Kiingereza aibu kwa mawaziri wa JK

Kwa hiyo hoja yako nini hapa?unaongela kila mtanzania anaathiriwa na lugha yake ya kuzaliwa, sasa unataka ngeleja awe na "accent" kama ya Obama au ya queen Elizabeth. Afadhali yeye mwenye accent yake kule wale wanao-tamani kuongea accent za kizungu. Mbona huwa hatuwacheki wenzetu wajapani, wachina na wahindi wanapoongea kiingereza kwa accent zao na wakati mwingine hakikunyooka?
 
Huo ufananisho wako umeniacha hoi...ina maana hujaona waziri aliepo madarakani anaejua kiingereza mpaka umtaje huyo ex mbunge?
 
Siyo lugha yake wala simshangai.mbona hamuwashanga waingereza wanapokosea kiswahili?

Watanzania tuna kazi kubwa. Sasa kwa mfano huyu Ngeleja atoke kwenye Kisukuma, aje kwenye Kiswahili kisha aende kwenye kiingereza huoni ni vigumu. Akifika kwenye kiingereza ubongo unakuwa umesahau ama umechoka. Wangekuwa wanaongea Kiswahili tu kwa kujificha kwenye kichaka kwamba tunapromote kiswahili badala ya kujitutumua kwa kidhungu!!
 
Watanzania huwa tunajifanya kuwa wamaana sana na kiswahili, ukiwa nje ya nchi kama hujui kiingeleza wewe ni kishoie tu. nchi nyingi zinazungumza kiingeleza. Serikali inabidi ibadilishe mfumo wa elimu watu waanze kusoma na kujifunza kiingeleza kuanzia chekechea na maana kwamba kmedium of communication iwe ni kiingeleza tu.
 
Leo nimempata Ngeleja akisoma hotuba, aibu. embu soma zikiza hii.. the the the the..... Masha yuko juu sana kwenye kiingereza

5. Opening speaker Minister William Ngeleja part 2 (International Energy Conference 2009) - YouTube

Mtoa mada, unataka kuendeleza kasumba ya kutukuza lugha ya wengine siyo?
Kumbuka mfumo wa elimu yetu unatubainishia kuwa Kiingereza ni lugha ya tatu,
unaanza na lugha ya asili (kwa mfano Kisukuma kwa Ngereja), Kiswahili na ya tatu
ndiyo Kiingereza, kwa hiyo unataka aongee accent kama ya Cameron au Obama
wakati yeye ni Mswahili? This is nonsense!
 
Kwel bado tumetawaliwa. Wazir kutojua kiingereza anaonekana kama ametenda dhamb. Mzungu asipojua kiswahil je?. Acha ujinga Ngeleja na wewe tumia Kiswahili.
 
Jana nilliona "live" ile press conference ya pamoja baada kikao cha Libya kule Paris. Sarkozy aliongea Kifaransa, Cameron akaongea Kiingereza, Ban Ki Moon akaongea Kiingereza chake kile, Waarabu wa Libya na Qatar wakaongea kwa Kiarabu chao. Sisi hapa tunashindwa nini?
 
bora yupi ajue kiingereza lakini uwezo mdogo wa utendaji??au asijue kiingereza lakini uwezo mkubwa kiutendaji???mtachanganyikiwa sana safari hii!
 
We vipi kwani ngereja ni waziri wa kingereza au Au ni alikuwa mwalimu wa HGL au english lingustic ? Na kwanza hii sio siasa. Peleka kwenye lugha.

Hukuwaii kuleta mada kesho unasema Tuna matatizo ya mgao wa umeme sababu ngereja hajui kingereza

Tulikuwa kwenye mkutano wa Jumuia ya Afrika Mashariki pale Naura Springs mwezi uliopita Meya wa Arusha Gaudence Lymo alianza kusoma speech yake hivi "Lady and Gentlemens" Hapa hakuna swala la accent bali ni ufinyo wa kuelewa lugha au elimu. Nilijisikia aibu sana kuwakilishwa na meya asiejua kusoma hotuba kwa kiingereza tena ya kuandikiwa. Aliyewakilisha Burundi alitoa hotuba yake kwa kifaransa na kurudiwa na mkalimani. Sisi pia tuanze kuwatumia wakalimani.
 
mbona Jk kwenye conference brussels alisema madam chairman!!!!
 
Huyu Ngeleja si aligradyueti na honors pale UDSM faculty of law.....na huko si nasikia ndo kuna manguli wa kingredha....sasa iweje aunganishe unganishe?
 
Afadhali huyo kuna siku Mkuu wa Kaya alikuwa anafanyiwa interview na Clouds Fm siku ya birthday yake. Basi msikilizaji akapiga simu na kum-wish ''happy birthday Mr. President'' jamaa akajibu ''oooh! The same to you''
 
HA HA HA HA MWITA UMEBADILIKA, DAAHHH.. Ndacha bhono bhonoo...kweli hakuna marefu yasio kua na ncha..na kingereza chako kile ha ha ha kama unatwanga!
 
Back
Top Bottom