GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,190
- 10,316
Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu, Jaji Mstaafu Mathew Maimu, anamtuhumu mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kuwa alivuka mipaka kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya mkazi wa Arusha aitwaye Kalisti aliyeuziwa nyumba ya milioni hamsini kwa mkopo wa shilingi milioni tatu.
Mkopo huo aliuchukua Kijenge RC Saccos, na alikuwa akiendelea na marejesho pindi alipouziwa nyumba yake.
Katika clips za video nitakazoziweka humu muda si mrefu, Makonda anaonekana kukazia uamuzi uliokuwa umekwishachukuliwa na Jeshi la Polis. Polisi walikuwa wameshamkamata mtuhumiwa, kwa hiyo kauli ya Makonda ilikuwa ni ya kukazia tu, siyo yeye "aliyeinitiate" agizo la kukamatwa kwa huyo mtu ambaye jina lake limehifadhiwa.
Kama tume ya haki za binadamu inaridhika kuwa Makonda alikiuka miiko ya kazi yake, kwa nini wasimsaidie mlalamikaji kufungua kesi ya madai?
Inawezekana ni kweli Makonda alikosea, lakini tume inafanya inayoyafanya kwa nia njema ya kulisaidia Taifa au kuna agenda ya siri nyuma ya pazia?