Kuna matatizo mengi sana katika hayo maandishi na sio English pekee. Hii inadhihirisha jinsi watu wasivyokuwa makini katika kazi. Hivi kweli hakuna hata mfanyakazi wa hapo uwanjani aliyeona hii kitu?
Ukosefu wa uwajibikaji na ufuatiliaji ndio matatizo yetu. Si ajabu walimpatia kazi ''painter'', wakachakachua malipo yake na biashara ikaishia hapo. Hakuna aliyekumbuka kuja kukagua kazi.
Kama mambo ''madogo'' kama haya hatuyaoni/hatuyasomi, vipi kwenye mkataba wenye kurasa zaidi ya 70, tena kwa kiKoloni? - no wonder DOWANS, Richard Monduli et la imekubwa wimbo tuliouzoea.