Kigodoro-kantangaze

Kigodoro-kantangaze

michepuko

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2014
Posts
1,192
Reaction score
346
Binafsi sio mpenzi wa filamu za kiswahili hasa kutoka Bongo movie,Nimebahatika kuitaza filamu hii ya kigodoro-kantangaze na kunifanya niamini ni moja kati ya filamu bora kabisa za kitanzania kuwai kutenegenzwa,ni filamu ya ki Tanzania iliyoongozwa na mwanadada Zamaradi Mketema,ikiwa ina akisi maudhui halisi kabisa ya maisha ya watanzania wengi maskini wanaoishi uswahilini,Kwa wewe uliyefanikiwa kuiona filamu hii unaizungumziaje?
 
Ngoja nimuulize hausegirl wangu hapa maana wao ndo watazamaji wa ujinga wa Bongo movie.

Nadhani kazi ya great thinkers ni kutoa maoni na kurekebisha huo unaouita 'ujinga', back to the point nami niliambiwa na kuitafuta na kuiona. Inaelezea maisha halisi ya mitaani ambayo kuna asilimia kubwa ( significant number ) tu ya watu inaishi. Kuna mambo mengi sana ya kujifunza ambayo nina hakika wengi wetu tulikuwa/ hatuyafahamu na huenda yakahitaji hata interventions kadhaa. nawashauri viongozi wanaopita kwenye mitandao waiangalie maaana najua wao hawana 'fursa' ya kuyajua maisha na mambo yaliyoigizwa kwenye movie hiyo! Nashauri usimwulize HG wako atakueleza kwa mtazomo wake yeye. Angalia mwenyewe kwani unaweza kuwapa moyo au hata kuwafundisha waandaaji wengine ili kuepuka hizo movie unazoziita za ' kijinga'.
 
Yaani mtu mzima na akili zako pengine msomi kiasi ufundishwe maisha kwa utakayoyaona kwenye bongo movie?
Nani kwanza wa kukupa hayo mafunzo
Iren Uwoya?
Rose Ndauka?
Johari? Ray? Mainda? Lulu? Tuache masikhara tusichukululie maisha kua ni simple kiasi hicho.
 
Q. what is life?
A. Life is simple...eat, drink and watch bongo movies.
 
Yaani mtu mzima na akili zako pengine msomi kiasi ufundishwe maisha kwa utakayoyaona kwenye bongo movie?
Nani kwanza wa kukupa hayo mafunzo
Iren Uwoya?
Rose Ndauka?
Johari? Ray? Mainda? Lulu? Tuache masikhara tusichukululie maisha kua ni simple kiasi hicho.

Bora hata umenisaidia ndugu yangu.
 
Binafsi sio mpenzi wa filamu za kiswahili hasa kutoka Bongo movie,Nimebahatika kuitaza filamu hii ya kigodoro-kantangaze na kunifanya niamini ni moja kati ya filamu bora kabisa za kitanzania kuwai kutenegenzwa,ni filamu ya ki Tanzania iliyoongozwa na mwanadada Zamaradi Mketema,ikiwa ina akisi maudhui halisi kabisa ya maisha ya watanzania wengi maskini wanaoishi uswahilini,Kwa wewe uliyefanikiwa kuiona filamu hii unaizungumziaje?

Ndugu nilitaka nikae kimya lakini nimeona niseme tu, kwa ninavyojua mimi great thinkers hawawezi kufuatilia kazi za wasanii hawa wa bongo movie ambazo nyingi zinaandikwa, kuandaliwa na watu wenye upeo mdogo sana wa kufikiri na maarifa, hivyo ukimpelekea mtu anae think outside the box ataishia kudharau na kukaa kimya, haziwez kuongoza akili kubwa kwa kuifikirisha au kuifunza kwa sababu zipo hovyo hovyo, ndo maana mkuu mmoja hapo juu amechangia kwa kusema ye huwa kwake anaziangalia hosegirl wake, bongo movies ""wanaigiza huku wanaigiza na wanaigiza hovyo hovyo""
 
Filamu nzuri, imeakisi maisha halisi ya uswahilini, wahusika wamevaa uhalisia hasa.
Hao wanaoponda waezaliwa posta na kukulia America....hahahaaaaa kantangazeeeeee!
 
niazime na mimi

Njoo chukue kwangu.
Kuna kichwa hicho kinaitwa Mama Sikujua ni nomaaa. Ila Hemedi na Kajala wametuangusha yaani wameshindwa kureflect maisha ya uswazi. Otherwise sina utaalamu wa video sijui kama iko poa au vipi lakini in short hutokaa uboreke ukiwa unaangalia.
 
Back
Top Bottom