Kigogo CCM na kashfa ya UTAPELI, ahaha kujisafisha

hapa kuna kulipizana kisasi, kwani haiwezekani mtu atoweke kazini 2008 atafutwe leo. je hapa kati kati angekuwa anatapeli pesa za wateja kwa jina la kampuni ingekuwaje? they are not serious.
ni siasa uchwara tu hao

Kwa hiyo unadhani ukikwiba leo halafu ukakwepa kukamatwa kwa siku kadhaa basi utakuwa umesalimika? Angalia mazingira ya kesi hii, kama mwajiri alimpa nafasi alipe na hakufanya hivyo badala yake akaendelea kukusanya pesa zaidi toka kwa wateja mwajiri amuache tu kisa kosa lilianza 2008?
 
Kwa hiyo unadhani ukikwiba leo halafu ukakwepa kukamatwa kwa siku kadhaa basi utakuwa umesalimika? Angalia mazingira ya kesi hii, kama mwajiri alimpa nafasi alipe na hakufanya hivyo badala yake akaendelea kukusanya pesa zaidi toka kwa wateja mwajiri amuache tu kisa kosa lilianza 2008?

Ni bora wewe umewafafanulia raia Matomaso
 
Sio viongozi peke yao na sisi raia ni wezi vile vile, tunaibia serikali kwa mbinu nyingi tu. Utapeli kwenye tenda, risiti feki na mengi tu.

Inasikitisha! Miaka nenda miaka rudi nimeisikia hoja hii ikitumika kujifariji au kuhalalisha wizi katika ofisi za umma. Na kwa bahati mbaya sana baada ya kuminya fursa za vipato halali, viongozi wetu wameishia kuikumbatia hoja hii kama ndio jibu rasmi la kuachia mambo yaendelee shaghalabaghala (kama vile mkakati wa kuhakikisha kila mtu anaguswa na tone la damu ilhali wachinjaji ni wao). Anayelalamika anaishia kutumiwa "wachunguzi" watafute "jeuri" yake inatoka wapi; anadokoa kisirisiri? nani anampa misaada? ...

Hapana, inabidi ifike mwisho. Na ni viongozi tu ndio wenye dhamana na uwezo wa kudhibiti kukithiri kwa utamaduni wa wizi - hata wa kughushi risiti!
 
Usishangae hiyo shortlists ya mh. mbona kuna watu walikuwa wanatuhumiwa kuuza madawa ya kulevya lakini mkuu aliwapigia debe wakati wa kampeni,hii ndo bongoland lazima utumie bongo,taifa la watu wadogo ukitaka chai nenda TATEPA
 
Hao MOGAS si wamkamate wamfungulie mashtaka?kuliko kuchafuana,mahakama ndiyo inauwezo wa kusema nani yuko sahihi mengine tuwaachie wenyewe,tofauti zao hazituhusu kama ilikuwa njama ya kupakana matope itabidi wamsafishe,mwache dogo achape mzigo.
 
This is a very serious issue! Hvi hiyo rb iliyofunguliwa polisi kituo cha kilwa imefikia wapi manake inaonyesha ni ya mwaka 2008 ? jamaa alipelekwa mahakamani? anyefahamu anijuze !
 
My country can not rest in peace, I see, but CCM will do instead..!!
 
El Toro, ungebadilisha title ya post yako, hata ianze kwa kusomeka, "utabiri watimia..." nna mashaka sana na Uteuzi huu wa maDC.
 
Mimi si kwamba namtetea huyu jamaa la ila je sisi wengine tunauhakika kuwa tu wasafi au tu kama yeye. ila kwa ili la kwenda kugombea tena ubunge kwa hawa inatiashaka sana maana watu wengi ni wezi tu. ila rais wetu saa nyingine anatia aibu sana katika uteuzi wake maana anaowateua wakati mwingine wanatia hata kichefuchefu jamani
 
Hilo jalada la wizi Polisi lilishafungwa? El Toro tujuze tujue pa kuanzia.
 
babu yangu alinieleza kitu pindi nikiwa na umri wa miaka 10 alisema ongopa sana familia ya wazazi wezi iwe siwe hata watoto wao watakuja rithi sikujua ila nimeyaona baada ya kuwa na kukua na ufahamu wangu kuongezeka nimeona alikuwa anaongea ukweli JK na wenzake hawawezi kaa sahani moja kama hawana maelewano ya wizi
 
Back
Top Bottom