Kigwangalla azidi kumkalia kooni Dr. Mwaka

Kigwangalla azidi kumkalia kooni Dr. Mwaka

Nipe takwimu ni kina mama wangapi waliofanikiwa na ni wangapi walipata damage? Mbona babu wa samunge maarufu kikombe cha babu alisababisha vifo vingi tu lakini kimya? Tuache siasa nyepesi tufanye kazi.

Clearly, utakuwa unaloga wewe. Kwa kuwa "Babu wa Samunge alisababisha vifo vingi", basi Mwaka aachwe aendelee kudanganya watu? Watu aina ya kina Mwaka na Babu wa Samunge wanashamiri kwa kuwa jamii yetu inaamini sana mazingaombwe (superstition/super natural stuff) na shortcuts. Ushauri wangu: Mwaka na wenzake wengi wa aina yake wachukuliwe hatua kali sana, ikiwa ni pamoja kufungwa jela na kufilisiwa mali zao walizopata kwa njia ya udanganyifu.
 
Hata hujui kumbe Kigwangallah alianza vipi kudeal na Mwaka...ni kupitia malalamiko ya watu kwa njia mbalimbali...sasa ikiwa kuna wengine unawajua basi usitegemee miujiza ifanyike ili na sisi tuwajue...fanya uwaweke hapa ili uwe sehemu ya raia wema kwa kutoa taarifa zitakazo fanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.

Mimi sitetei anachofanya Mwaka kama kipo nje ya maadili hoja yangu ni kuwa kuna maelfu ya watu wa aina yake yeye kama waziri badala ya kudeal na MTU mmoja akatoa maelekezo kuhusu Hawa jamaa wa tiba mbadala. Hivi babu wa loliondo na mwaka nani alisababisha madhara makubwa kwa taifa, na Si yupo? vipi kuhusu maelfu ya manabii na wachungaji wanaojitapa kuwa wanatibu magonjwa Fulani? Sidunishi jitihada za mh. Bali aende mbali zaidi ili umma usiishie kuona tatizo ni mwaka tu Bali tatizo ni kubwa zaidi, aadress tatizo sio MTU ili ionekane ana deal na tatizo na Si MTU.
 
kuna mtu mmoja pia ni kariba ya Dr mwaka anajiita Dr Joseph manyirizu yupo mwanza mabatini Barbara ya kuelekea shule ya msingi mabatini ukitokea stend ya hice mabatini yeye huyu jamaa hata form four hajamaliza lakin anajitangaza yeye ni suluhu ya matatizo ya moyo kisukari pamoja na magonjwa yote ya akina mama. Simuonei haya manyirizu anadanganya anakipimo cha kompyuta kinaitwa Quantum kinachopima mishpa ya damu kama inamafuta na pia kina kuangalia matatizo ya kina mama. Anaajili mpaka mabaa medi kuwa madaktari na watoa huduma kwa kuwafundisha udaktar kwa mwezi mmoja wakat yeye hana taaluma hiyo. Manyirizu amekua mswahili sana juu ya tiba zake kwani anadai anatiba ya kuongeza CD4 kwa waathirika wa UKIMWI huu ni uhujumu wa afya zetu kituo chake kinaitwa SUNVERA HERBAL CLINIC yupo mkono wa kulia ukiwa unaelekea shule ya msingi mabatini kalibu na MWANGA GUEST HOUSE. Kigwangala agiza watendaji walioko jijini Mwanza wakachunguze huyu mtu maana ni janga tayari .
 
Hii nchi bana, ni vituko vituko vituko! Dr. Kigwangala nakushauri kama unapenda ujulikane zaidi kwenye unaibu Waziri wako, nenda katibu wagonjwa walau Mara moja kwa wiki katika hospitali yetu ya Muhimbili, hili litamfanya Rais wetu Dr Magufuli akuamini zaidi. Mwaka mwaka mwaka why? Huu ni mwaka 2015 tufanye kazi tupunguze porojo za media

Wacha Waziri afanye kazi, utapel umezidi sana nchi hii. Kigwangala angekuepo enzi za mzee wa loliondo watu wasingekufa kiasi kile....
 
