere angekuwa hai huu upuuzi ungefanyika kweli? Ccm mbonamnajidhalilisha mbele ya wananchi? Siamini kama mmefikia hapo.

Sioni mantiki ya kujadili hili jambo. Kama ni wezi fukuzeni na warudishe hela. Kinyume na hivyo tuaminisheni mnajua mpango wote wa wizi kwa manufaa ya chamachenu. Familia ya panya.
 
Mpk ndege ya kukodi kuleta barua? Dhl wamekataa kuipeleka naona. Hivi Tanzania tumelogwa na nani?
 
Watapigana lakini watapigwa, watashindana nasi lakini watashindwaaaa! majambazi wote lazima wakamatwe tu.
 
Ukiumwa na nyoka, hata ukiona kamba utaruka. Ninaanza kupata harufu ya hawa hawa walivyokaa waafikiana ku halifu BMK. Ccm hawaaminiki tena kwa kuwa wao dio mafisadi, nahisi kama wanatafuta namna ya kuharibu mpango mzima.

Ninaomba, report iwekwe hapa mtandani kama zile picha za Mauji ya Mwangosi ili wananchi kwanza tuupate ukweli, kusudi tusije kunaswa na hila na uzushi wa ccm.

Pili naomba tuisome report full ili tuweze ku monitor kinachoendelea na chochote kitakachofanyika kesho.

Tatu tukishaisoma na kuielewa, tutakaopoona ugaidi ama uharamia wowote, sisi kama wenye nchi, tutatoa maamuzi na kuyatekeleza. Binadamu anayeshindwa kutetea watoto wake wakati wa matatizo, hafai hat kuwa sehemu ya jamii. Sasa ni vita, wananchi na mafisadi, kwa ajili ya maisha ya vizazi vyetu.

Hatupendi waje wafukue makaburi yetu wakiomboleza kwamba tuliwazaa na kuwatelekeza na hatukuwalinda katika nchi tuliyowaweka. Hapana. Sasa ni misho.

MUNGU SIMAMA UPANDE WA WANAOONEWA.
 
Nimependa maelezo yako ila hapo mwishoni ndo umekua mnafiki.. huyo wakili aliyeleta hiyo barua na ndege ya kukodi kwanini usiseme zamani alikua Nccr na sasa yuko Chadema(marando)? Jaman mbona unafiki unawazidi mnashindwa kuinena kweli tupu?
 
Eee Mungu wa yakobo na isaka tenda haki. Sasa chama kinawaitaje pac? kwani pac ni ccm?naje pac inawajibika kwa ccm hafi waitwe na hicho chama? Naje kweli pac zito wamekubali kuingia kwa hicho kikao cha pukoo wa panya? Nani wakunijibia maswali haya. Ee Mungu tuokoe cc watz

Huyu Mungu unaemlilia alishakwambia'jisaidie na mimi nitakusaidia',ni vizuri ukawa wa kwanza kujiandikisha katika daftari la wakaazi na ukaishawishi jamii inayokuzunguka nayo ikafanya hivyo ili uweze kupata haki ya kuweka Serikali safi madarakani lakini kulia tu bila ya kuchukua hatua ni kazi bure.
 
Kwa maandishi makubwa, CCM NI GILIATH NA UKAWA NI MUSA. Despite of their hugeness but truth will be revealed
 
Hivi kwanini Ccm inatumia nguvu kubwa hivyo kuwa tetea wezi? Kuna siri gani hapo kati kayi? Hivi Mwalimu Nyerere angekuwa hai huu upuuzi ungefanyika kweli? Ccm mbonamnajudhalilisha mbele ya wananchi? Siamini kama mmefikia hapo. Sioni mantiki ya kujadili hili jambo. Kama ni wexi fukuzeni na warudishe hela. Kinyume na hivyo tuaminisheni mnajua mpango wote wa wizi kwa manufaa ya chamachenu. Familia ya panya.
NYerere akifufuka leo anakufa tena hapo hapo kwa shinikizo la moyo
 
Huyu Mungu unaemlilia alishakwambia'jisaidie na mimi nitakusaidia',ni vizuri ukawa wa kwanza kujiandikisha katika daftari la wakaazi na ukaishawishi jamii inayokuzunguka nayo ikafanya hivyo ili uweze kupata haki ya kuweka Serikali safi madarakani lakini kulia tu bila ya kuchukua hatua ni kazi bure.

Kaka nipo vizuri hayo yote nayafanya na naendelea kufanya
 
Back
Top Bottom