Kijana asimulia jinsi Mchina alivyomtupa kwenye banda la mbwa, kisha mbwa mmoja kumuokoa

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,803
2,000
Kijana huyu ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kiwanda cha kutengenezea viatu vya yeboyebo ambapo mmiliki wa hicho kiwanda ni mtu mwenye asili ya China (Mchina).

Kwa mujibu wa kijana huyo anadai muajiri wake huyo mchina alimtupa kwenye banda la mbwa wanne ambao watatu ndio walimshambulia na yeye akawa anapambana nao.


Mmoja wa mbwa hao wanne alikuwa mbwa mkubwa ambaye hakumshambulia ila alipoona kijana ameanguka chini na hawezi kupambana tena na wale watatu ndipo alipowakoromea mbwa hao wengine watatu wakaacha kumshambulia

Baadae wafanyakazi wengine wa kiwanda walikuja kumtoa kijana huyo hospitali na akenda kujitibu lakini kutokana na uhaba wa fedha hajapona vizuri mpaka sasa

Kisa cha muajiri huyo kufanya hivyo kwa mujibu wa kijana anasema alimwambia kuwa hawezi kufanya kazikatika kitendo ambacho alipangiwa kwa kua kulikuwa na moshi mkali

Msikilize zaidi hapa

 

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,552
2,000
No wonder kuna watu wanaua ila si kama wanaroho za kuua, ni uonevu kama huu, mimi kwa akili zangu hizi mbili zisizopenda manyanyaso ningeenda kubeba lile gobole na kuelekeza kwenye kichwa cha mchina halaf naachia triger halaf nasubir adhana nizike, pona yake nimtengue miguu halaf nimpigie msumali wa inch 6 kwenye paji la uso nimwache aende zake kwa kujidai.
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,731
2,000
Na sio ajabu mamlaka zipo na zina taarifa lakini kwa kuwa haina uchochezi, hawahangaiki mpaka pale mchina huyo atakapokosa uzalendo! Ni aibu kwa mamlaka za kukamata na kushtaki kwani kila opd ya hosptali ya umma kuna dawati la polisi lenye kutoa form ya ruhusa ya kupata matibabu (pf 3) hasa kama maumivu hayo yamaesababishwa na mwingine. Kama ana hiyo pf3 aishtaki polisi kwa kutomtimizia hitaji lake la kumkamata mchina na kumshtaki kwa mbwa wake kumshambukia ili wale mbwa wawekwe chini ya ulinzi pamoja na mwenye nao! Nchi nyingine hukuti ujinga huu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom