Ubaguzi ni sera mpya ya CCM mpya, tunagawanywa kwa misingi ya dini, ukabila, ukanda na uvyama

  • Thread starter Return Of Undertaker
  • Start date
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,345
2,000
UBAGUZI SERA MPYA CCM

1. Utangulizi

Mbegu ya ubaguzi ilipandwa na ccm ya serikali ya awamu ya 4 na imechipua awanu ya 5.

2. Ubaguzi wa ccm ulianza miaka ya 2010 - 2015

Wakati wa serikali ya JK, umoja wa vijana wa ccm mkoa wa pwani ulianza ubaguzi kwa kusema rais wa awamu ya 5 hawezi kutoka kaskazini. Kabla ya kipindi hicho, sera ya ccm ilikuwa mgombea wa kiti cha urais anaweza katoka sehemu yo yote ya Tanzania. Hakuna kiongozi ye yote wa ccm aliyekemea hizo kauli za uvccm wakati huo na kwa hivyo ziliendelea kushamiri hadi kwenye uchaguzi mkuu 2015.

3. Ubaguzi haukuwepo ccm ya Mwalimu Nyerere

Mwalimi aliuchukia ubaguzi moyoni na kwa vitendo. Sera ya ccm ilikuwa ni kuweka uwiano kati ya makabila/mikoa kwenye kugawa raslimali na kwenye kutoa fursa mbalimbali. Mwalimu aliuchukia ubaguzi na kwa hivyo tabia ya kupandikiza chuki za kikabila na kikanda hazikuwepo.

4. Dalili ubaguzi wa kikabila miaka ya 1990 - 1995

Dalili za ubaguzi wa kikabila zilianza kujitokeza miaka ya 1990 - 1995 lakini Mwalimu alizikemea vikali hizo tabia. Dalili hizo zilikuwa ni kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 1995. Mwalimu aliweka msimamo kuwa kama mgombea ana sifa/vigezo, ateuliwe kuwa mgombea urais hata kama kabila lake ni Mkara. Aliwaasa ccm kutomteua mgombea wa kiti cha urais kwa msingi wa ukabila au uZanzibari bali waangalie sifa tu. Alisema kuzingatia kabila au eneo badala ya sifa za mgombea na vigezo husika ni kufanya dhambi kubwa.

5. Ubaguzi wakati wa kampeni chaguzi mkuu 2015.

Ubaguzi wa kikanda na kikabila ulikuwa silaha ya kuwashawishi wapiga kura wa kanda ya ziwa wamchague mgombea urais kwa tiketi ya ccm na sio Edward Lowassa wa chadema. Kipindi hicho ndipo chuki dhidi ya wachagga zilipandikizwa. Ilikuwa ni kete ya wana ccm kuwashawishi wasukuma kuwa wachagga hawafai kuongoza Tanzania maana wao ni wezi. Kipindi hicho Lowasa na wote wa kanda ya kaskazini walihesabika ni wachagga.

Ushawishi huo umewafanya baadhi ya wananchi wenye uelewa mdogo waamini kuwa ni kweli wachagga wezi. Wengine wameaminishwa kuwa kuna uhuhusiano kati ya I maskini wao na utajiri wa wachagga.

6. Sura xa ubaguzi katika awamu ya 5

Yanayoendelea nchini ni muendelezo wa sera mpya ya ccm maana tokea Tanganyika ipate Uhuru mwaka 1961, ndio mara ya kwanza sasa kaskazini wanaambiwa maendeleo yao inabidi yasubiri kwanza. Ugawaji wa bajeti kwa uwiano sasa basi. Kwa mtazamo wa watawala wa sasa, hakuna tena haja ya uwiano katika kugawa bajeti ya taifa.

Uteuzi wa viongozi mbalimbali na ajira katika ngazi mbalimbali serikalini hazingatii uwiano wa kimkoa kama zamani. Pamoja na kuwa wachagga ndiyo wanaongoza kwa usomi nchini lakini wao ndiyo wenye uwakilishi mdogo zaidi serikalini.

Kaskazini ina majimbo mengi yanayoongozwa na wabunge wa upinzani na mara nyingi viongozi wa ccm walisikika wakisema majimbo hayo ya wapinzani siyo kipaumbele cha serikali ya sasa kupeleka maendeleo. Majimbo yanayoongozwa na wabunge ccm ndiyo yanapewa kipaumbele.

7. Ugomvi kuwania madaraka chanzo cha ubaguzi wa kikabila/kikanda ndani ya ccm

Ccm ya serikali ya awamu ya 4 ilicheza kete ya ukanda kama silaha ya kumthihiti Lowassa asiwe mgombea urais kwa tiketi ya ccm. Hakuna katika viongozi wa ccm aliyetafakari madhara ya muda mrefu ya kauli zao hizo za kibaguzi. Kuwa wanapandikiza mbegu za chuki miongoni mwaka makabila/kanda mbalimbali za Tanzania hilo wao hawakujali.

Awamu ya 5 inaenda mbali zaidi kwa kusema wachagga ni bahili. Kiongozi mkubwa wa serikali anapotoa kauli kama hiyo inakuwa ni msimamo wa serikali hadi hapo kauli hiyo itakapokanwa na ngazi ya juu zaidi ya serikali.

8. Hitimisho

Umoja na mshikamano wa watanzania ulijengwa na baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwa jasho, muda na raslimali nyingi. Tukemee ubaguzi wa aina yo yote maana utavuruga amani, upendo na mshikamano wa kitaifa. Amani ikivurugika na maendeleo nayo pia hurudi nyuma.

Mungu ibariki Tanzania ili viongozi wasiwe wabaguzi.
 
P

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,278
2,000
Sheikh Suleiman Takdeer alikemea wakati tupo ‘shambani ‘ tunapanda ubaguzi 1958 leo imepita miaka 61 ndio tunastuka eti Mbegu inapandwa wakati Jiti zaid ya Mbuyu limeshakomaa

Ubaguzi ukikomaa unatoka upande mmoja kwenda mwingine

Mkibagua Wakristo mkibaki peke yenu mtakuta kuna Mndengereko na Mzaramo

Mkibagua Wakristo mkibaki peke yenu mtakuta kuna Wamachame na Wakaoromije

Burundi kwa Nkuruzinza sasa hivi wana parurana Wahutu kwa Wahutu na Rwanda wanaparurana Watutsi kwa Watutsi
 
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
1,925
2,000
Hahaha! Ndiko kuna wasomi wengi?
 
Top Bottom