Kigoma: Mganga wa Kienyeji afungwa jela maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka 8

Hivi ni kwanini watu wanategemea sana tiba mbadala?
hata za kawaida madaktari wanabaka wagonjwa wao rejea yule Dokta aliyembaka mama mjamzito.
tatizo ni Alkasusu ikishakolea kwenye Damu hamna control
 
Halafu Zitto hataki World Bank watuletee fedha za kuondoa Ujinga huu Kigoma
Nadhani una lako jambo na huyo Zitto. Kama unataka hayo manoti ya WB nenda kalambe viatu vyao utapata tu. Hapa tunamzungumzia mganga wa huko huko Kigoma kwenu aliyemlawiti mtoto wa kike wa miaka 8.
Huo mkopo ungesaidia nini hapo kigoma kwa mganga mjinga ka huyu?? Mbona hakumtamani mamake mtoto badala yake kamtuma wembe mbali ili amalize kiu yake???
Mganga angemtishia mamake kuwa kama havui nguo saa hiyo mtoto angemfia. Nadhani mambo yangekuwa verry
 
Mungu amlaze gereza LA bangwe salama....amiin.
Sifa mbaya kwa mkoa wangu Wa kigoma shenzi sana huyu pumbavu.
 
Mahakama ya Wilaya Kigoma Mkoa wa Kigoma imemhukumu mganga wa kienyeji, Venas Edward (48), mkazi wa Ujiji Manispaa ya Kigoma/Ujiji kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnajisi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane

View attachment 1337779

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Katoki Mwakitalu, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kosa hilo pasipokuacha shaka yoyote.

Hakimu Mwakitalu alisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Raymond Kimbe, na ulipeleka mashahidi wanne na kielelezo kimoja ambacho ni PF3.

Alisema mama wa mtoto huyo alimpeleka mtoto wake nyumbani kwa mshtakiwa kwa ajili ya kutibiwa, na baada ya kumfikisha, mganga alimtuma mama huyo aende dukani kununua wembe.

Alisema baada ya mama kwenda dukani, mshtakiwa alimfanyia mtoto huyo kitendo hucho cha kikatili.

Alieleza kuwa baadaye mama wa mtoto huyo alifika kutoka dukani na kumchukua mtoto wake na kurudi nyumbani kwake.

Alieleza zaidi kuwa baada ya muda mama alisikia mtoto wake analalamika kusikia maumivu sehemu zake za siri, ndipo mama alipomkagua na kugundua kuwa mtoto wake alikuwa amenajisiwa.

Aliendelea kueleza kuwa mama wa mtoto huyo alimbana mtoto wake kwa kumuuliza ni nani aliyekufanyia kitendo hicho ndipo alimjibu kuwa ni mshtakiwa.

Mshtakiwa huyo baada ya kuhukumiwa kwenda jela maisha, aliangua kilio hadharani na kusababisha ndugu zake nao kuanza kuangua vilio mahakamani mbele ya umati uliofika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza hukumu hiyo.

Awali akisoma hati ya mashtaka Wakili Kimbe alidai kuwa Aprili 23, mwaka 2019 majira ya asubuhi eneo la Kasoko Ujiji, mshtakiwa alinajisi mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.
ANA LAANA ZOTE HUYO EDWARD
 
Back
Top Bottom