Kuna mawili hapa , la kwanza ni Fitna za kibiashara toka Kwa Wamiliki wengine wa clinic za Dawa Asili , pili kinachomtafuna sasa ni ile Tabia aliyokuwa ameanza ya kuwavua nguo Wanawake kisha kusingizia kuwa anawapima Ugumba , UTI na magonjwa ya zinaa , kibaya zaidi alimchungulia Mke wa kigwangala pindi alipoenda kutibiwa pale.

Basi Kingwangala akachungulie huyo wa kakwe ngoma iwe droo. Kila dakika Mwaka mwaka , waziri mzima hata aibu hamna? Si umeite huko ofisini kwako mmalizane? Huku kwenye media unadhani anayeaibika ni nani kama si wewe?
 
Kuwe na personal issues au lah...the bottom line ni kwamba Mwaka ni tapeli and somebody sensible has to STOP him and fortunate that person appeared to be Kigwangala.

Waathirika wakubwa wa utapeli wake ni mama zetu, dada zetu na bibi zetu na shangazi zetu and on top of all, wake zetu.

Kama utapeli huu wa Mwaka haujakukuta huwezi kuelewa lolote.
Sawa....na pole sana, wajinga ndio waliwao
 
Hivi hakuna mengine ya kujadili humu? Dr Mwaka ni ktk nchi hii ajadiliwe? Alikkwepa kodi? Ni chuki tu!

Huyu ni tapeli, lazima ajadiliwe, Wahanga wa utabibu wake ni wengi sana watu wametapeliwa hela nyingi sana na mwaka
 
hospitali zipo wakaacha kwenda wakamwamini mwaka sasa wanalia nini?
 
Mkuu wakati mwingine sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana! Wakina mama wengi watakuwa wame athilika kiafya kutokana na utapeli wa jamaa huyu,sijui nani alikuwa anaidhinisha apewe AIRTIME ya kuwazuga wakina mama.

Watu wanaweza kudhalilishwa hata Vyombo vya habari visilipoti hata Mara moja,
Au mkuu umewahi kusikia malalamiko utujuze.
 
Waache maigizo...hawa mawaziri warudi ofisini waongee na watendaji washughulikie changamota za wananchi
 
Tujadili masuala mtambuka ya nchi yetu. WHO IS MWAKA?
 
Alimla mchepuko wake au? Maana hakuna mgonjwa amelalamika mpaka sasa hivi
 
Si tusubiri huo uchunguzi ufanyike tupewe majibu. Mnaomtetea Dr Mwaka mnamjua vizuri au? au na nyie mnaathirika indirect.
 
Kwenye hilo jimbo lake la Nzega vijijini kwenye jimbo lake hakuna hata hospital. Kwanini asianze na hilo kwanza? Yale yale ya babu seya na jk
 
Lazima tutambua waziri hicho anachokifanya kipo ktk himaya yake,sasa basi lazima aanze na yule ambae kila kukicha tunamsikia na baade a deal na wengine
 
Mimi sitetei anachofanya Mwaka kama kipo nje ya maadili hoja yangu ni kuwa kuna maelfu ya watu wa aina yake yeye kama waziri badala ya kudeal na MTU mmoja akatoa maelekezo kuhusu Hawa jamaa wa tiba mbadala. Hivi babu wa loliondo na mwaka nani alisababisha madhara makubwa kwa taifa, na Si yupo? vipi kuhusu maelfu ya manabii na wachungaji wanaojitapa kuwa wanatibu magonjwa Fulani? Sidunishi jitihada za mh. Bali aende mbali zaidi ili umma usiishie kuona tatizo ni mwaka tu Bali tatizo ni kubwa zaidi, aadress tatizo sio MTU.

Hivi mnafahamu kuwa kuna tiba mbadala zinaweza kutibu mfupa uliovunjika kabisa ambao hospitalini hauwezekani?

Dr. Mwaka anaweza kuwa a?a mapungufu lkn ana mchango mkubwa kwa wenye ugumba.

ikumbukwe aliwahi kufungiwa akina mama wakalalamika.
kwa hiyo wapo wanaofurahia tiba zake.

inetakiwa aelekezwe anachotakiwa kufanya na asichotakiwA kufanya.
 
Back
Top Bottom